settings icon
share icon
Swali

Tunapaswa kujifunza nini katika maisha ya Isaya?

Jibu


Isaya, ambaye jina lake linamaanisha "Yahweh ni wokovu," anajulikana kwa kuandika kitabu kinachoitwa sawia na jina lake katika Agano la Kale. Maandishi yake ni ya muhimu sana kwa unabii aliofanya kuhusu kuja kwa Masihi, mamia ya miaka kabla ya kuzaliwa kwa Yesu (Isaya 7:14, 9: 1-7, 11: 2-4; 53: 4-7, 9, 12) . Mathayo anukuu Isaya wakati anaelezea huduma ya Yohana Mbatizaji (Mathayo 3: 3; Isaya 40: 3), na wakati Yesu alihamia Galilaya kuanza huduma Yake, unabii wa Isaya ulitimizwa (Mathayo 4: 13-16, Isaya 9: 1-2) ). Yesu ananukuu unabii wa Isaya wakati akizungumza kwa mifano (Isaya 6: 9; Mathayo 13: 14-15), mtume Paulo pia anarejelea unabii huo huo wakati akiwa Roma (Matendo 28: 26-27). Wakati Yesu anasoma kutokakitabu cha Isaya (Isaya 61: 1-2) katika sinagogi ya Nazareti, Anawashangaza Wayahudi wengi kwa kudai unabii unatimizwa ndani yake (Luka 4: 16-21). Pia ni ya kushangaza kutambua kwamba vitabu vya Injili vinanukuu zaidi kutoka kwa maandishi ya Isaya kuliko kutoka kwa manabii wengine wowote wa Agano la Kale.

Machache tu yameandikwa kuhusu Isaya. Tunajua kwamba alikuwa mwana wa Amozi na kwamba alioa na kuwa na wana wake mwenyewe (Isaya 1: 1; 7: 3; 8: 3). Ingawa kutambulika kwa Isaya kama nabii mkuu kama inavyoonekana katika vitabu vya Wafalme na Mambo ya Nyakati, inawezekana pia kuwa alikuwa kuhani, kwa kuwa wito wake kutoka kwa Mungu ulifanyika hekaluni (Isaya 6: 4), eneo ambalo lilitengwa tu kwa makuhani. Upako anaopokea katika wito wake ni sawa na ule wa nabii Yeremia (Yeremia 1: 9; Isaya 6: 7).

Pamoja nabii Mika, mtume wake wa wakati huo, Isaya alitumikia ufalme wa kusini wa Yuda chini ya utawala wa wafalme wanne. Wakati wa huduma ya Isaya, Yuda ilikuwa taifa lenye dhambi na lisilo la haki. Hata hivyo, Isaya aliamini kuwa Yuda ilikuwa taifa lililochaguliwa na Mungu na lingeweza kutetewa na Mungu. Kupitia usaidizi wa Mika na Mfalme Hezekia aliyekuwa mha Mungu, maadui wao walishindwa na uamsho ulifanyika katika taifa la Yuda (2 Wafalme 19: 32-36; 2 Mambo ya Nyakati 32: 20-23). Wasemaji wengi wanaelezea Isaya kama mhubiri wa Yuda kwa sababu alifanya kazi juu chini ili kuwawezesha watu kumrudia Mungu.

Kulikuwa na mengi ya kufurahia na pia ya kuhuzunisha katika maisha ya Isaya. Alipata kutuzwa kupitia miujiza ya ajabu kwa sababu ya aminifu wake kwa Mungu. Katika jibu la sala ya Isaya, Mungu akakirudisha nyuma kile kivuli madaraja kumi, kama ishara kwa Mfalme Hezekia kwamba Mungu angeongeza miaka 15 kwa maisha ya Hezekia (2 Wafalme 20: 8-11; 2 Mambo ya Nyakati 32:24). Hata hivyo, kwa miaka mitatu Isaya alibaki uchi na bila viatu miguuni mwake, kwa kumtii Mungu, kama "ishara na ajabu" dhidi ya Wamisri (Isaya 20: 2-4). Mik pia alifanya vivyo hivyo (Mika 1: 8), ingawa hatuambiwi kwa muda gani.

Tunapata kumjua mtu vyema katika kuchunguza moyo wa wake. Yesu alisema kwamba kinywa cha mtu huyanena yaujazayo moyo wake. (Mathayo 12:34). Katika maandiko ya Isaya tunaona uaminifu wake imara na unyenyekevu wake kamili mbele ya Mungu. Pia alikuwa na heshima kubwa kutoka kwa mahakama ya Mfalme Hezekia na wenzake, ambayo ilikuwa dhahiri wakati wa mgogoro. Baadhi ya sanaa bora duniani, muziki na mashairi zimeundwa na watu ambao walitembea kwa ukaribu na Mungu, na Isaya ni baadhi yao. Umahiri wake wa lugha ya Kiebrania umelinganishwa na ule wa Kiingereza wa Shakespeare, kama tunavyosoma katika Isaya, baadhi ya maandishi mazuri zaidi katika Biblia. Ingawa kitabu cha Isaya kiliandikwa zaidi ya miaka 2,500 iliyopita, ni vyema kusoma kitabu kizima, kwa sababu ndani yake tunaona hekima nyingi ambazo zinatumika katika maisha yetu ya Kikristo leo.

Inaonekana kwamba Isaya alikuwa mtu mwenye siri sana. Tunapokutana na baadhi ya wasemaji maarufu wa leo kwa uso, tunaweza kuona kwamba wanaonekana kuwa wamejitenga na shughuli za wengine. Hata hivyo, sawia na Isaya, tunaona kwamba huduma yao inahusu kuwaelekeza watu kwa Mungu, ila sio kwao wenyewe. Na licha ya unyamavu wake, umaarufu wa Isaya unaonekana kupitia matokeo ya huduma yake kwa watu. Katika siku hizi za mwisho, tunahitaji kufanya chochote tunachozungumzia kiwe cha msaada kwa ufalme. Kutoka kwa maisha ya Isaya tunajifunza kwamba, wakati Mungu anatekeleza mpago Wake kupitia kwetu, tunapaswa kuhakikisha kwamba utukufu wote unakwenda kwake.

Zaidi ya hayo, inaonekana huduma ya Isaya ilikuwa na uhusiano wa karibu na watu wengine wa Mungu, kama vile Mika na Mfalme Hezekia. Kufanya huduma peke yetu mara nyingi kunaweza kutuacha katika mazingira magumu, lakini tunapounganishwa na wengine katika ushirika wa Kristo na Roho Mtakatifu kupitia ushirika na sala, huduma yetu huwa na ufanisi kwa sababu ya ulinzi wa wengine.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Tunapaswa kujifunza nini katika maisha ya Isaya?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries