settings icon
share icon
Swali

Je! Tunaweza kujifunza nini kutokana na maisha ya Musa?

Jibu


Musa ni mtu mmoja maarufu zaidi katika Agano la Kale. Wakati Ibrahimu anaitwa "Baba wa Waaminifu" na mpokeaji wa agano la Mungu lisilo na masharti la neema kwa watu Wake, Musa alikuwa mtu aliyechaguliwa kuleta ukombozi kwa watu Wake. Mungu hasa alimchagua Musa kuwaongoza Waisraeli kutoka utekaji nyara katika Misri hadi wokovu katika Nchi ya Ahadi. Musa pia anajulikana kama mpatanishi wa Agano la Kale na hujulikana sana kama mtoaji wa Sheria. Hatimaye, Musa ndiye mwandishi mkuu wa Torati, vitabu vya msingi vya Biblia nzima. Jukumu la Musa katika Agano la Kale ni aina na kivuli cha jukumu la Yesu katika Agano Jipya. Kwa hivyo, maisha yake ni ya thamani kuchunguza.

Tunakutana na Musa mara ya kwanza katika sura za ufunguzi wa kitabu cha Kutoka. Katika sura ya 1, tunajifunza kwamba, baada ya mzee Yusufu kuokomboa familia yake kutokana na njaa kubwa na kuiweka katika nchi ya Gosheni (katika Misri), wazao wa Ibrahimu waliishi kwa amani kwa vizazi kadhaa hadi akainuka farao kutawala Misri ambaye "hakumjua Yusufu" (Kutoka 1:8). Farao huyu alitawala watu wa Kiebrania na kuwatumia kama watumwa kwa ajili ya miradi yake mikubwa ya ujenzi. Kwa sababu Mungu aliwabariki watu wa Kiebrania na ukuaji wa haraka wa idadi, Wamisri walianza kuogopa idadi inayoongezeka ya Wayahudi wanaoishi katika nchi yao. Hivyo, Farao aliamuru kifo cha watoto wote wa kiume waliozaliwa na wanawake wa Kiebrania (Kutoka 1:22).

Katika Kutoka 2, tunaona mamake Musa akijaribu kumwokoa mtoto wake kwa kumtia katika kikapu na kumweka katika Nile. Kikapu hicho hatimaye kilipatikana na binti ya Farao, naye akamchukua kama wake mwenyewe na akamleta katika kasri ya farao mwenyewe. Musa alipokuwa mtu mzima, alianza kuhisi na taabu ya watu wake, na baada ya kushuhudia Mmisri akimpiga mtumwa wa Kiebrania, Musa aliingilia na kumwua Mmisri. Katika tukio lingine, Musa alijaribu kuingilia kati katika mabishano kati ya Waebrania wawili, lakini mmoja wa Waebrania alimkemea Musa na kusema kwa kejeli, "Je! Wataka kuniua mimi kama ulivyomwua yule Mmisri?" (Kutoka 2:14). Alipotambua kwamba tendo lake la uhalifu limefahamika, Musa alikimbia kwenda nchi ya Midiani ambapo aliingilia tena-wakati huu akimwokoa binti ya Yethro kutoka kwa maharamia wengine. Kwa shukrani, Yethro (pia aitwaye Reueli) alimpa binti yake Sipora kwa Musa katika ndoa (Kutoka 2:15-21). Musa aliishi Midiani kwa takribani miaka arobaini.

Tukio lingine kubwa katika maisha ya Musa lilikuwa kukutana kwake na Mungu kwenye kichaka cha moto (Kutoka 3-4), ambapo Mungu alimwita Musa kuwa mwokozi wa watu Wake. Licha ya udhuru wake wa awali na ombi la wazi kwamba Mungu atume mtu mwingine, Musa alikubali kumtii Mungu. Mungu aliahidi kumtuma Haruni, nduguye Musa, pamoja naye. Hadithi nyingine yote inajulikana vizuri. Musa na ndugu yake, Haruni, walienda kwa Farao katika jina la Mungu na kutaka kwamba awaachilie watu kwenda kumwabudu Mungu wao. Farao anakataa kwa kiburi, na mateso kumi ya hukumu ya Mungu yaliwaangukia watu na nchi, dhiki ya mwisho ni kuuawa wa mzaliwa wa kwanza. Kabla ya dhiki hii ya mwisho, Mungu anamwaagiza Musa kuanzisha Pasaka, ambayo ni kumbukumbu ya tendo la Mungu la kuokoa katika kuwakomboa watu Wake kutoka utumwa huko Misri.

Baada ya kutoka, Musa aliwaongoza watu kwenye ukingo wa Bahari ya Shamu ambapo Mungu alitoa muujiza mwingine wa kuokoa kwa kugawanya maji na kuruhusu Waebrania kuvuka kwa upande mwingine huku akizamisha jeshi la Misri (Kutoka 14). Musa aliwaleta watu kwenye mguu wa Mlima Sinai ambapo Sheria ilitolewa na Agano la Kale lilianzishwa kati ya Mungu na taifa jipya lilofanyika la Israeli (Kutoka 19-24).

Sehemu nyingine ya kitabu cha Kutoka na kitabu kizima cha Mambo ya Walawi kinafanyika wakati Waisraeli wamepiga kambi chini ya Sinai. Mungu anampa Musa maelekezo ya kina kwa ujenzi wa hema-hema ya kuhamisha ya ibada ambayo ingeweza kuunganishwa na kutenganishwa kwa kubebeka urahisi-na kwa ajili ya kufanya vyombo vya ibada, vazi la ukuhani, na sanduku la agano, mfano wa uwepo wa Mungu kati ya watu Wake pamoja na mahali ambapo kuhani mkuu angefanya upatanisho wa kila mwaka. Mungu pia anampa Musa maelekezo ya wazi kuhusu jinsi Mungu anapaswa kuabudiwa na miongozo ya kudumisha usafi na utakatifu kati ya watu. Kitabu cha Hesabu kinaona Waisraeli wakiondoka Sinai hadi mpaka wa Nchi ya Ahadi, lakini wakakataa kuingia wakati wapelelezi kumi kati ya kumi na mbili walileta ripoti mbaya kuhusu uwezo wa Israeli kuchukua nchi. Mungu anahukumu kizazi hiki cha Wayahudi kufa katika jangwa kwa sababu ya kutotii na kuwaadhibu kwa miaka arobaini ya kuzunguka jangwani. Mwishoni mwa kitabu cha Hesabu, kizazi kijacho cha Waisraeli kinarudi kwenye mipaka ya Nchi ya Ahadi na kujiamini kutegemea Mungu na kuichukua kwa imani.

Kitabu cha Kumbukumbu la Torati kinaonyesha Musa akitoa hotuba kadhaa kama mahubiri kwa watu, akiwakumbusha nguvu za kuokoa na uaminifu wa Mungu. Anatoa usomaji wa pili wa Sheria (Kumbukumbu la Torati 5) na kuandaa kizazi hiki cha Waisraeli kupokea ahadi za Mungu. Musa mwenyewe anazuiwa kuingia nchi kwa sababu ya dhambi yake huko Meriba (Hesabu 20:10-13). Mwishoni mwa kitabu cha Kumbukumbu la Torati, kifo cha Musa kinaandikwa (Kumbukumbu la Torati 34). Alipanda Mlima Nebo na kuruhusiwa kutazama Nchi ya Ahadi. Musa alikuwa na umri wa miaka 120 alipokufa, na Biblia inasema kwamba "jicho lake halikupofuka, wala nguvu za mwili wake hazikupunguka" (Kumbukumbu la Torati 34:7). Bwana mwenyewe alimzika Musa (Kumbukumbu la Torati 34:5-6), na Yoshua akachukua hatamu kama kiongozi wa watu (Kumbukumbu la Torati 34:9). Kumbukumbu la Torati 34:10-12 linasema, "Wala hajainuka tena katika Israeli nabii kama Musa, ambaye BWANA alimjua uso kwa uso; katika ishara zote na maajabu yote, ambayo BWANA alimtuma kuyatenda katika nchi ya Misri, kwa Farao, na kwa watumishi wake wote, na kwa nchi yake yote; na katika ule mkono wa nguvu wote, tena katika ule utisho mkuu wote, alioutenda Musa machoni pa Israeli wote."

Yaliyo hapo juu ni madokezo mafupi ya maisha ya Musa na hayazungumzii juu ya kuingiliana kwake na Mungu, namna ambayo aliwaongoza watu, baadhi ya njia maalumu ambazo alionyesha kivuli cha Yesu Kristo, umuhimu wake kwa imani ya Kiyahudi, mwonekano wake katika kubadilika kwa Yesu, na maelezo mengine. Lakini haitupi mfumo wa mtu. Hivyo, sasa, tunaweza kujifunza nini kutokana na maisha ya Musa? Maisha ya Musa kwa ujumla yamevunjwa katika vipindi vitatu vya miaka 40. Kwanza ni maisha yake katika ua la Farao. Kama mtoto aliyeasiliwa wa binti ya Farao, Musa angekuwa na marupurupu na faida zote za mwana mfalme wa Misri. Alifundishwa "kwa hekima yote ya Wamisri, akawa hodari wa maneno na matendo" (Matendo 7:22). Kama taabu za Waebrania zilianza kuvuruga nafsi yake, Musa alijiamulia mwenyewe kuwa mwokozi wa watu wake. Kama Stefano anasema mbele ya baraza la utawala wa Kiyahudi, "[Musa] alidhani kwamba ndugu zake watafahamu ya kuwa Mungu anawapa wokovu kwa mkono wake" (Matendo 7:25). Kutokana na tukio hili, tunajifunza kwamba Musa alikuwa mtu wa vitendo pamoja na mtu mwenye hasira kali na maamuzi ya haraka ya mara kwa mara. Je, Mungu alitaka kuokoa watu Wake? Ndiyo. Je! Mungu alitaka kutumia Musa kama chombo Chake kilichochaguliwa kwa wokovu? Ndiyo. Lakini Musa, ikiwa kweli alifahamu au la jukumu lake katika wokovu wa watu wa Kiebrania, alifanya kwa haraka na kwa nguvu. Alijaribu kufanya kwa wakati wake kile Mungu alitaka kifanywe kwa wakati Wake. Somo kwetu ni la kawaida: tunapaswa kuwa na ufahamu wa kutofanya tu mapenzi ya Mungu, bali kufanya mapenzi ya Mungu kwa wakati wake, sio wetu. Kama ilivyo na mifano mingi ya kibiblia, tunapojaribu kufanya mapenzi ya Mungu kwa wakati wetu, tunafanya makosa kubwa zaidi kuliko walivyokuwa hapo awali.

Musa alihitaji muda wa kukua na kukomaa na kujifunza kuwa mpole na mnyenyekevu mbele ya Mungu, na hii inatuleta kwenye sura inayofuata katika maisha ya Musa, miaka 40 katika nchi ya Midiani. Wakati huu, Musa alijifunza maisha rahisi ya mchungaji, mume, na baba. Mungu alichukua kijana mwenye hasira kali na mwenye uamuzi wa haraka na kuanza mchakato wa kumfinyanga na kumuunda kuwa chombo kamili cha Mungu kutumia. Tunaweza kujifunza nini kutoka wakati huu katika maisha yake? Ikiwa somo la kwanza ni kusubiri wakati wa Mungu, somo la pili ni tusiwe wavivu wakati tunapongojea wakati wa Mungu. Wakati Biblia haitumii muda mwingi juu ya maelezo ya sehemu hii ya maisha ya Musa, sio kama Musa alikuwa ameketi bila kujali kwa kusubiri wito wa Mungu. Alitumia sehemu bora zaidi ya miaka 40 kujifunza njia za mchungaji na kukimu na kukuza familia. Hizi sio vitu vichache! Wakati tunaweza kutamani uzoefu wa "kilele cha mlima" na Mungu, asilimia 99 ya maisha yetu yanaishiwa katika bonde kufanya kidunia, mambo ya kila siku ambayo hufanya maisha. Tunahitaji kuishi kwa ajili ya Mungu "katika bonde" kabla ya Yeye kutusaidia katika vita. Mara nyingi katika vitu vinavyoonekana visivyo na maana sana ambavyo Mungu hutufundisha na kututayarisha kwa mwito Wake katika msimu ujao.

Kitu kingine tunachoona kutoka kwa Musa wakati wa muda alitumia huko Midiani ni kwamba, wakati Mungu alipomwita hatimaye kwa huduma, Musa alikuwa mpinzani. Mtu wa hatua mapema katika maisha yake, Musa, sasa mwenye umri wa miaka 80, akawa na hofu kubwa. Wakati alipoulizwa kuzungumza kwa Mungu, Musa alisema alikuwa "si mwepesi wa hotuba na ulimi ulikuwa mzito" (Kutoka 4:10). Watoa maoni wengine wanaamini kwamba Musa anaweza kuwa na kikwazo cha kuzungumza. Pengine, lakini basi itakuwa kinyume kwa Stefano kusema Musa alikuwa "mwenye nguvu kwa maneno na matendo" (Matendo 7:22). Pengine Musa hakutaka tu kurudi Misri na kushindwa tena. Hii si hisia isiyo ya kawaida. Ni wangapi wetu wamejaribu kufanya kitu (ikiwa ni kwa ajili ya Mungu au la) na kushindwa, na kisha kusita kujaribu tena? Kuna mambo mawili Musa alionekana kutotilia maani. Moja ilikuwa mabadiliko ya wazi ambayo yalitokea katika maisha yake katika kipindi cha miaka 40. Nyingine, na muhimu zaidi, mabadiliko ni kwamba Mungu angeweza kuwa pamoja naye. Musa alishindwa kwa mara ya kwanza sio kwa sababu alitenda kwa musukumo, lakini kwa sababu alitenda bila Mungu. Kwa hivyo, somo la kujifunza hapa ni kwamba unapotambua wito wazi kutoka kwa Mungu, enda mbele kwa imani, ukijua kwamba Mungu huenda pamoja nawe! Usiogope, lakini kuwa na nguvu katika Bwana na katika nguvu ya uwezo wake (Waefeso 6:10).

Sura ya tatu na ya mwisho katika maisha ya Musa ni sura ambayo Maandiko hutumia muda mrefu Zaidi kuandika, yaani, jukumu lake katika ukombozi wa Israeli. Masomo kadhaa yanaweza kupatikana kutoka sura hii ya maisha ya Musa pia. Kwanza ni jinsi ya kuwa kiongozi wa kufaa wa watu. Kimsingi Musa alikuwa na wajibu juu ya wakimbizi milioni mbili wa Kiebrania. Wakati vitu vilianza kumchosha, baba mkwewe, Yethro, alipendekeza kwamba awape wajibu kwa wanaume wengine waaminifu, somo ambalo watu wengi wenye mamlaka juu ya wengine wanahitaji kujifunza (Kutoka 18). Tunaona pia mtu ambaye alitegemea neema ya Mungu ili kusaidia na kazi yake. Musa alikuwa akiendelea kuomba kwa niaba ya watu mbele ya Mungu. Ingekuwa kwamba watu wote wenye mamlaka wangeweza kuomba Mungu kwa niaba ya wale ambao wanasimamia! Musa alikuwa anafahamu sana kwa umuhimu wa uwepo wa Mungu na hata aliomba kuona utukufu wa Mungu (Kutoka 33). Musa alijua kwamba, mbali na Mungu, kutoka ingekuwa hauna maana. Alikuwa Mungu ambaye aliwafanya Waisraeli tofauti, na walimhitaji Yeye zaidi. Maisha ya Musa pia yanatufundisha somo kwamba kuna dhambi fulani ambazo zitaendelea kutuchukiza katika maisha yetu yote. Hasira hiyo hiyo kali ambayo ilimwingiza Musa kwa shida huko Misri pia alimtia kwa shida wakati wa kuzunguka jangwani. Katika tukio lililotajwa hapo awali huko Meriba, Musa alipiga mwamba kwa hasira ili kutoa maji kwa ajili ya watu. Hata hivyo, hakumpa Mungu utukufu, wala hakufuata amri sahihi ya Mungu. Kwa sababu hii, Mungu alimzuia kutoka kuingia katika Nchi ya Ahadi. Kwa namna hiyo hiyo, sisi sote tunakabiliwa na dhambi za kudumu ambazo zinatukera siku zetu zote, dhambi ambazo zinatuhitaji kuwa tahadhari daima.

Kuna masomo machache tu ambayo tunaweza kujifunza kutokana na maisha ya Musa. Hata hivyo, ikiwa tunatazama maisha ya Musa kulingana na deraya ya jumla ya Maandiko, tunaona ukweli mkubwa wa kiteolojia ambao unaofaa katika hadithi ya ukombozi. Katika sura ya 11 mwandishi wa Waebrania anatumia Musa kama mfano wa imani. Tunajifunza kwamba ilikuwa kwa imani kwamba Musa alikataa utukufu wa kasri la Farao ili kutambua na taabu ya watu wake. Mwandishi wa Waebrania anasema, "[Musa] kushutumiwa kwake Kristo ni utajiri mkuu kuliko hazina za Misri" (Waebrania 11:26). Maisha ya Musa yalikuwa moja ya imani, na tunajua kwamba bila imani haiwezekani kumpendeza Mungu (Waebrania 11:6). Vivyo hivyo, ni kwa imani kwamba sisi, tunatarajia utajiri wa mbinguni, tunaweza kuvumilia shida za muda katika maisha haya (2 Wakorintho 4:17-18).

Kama ilivyoelezwa hapo awali, pia tunajua kwamba maisha ya Musa yalikuwa uainishi wa maisha ya Kristo. Kama Kristo, Musa alikuwa mpatanishi wa agano. Tena, mwandishi wa Waebrania huenda kwa urefu mkubwa kuonyesha jambo hili (tazama Waebrania 3; 8-10). Mtume Paulo pia hufanya hoja sawa katika 2 Wakorintho 3. Tofauti ni kwamba agano ambalo Musa alipatanisha lilikuwa la muda na la masharti, wakati ambapo agano ambalo Kristo anapatanisha ni la milele na lisilo na masharti. Kama Kristo, Musa alitoa ukombozi kwa watu wake. Musa aliwaokoa watu wa Israeli kutoka utumwa na minyororo ya dhambi huko Misri na kuwaleta katika Nchi ya Ahadi ya Kanaani. Kristo huwaokoa watu Wake kutoka utumwa na minyororo ya dhambi na kuwahukumu na kuwaleta katika Nchi ya Ahadi ya uzima wa milele katika ulimwengu mpya wakati Kristo atakaporudi kukamilisha Ufalme Yeye alizindua katika kuja Kwake kwa mara ya kwanza. Kama Kristo, Musa alikuwa nabii kwa watu wake. Musa aliongea maneno ya Mungu kwa Waisraeli kama vile Kristo alivyofanya (Yohana 17:8). Musa alitabiri kwamba Bwana angeinua nabii mwingine kama yeye kutoka miongoni mwa watu (Kumbukumbu la Torati 18:15). Yesu na kanisa la kwanza walifundisha na kuamini kwamba Musa alikuwa akizungumza juu ya Yesu wakati aliandika maneno hayo (tazama Yohana 5:46, Matendo 3:22, 7:37). Kwa njia nyingi, maisha ya Musa ni mtangulizi wa maisha ya Kristo. Kwa hivyo, tunaweza kupata maelezo mafupi ya jinsi Mungu alivyofanya mpango Wake wa ukombozi katika maisha ya watu waaminifu katika historia ya mwanadamu. Hii inatupa tumaini kwamba, kama vile Mungu alivyowaokoa watu Wake na kuwapa pumziko kupitia matendo ya Musa, hivyo, pia, Mungu atatuokoa na kutupa pumziko la Sabato ya milele katika Kristo, sasa na katika maisha ijayo.

Hatimaye, ni jambo la kupendeza kufahamu kuwa, ingawa Musa hakuingia katika Nchi ya Ahadi wakati wa maisha yake, alipewa fursa ya kuingia katika Nchi ya Ahadi baada ya kifo chake. Juu ya mlima wa mageuzo, wakati Yesu aliwapa wanafunzi wake dhuku ya utukufu Wake kamili, alikuwa akifuatana na watu wawili wa Agano la Kale, Musa na Eliya, ambao waliwakilisha Sheria na Manabii. Musa, leo, anapata mapumziko ya Sabato ya kweli katika Kristo kwamba siku moja Wakristo wote watashiriki (Waebrania 4:9).

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Tunaweza kujifunza nini kutokana na maisha ya Musa?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries