settings icon
share icon
Swali

Ni nini tunaweza kujifunza kutoka kwa maisha ya Haruni?

Jibu


Haruni anajulikana sana kwa sababu ya jukumu lake katika kutoka na kwa kuwa wa kwanza wa Walawi, au Uharuni, ukuhani. Alizaliwa katika familia ya Walawi wakati wa utumwa wa Israeli kule Misri na alikuwa nduguye Musa mkubwa, alimshinda Musa miaka mitatu (Kutoka 7: 7). Haruni tunamwona mara ya kwanza katika Kutoka mlango wa 4 wakati Mungu anamwambia Musa kwamba atamtuma Haruni nduguye, kuandamana pamoja naye kwa kuwaokoa Waisraeli toka kwa Farao.

Waisraeli walibaki kule Misri baada ya Yusufu na kizazi chake kufa, na idadi yao ikaongezeka. Farao mpya aliyeingia mamlakani aliogopa kuwa Waisraeli wangewageuka Wamisri, kwa sababu hiyo akawawekea wasimamizi wa utumwa juu yao na kutekeleza sheria kali (Kutoka 1: 8-14). Pia aliwaamuru wakunga wa Kiebrania kuwaua watoto wote wachanga wa kiume pindi tu walipozaliwa. Wakati wakunga walikaidi amri, Farao akawaamuru watu wote kuwatupa watoto wote wa Kiume katika mto Nile. Sheria hizi zilikuwa zimekwisha tekelezwa kabla Musa kuzaliwa. Huenda Haruni alizaliwa kabla ya sheria, au kuponea kifo kwa sababu wakunga/wazalisha walimcha Mungu badala ya kumtii Farao (Kutoka 1: 15-22). Hatusomi chochote kumhusu Haruni hadi pale Mungu anamtuma kwa Musa aliyekuwa na umri wa miaka themanini.

Wakati Mungu alimsungumzia Musa kutoka katika kijiti kilichowaka moto, akimwita arejee kule Misri na kumsihi Farao awaachilie huru Waisraeli (Kutoka 3-4), Musa alitoa sababu za ni kwa nini yeye hakuwa chaguo bora kwa kazi hiyo. Mwishowe Musa alimsihi Mungu amtume mtu mwingine (Kutoka 4:13). Hapo hasira ya Bwana ikawaka juu ya Musa, akasema, "Je! Hayuko Haruni, ndugu yako, Mlawi? Najua ya kuwa yeye aweza kusema vizuri. Pamoja na hayo, tazama, anakuja kukulaki; naye atakapokuona, atafurahi moyoni mwake" (Kutoka 4:14). Mungu aliendelea na kumwambia Musa kwamba Haruni angekuwa msemaji wake (Kutoka 4: 15-17).

Mungu pia alisungumzia Haruni, na kumwambia akutana na Musa jangwani. Haruni kwa utii alienda. Musa akamwambia Haruni kile Mungu alikuwa amekwisha kisema, ikiwa ni pamoja na maagizo ya ishara watakazozifanya mbele ya Farao. Nchini Misri, Musa na Haruni waliwakusanya wazee wa Waisraeli, na Haruni akawaambia kile Mungu alichomwambia Musa (Kutoka 4: 27-31). Ni tukio la kuvutia kumbuka jinsi Haruni alivyoitikia wito wa Mungu kwa utiivu na jinsi alivyoamini kwa haraka kile Musa alichomwambia. Haruni alionekana kuwa tayari kwa kazi ambayo Mungu alimwita bila swali, kwa hiari alimsaidia nduguye kwa na kusungumza na watu kwa niaba yake. Pengine Haruni aliwahi kuwa kama mpatanishi kati ya Musa na Waisraeli, kwa sababu Musa alikuwa akikwisha ishi mbali na watu wake maisha yake yote-kwanza katika jumba la mfalme wa Misri na kisha kama mkimbizi huko Midiani.

Vile hadithi ya kutoka inavyojifunua, tunawaona wote waili Musa na Haruni mbele ya Farao, wakimwomba Farao kuwaachalia huru Waisraeli na walifanya ishara nyingi. Mungu alitumia fimbo ya Haruni katika ishara nyingi na mapigo. Wanaume waliitii amri za Mungu, na hatimaye Waisraeli walikombolewa.

Haruni aliendelea kuongoza pamoja na Musa wakati wa kurandaranda jangwa kwa Waisraeli, akihudumu kama msaidizi wake na msemaji. Waisraeli walipomnung'unikia Musa na Haruni (Kutoka 16: 2), "Musa na Haruni wakawaambia wana wote wa Israeli, Jioni ndipo mtakapojua ya kuwa Bwana amewaleta kutoka nchi ya Misri; na asubuhi ndipo mtakapouona utukufu wa Bwana; kwa kuwa yeye asikia manung'uniko yenu mliyomnung'unikia Bwana; na sisi tu nani, hata mkatunung'unikia?" (Kutoka 16: 6-8). Musa aliwaambia Haruni awakusanye watu pamoja na waje mbele za Bwana, na utukufu wa Bwana ulionekana juu yao katika wingu (Kutoka 16:10). Ilikuwa ni wakati huu kwamba Mungu aliwalisha kwa pishi la mana. Mungu alimwagiza Musa kuhifadhi kipande cha pishi ya mana kama kumbukumbu kwa vizazi vijavyo; Musa alimuuliza Haruni kuikusanya (Kutoka 16: 32-35).

Baada ya uasi wa Kora dhidi ya Musa na Haruni, Mungu alifanya muujiza ili kuthibitisha kuwa Haruni na uzao wake walikuwa wamechaguliwa kuhudumu mbele za uwepo wa Bwana. Fimbo kumi na mbili zilikuzanywa, moja moja kutoka kila kabila. Fimbo iliyowakilisha kabila la Lawi jina la Haruni lilikua limeandikwa juu yake. Fimbo hizo zililazwa ndani ya hema mbele ya sanduku la agano usiku kucha, na asubuhi yake fimbo ya Haruni "ile fimbo ya Haruni iliyokuwa kwa nyumba ya Lawi ilikuwa imechipuka, imetoa michipukizi " (Hesabu 17: 8). Mungu alimwamuru Musa kuiweka fimbo ya Haruni ndani ya safina pia, akisema, "ili uyakomeshe manung'uniko yao waliyoninung'unikia" (mstari wa 10).

Wakati wa vita dhidi ya Wamaleki, Yoshua, jemadari wa jeshi la Israeli, alikuwa na ushindi tu wakati mikono ya Musa ilikuwa imeinuliwa. Musa alipolemewa na uchovu, Haruni na Huri wakaweka mawe chini kisugudi chake na kusimamisha mikono yake. Kwa njia nyingi, hii ni picha ya huduma nyingi ya Haruni kwa Musa. Alimsaidia nduguye, ambaye Mungu alikwisha mchagua kuwaongoza Waisraeli kutoka utumwani.

Juu ya Mlima wa Sinai, Mungu aliwaonya watu kusimama mbali wakati Mungu alikuwa anakutana na Musa na kumpa Sheria. Kwa sababu ya usemi wa Musa, Mungu alimwambia aje pamoja na Haruni (Kutoka 19:24). Baadaye, wakati Musa alipokawia mlimani na Mungu, aliwaweka Haruni na Huri kutatua matatizo yoyote ambayo yangeweza kutokea (Kutoka 24:14).

Kwa bahati mbaya, mambo hayakumwendea Haruni vizuri wakati alipokuwa anaongoza. Watu wakawa wasio na subira kwa kurudi kwa Musa na kumsihi Haruni kuwatengenezea sanamu. Na bile kuonekana kupinga uamuzi wa watu, Haruni aliwaomba mapambo yao ya dhahabu, na akafanya sanamu iliyokuwa na umbo la ndama. Haruni akajenga madhabahu mbele ya sanamu huyo wa ndama na kutangaza tamasha kuu kwao (Kutoka 32: 1-6). Inaweza kuonekana kuwa ngumu kuelewa jinsi mtu ambaye alitii wito wa Mungu kwa hiari ili kumsaidia nduguye ili kuwaongoza watu kutoka Misri, ambaye aliona kazi za ajabu za Mungu wakati huo huo, na ambaye hivi karibuni alimwona Mungu Mlimani Sinai angeweza kufanya jambo kama hilo. Kuanguka kwa Haruni ni dhihirisho letu la asili zetu za kibinadamu. Hatujui msukumo wa Haruni, lakini si vigumu kudhania kwamba aliweza kumtilia Mungu shaka na kuwaogopa watu.

Wakati Mungu alimwambia Musa yaliyokuwa yanaendelea kwa watu na sanamu ya ndama, alitishia kuwaangamiza watu na badala yake kufanya taifa kubwa kutoka kwa Musa. Musa aliingilia kati kwa niapa ya watu na akurudi kwao (Kutoka 32: 7-18). Wakati Musa aliona yaliyokuwa yanaendelea tokea, "Hasira ya Musa ikawaka, akazitupa zile mbao mikononi mwake, akazivunja chini ya mlima" (Kutoka 32:19). Zile mbao zilikuwa na agano la Mungu; inaonekana kuwa Musa aliziharibu sio kwa ajili ghadhabu, bali pia kwa sababu watu walikuwa wamevunja agano kwa njia ya kutotii. Musa aliiteketeza sanamu ile, na kumwagawa jivu yake katika maji, na akawafanya Waisraeli kuyanywa yale maji (Kutoka 32:20). Wakati Musa alimwuliza Haruni ni kwa nini watu wamefanya jambo hili na ni kwa nini aliwaongoza kufanya hivyo, Haruni alikuwa mkweli kuhusu lalama za watu na ombi lao la kutaka kufanyiwa mungu, lakini hakuwajibika kwa jukumu lake mwenyewe. Haruni alikiri kuwa yeye ndiye aliwakusanyisha mapambo yao lakini akasingizia kuwa, wakati "nami nikaitupa ndani ya moto, akatoka ndama huyu" (Kutoka 32:24). "Basi Musa alipoona ya kuwa watu hawa wameasi, maana Haruni amewaacha waasi, ili wawe dhihaka kati ya adui zao" (Kutoka 32:25). Musa akawaita wale ambao walikuwa wa Bwana waje kwake. Walawi walijikusanya kwake, na kisha Musa akawaagiza kuua baadhi ya watu. Musa baadaye akawaombea watu. Mungu akamhakikishia Musa lakini pia akawapiga kwa watu kwa dhambi zao (Kutoka 32: 33-35).

Tukio la ndama ya dhahabu sio kosa tu pekee Haruni alifanya. Katika Hesabu 12 Haruni na Miriamu (Haruni na dadaye Musa) wanamcha Musa: "Kisha Miriamu na Haruni wakamnenea Musa kwa sababu ya mwanamke Mkushi aliyekuwa amemwoa; maana, alikuwa amemwoa mwanamke Mkushi. Wakasema, Je! Ni kweli Bwana amenena na Musa tu? Hakunena na sisi pia? Bwana akasikia maneno yao, "Je! hajasema pia kupitia kwetu?" (Hesabu 12: 1-2). Kiburi kama hicho sio uungu, lakini ni hatari ya kawaida miongoni mwa viongozi; wengine wetu labda tu kama Haruni. Mungu aliwaita ndugu zake Haruni watatu kukutana Naye, na akamtetea Musa na kuwauliza Haruni na Miriamu, ni kwa nini Haruni na Miriamu hawakuofu kunena kinyume dhidi ya Musa. Wakati wingu ambalo Bwana alinena kutoka lilipotoweka, Miriamu akashikwa na ukoma. Haruni akamsihi Musa kwa niaba yake; Musa akamlilia Mungu, na baada ya siku saba Miriamu akiwa nje ya kambi, aliponywa (Hesabu 12: 3-16). Inashangaza kuwa Miriamu alikuwa na ukoma huku Haruni hakuwa nao. Pia inastaajabisha kuona ombi la Haruni kwa Musa, akikubali dhambi ya upumbavu wake na kumsihi asiruhusu Miriamu kuteseka. Inaonekana kwamba Haruni alikuwa ametubu ya kweli.

Haruni na wanawe walichaguliwa na Mungu ili kuwa makuhani kwa watu, na Haruni alikuwa kuhani mkuu wa kwanza. Mungu akampa Musa amri juu ya ukuhani, ikiwa ni pamoja na jinsi ya kuwaweka wakfu wakfu na ni mavazi gani walipaswa kuvaa, juu ya Mlima Sinai. Mungu alimwambia Musa kwamba ukuhani utakuwa wa Haruni na uzao wake kama amri ya kudumu (Kutoka 29: 9). Haruni alifanywa kuwa kuhani mkuu, na uzao wa familia yake uliendelea kutumika kama makuhani hadi pale uharibifu wa hekalu ulifanyika mwaka AD 70. Kitabu cha Agano Jipya cha Waebrania kinatumia muda mwingi kulinganisha ukuhani wa Yesu wa kudumu na ukuhani wa Haruni. Makuhani wa uzao wa Lawi walipaswa kutoa dhabihu kwa ajili ya dhambi zao na dhabihu kwa niaba ya watu kila wakati. Yesu hakuwa na dhambi, na dhabihu yake kwa ajili ya watu ilifanywa mara moja na imekamilika (tazama Waebrania 4-10).

Huku wana wa Haruni wakimwiga baba yao kwa ukuhani, wawili wa wanawe-Nadabu na Abihu-waliuawa na Mungu wakati walipotoa "moto wa kigeni mbele ya Bwana, ambao yeye hakuwaagiza" (Mambo ya Walawi 10: 1). Wakati Musa alimwambia Haruni kwamba hili ndilo Mungu alimaanisha wakati alisema kuwa yeye atakuwa mtakatifu, Haruni alibaki kimya (Mambo ya Walawi 10: 3). Haruni hakujaribu kuwatetea wanawe, wala kumkashifu Mungu kuwa amefanya uovu. Inaonekana wazi kuwa Haruni aliuelewa utakatifu wa Mungu na kukubali hukumu yake kwa wanawe.

Kama Musa, Haruni hakuruhusiwa kuingia katika Nchi ya Ahadi kwa sababu ya dhambi zao huko Meriba (Hesabu 20:23). Mungu alimwagiza Musa, Haruni, na Eleazari mwanawe Haruni, kwenda Mlimani Hori. Huko mlimani Eleazeri alifanywa kuhani mkuu, na Haruni papo hapo angekufa (Hesabu 20: 26-29).

Maisha ya Haruni ni dhihirisho ya utakatifu wa Mungu na neema yake. Haruni alianza kama mtumishi kwa unyenyekevu na uaminifu, na kwa hiari alienda kwa Musa na kumtumika kama muunganishi kati ya watu na Musa. Haruni pia kwa uaminifu alitumika kama kuhani katika mfumo wa dhabihu ambazo Mungu alitumia kama kivuli cha mpango Wake wa mwisho wa wokovu kupitia Yesu Kristo. Kama mwanadamu yeyote yule, Haruni alikuwa mwenye dhambi. Lakini baada ya kuona kazi takatifu ya Mungu, bado aliunda sanamu ya ndama na kuwaongoza watu kuiabudu. Lakini Haruni anaonekana kuwa alijifunza na kukomaa, kwa kukubali dhambi yake ya pingamizi dhidi ya Musa na kukubali kifo cha wanawe ambao hawakuwa waaminifu. Kutoka kwa Haruni tunajifunza juu ya kuwahudumia wengine, kushiriki katika wajibu wa uongozi, na kunyenyekea kwa Mungu.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ni nini tunaweza kujifunza kutoka kwa maisha ya Haruni?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries