settings icon
share icon
Swali

Lazaro alikuwa katika Biblia?

Jibu


Kuna watu wawili wanaoitwa Lazaro katika Biblia. Lazaro wa kwanza yupo katika hadithi anayosimuliwa na Yesu (Luka 16: 19-31). Lazaro alikuwa maskini sana, labda hakuwa na makao na alikuwa mwenye kuombaomba (Luka 16:20). Mara nyingi alikaa kwenye lango la mtu tajiri kwa matumaini ya kupata makombo kutoka meza yake. Wanaume hao wawili walikufa, na Yesu anasema jinsi Lazaro alivyochukuliwa na malakika "kifuani cha Ibrahimu," mahali pa faraja na kupumzika, wakati mtu tajiri alienda"kuzimu," mahali pa maumivu na mateso (Luka 16: 22-23). Baadhi ya wasomi wa Biblia wanaamini kwamba Yesu alikuwa anapatiana mfano tu, yaani, hadithi ya isiyo ya ukweli. Hata hivyo, Yesu hutumia majina halisi katika hadithi, haitafsiri hadithi, wala haongezi maadili yanayowekwa wazi katika hadithi hio. Anawacha hadithi kujieleza yenyewe. Kwa sababu ya maelezo haya, hadithi ya Lazaro na tajiri inaweza kuwa tukio la kweli, inayoonyesha hatima halisi ya Lazaro na mtu tajiri asiyeamini. Kwa namna yoyote ile, mafundisho ya Yesu juu ya ukweli wa mbingu na kuzimu ni wazi. Lazaro katika hadithi ya Yesu hajatajwa mahali pengine popote katika Biblia, na hatujui aliishi wakati gani katika historia, ikiwa alikuwa mtu halisi.

Lazaro wa pili, anayeitwa Lazaro wa Bethania, alikuwa ndugu wa Maria na Martha. Hawa ndugu watatu walikuwa marafiki na wanafunzi wa Yesu, na walipendwa na Yesu(Yohana 11: 5). Siku moja, ujumbe wa haraka uliletwa kwa Yesu kutoka Bethania: Rafiki yake Lazaro alikuwa mgonjwa, na Maria na Martha walitaka Yesu aje kumponya, kwa maana alikuwa karibu kufa. Yesu kisha akawashangaza wanafunzi na marafiki wake. Alianza kwa kusema kwamba ugonjwa huo si wa mauti, bali ni kwa ajili ya utukufu wa Mungu, ili Mwana wa Mungu atukuzwe. (Yohana 11: 4). Kisha Yesu akakaa siku mbili ambako alikuwa na baadaye alitaka kwenda Yudea, ambako Lazaro alikuwa na pia ambapo adui za Yesu walitaka kumuua kwa mawe muda mfupi tu uliopita(Yohana 11: 5-8). Wakati wa kuchelewa kwa Yesu, Lazaro alikufa, lakini Yesu alisema kuwa alikuwa "amelala" na kuwaambia wanafunzi kwamba angekwenda kumwamsha (Yohana 11:11). Wanafunzi walijibu, "Bwana, ikiwa analala, basi atapona," walidhani kuwa Yesu alisema juu ya usingizi wa kimwili (Yohana 11:12). Kisha Yesu akawaambia waziwazi kwamba Lazaro alikufa, lakini bado walienda kumwona (Yohana 11:14). Tomasi anafafanua kikamilifu kuchanganyikiwa kwa wanafunzi kwa kusema, "Na tuende, ili tupate kufa pamoja naye" (Yohana 11:16) — aliona kwamba Yesu alikuwa na uhakika, lakini alijua hatari za safari hiyo (Yohana 11: 8).

Walipofika nyumbani kwa Lazaro huko Bethania, walimwona Maria na Martha wakiwa na huzuni. Walikuwa washamzika ndugu yao siku nne mbeleni. Yesu hakuja kuwasaidia. Walikuwa wamechanganyikiwa na kufadhaika, lakini imani yao katika Yesu ilikuwa imara (Yohana 11: 17-36). Kila kitu kikawa wazi wakati Yesu alifanya kile hakikutarajiwa: Alikwenda kwenye kaburi ambamo Lazaro alikuwa amelazwa na kumfufua kutoka wafu (Yohana 11: 43-44).

Tukio lote la ugonjwa wa Lazaro, kifo, na ufufuo vilifanyika ili kumtukuza Mungu na kuongeza imani ya wafuasi wa Yesu, kama vile Yesu alivyokwishasema wakati aliposikia kuhusu ugonjwa wa Lazaro. Kabla ya kumfufua Lazaro, Yesu aliomba, "Baba, nakushukuru kwa kuwa umenisikia. Nami nalijua ya kuwa wewe wanisikia sikuzote; lakini kwa ajili ya mkutano huu wanaohudhuria nalisema haya, ili wapate kusadiki kwamba ndiwe uliyenituma" (Yohana 11: 41-42). Sala ya Yesu ilijibiwa: Lazaro akafufuka, na "Wayahudi waliokuja kwa Mariamu, na kuyaona yale aliyoyafanya, wakamwamini" (Yohana11: 45).

Yesu alipomwita Lazaro, Lazaro alitoka kaburini-sio mfu au nusu-mfu au asiye na uharibifu, bali mtu aliye hai na mzima. Nguvu kama hiiyo ni ya Kristo. Maandiko hayasemi kile Lazaro alichopitia wakati wa siku zake nne kaburini. Huwa tunadhani kwamba nafsi / roho yake ilikuwa paradiso, ambapo Lazaro mwingine alikuwa.

Baada ya Lazaro kufufuliwa kutoka wafu, makuhani wakuu na Mafarisayo walipanga kumwua, kwa sababu mashahidi wengi wa muujiza walimwamini Yesu (Yohana 12: 9-11). Maadui wa Kristo hawangeweza kukuataa muujiza; jambo la muhimu kwa mtazamo wao, ilikuwa ni kuharibu ushahidi-wa kesi hii, na ushahidi ulikuwa ni wa mtu aliyerejeshewa uhai, na anayepumua. Lakini hawangeweza kuzuia ukweli kutoka kuenea.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Lazaro alikuwa katika Biblia?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries