settings icon
share icon
Swali

Tunapaswa kujifunza nini kutoka kwa maisha ya Ezra?

Jibu


Ezra alikuwa wa pili kati ya viongozi watatu wakuu walioondoka Babeli kwa ajili ya ujenzi wa Yerusalemu. Zerubabeli alijenga upya hekalu (Ezra 3: 8), Nehemia akajenga upya kuta (Nehemia sura ya 1 na 2) na Ezra akarejesha ibada. Ezra alikuwa mwandishi na kuhani aliyetumwa na Artashasta, Mfalme wa Uajemi kwa mamlaka ya kidini na kisiasa ili kuongoza kikundi cha Wayahudi kutoka Babeli kwenda Yerusalemu (Ezra 7: 8, 12). Ezra alihukumu ndoa za makabila tofauti na alihimiza Wayahudi kutaliki wake zao wa kigeni. Ezra alifanya upya sherehe za tamasha na kuunga mkono kutawazwa kwa hekalu na ujenzi wa ukuta wa Yerusalemu. Ezra 7:10 inaelezea kuundwa kwa jamii kulingana na Torati. Lengo la Ezra lilikuwa kutekeleza Torati, na sifa zake za kuhani na za mwandishi zilimfanya kuendelea kuwa kiongozi wa kuiga.

Kitabu cha Ezra kinaendelea na mahali ambapo kitabu cha pili cha Mambo ya Nyakati kinakamilika. Koreshi, mfalme wa Uajemi,alikuwa ametoa amri ambayo iliruhusu Wayahudi katika ufalme wake kurudi Yerusalemu baada ya miaka sabini ya utumwa. Mungu ni mkuu wa ulimwengu na anaweza kutumia mfalme wa Uajemi ambaye alikuwa mshirikina ili kuwezesha watu wake kuwekwa huru. Alitumia Artashasta, mfalme mwingine wa Uajemi, kuidhinisha na kulipia safari na Ezra ili kuwafundisha watu wa Mungu Sheria Yake. Mfalme huyo huyo pia alimsaidia Nehemia kurejesha kiwango fulani cha heshima kwa mji mtakatifu wa Mungu.

Huduma ya Ezra yenye ufanisi ilikuwa ni pamoja na kufundisha Neno la Mungu, kuanzisha mageuzi, kurejesha ibada na kuongoza uamsho wa kiroho huko Yerusalemu. Mageuzi haya yalisisitiza umuhimu wa kulinda ile sifa na mfano bora kwa jamii. Je! Ulimwengu unapaswa kufikiria nini kuhusu watu wa Mungu wenye kuta za zilizobomoka? Ni nini kingeweza kutofautisha watu wa Mungu ambao walikuwa na hatia ya kuolewa na makabila mengine na watu wasio na uhusiano sahihi wa agano na Mungu mmoja wa kweli? Nehemia na Ezra walikuwa wenye kuhimiza wakati huo, na mpaka sasa wanahimiza watu wa Mungu kumtukuza kama kipaumbele na kusisitiza haja na matumizi ya Neno la Mungu kama kanuni pekee ya mamlaka ya kuishi na pia kujali kuhusu ile picha watu wa Mungu huonyesha ulimwengu.

Ezra alirudi kutoka utumwa huko Babeli akitarajia kupata watu wakimtumikia Bwana kwa furaha, lakini aliporudi Yerusalemu, alipata kinyume chake. Alifadhaika na kuhuzunika. Alivunjika moyo, lakini bado alimwamini Bwana. Alimtaka Bwana kubadili hali hiyo na alijihukumu kwa sababu hakuweza kubadili mioyo ya watu. Aliwataka watu kujua umuhimu wa Neno la Mungu. Hakuna kinachozidi kumwabudu Mungu, na utiifu sio kwa hiari. Mungu Mwenye nguvu huwalinda watoto wake. Yeye daima huweka ahadi zake na kutoa faraja kwa wale anaowatuma (Ezra 5: 1-2) Hata wakati Mpango Wake unaonekana kuingiliwa, kama vile katika ujenzi wa Yerusalemu, Mungu huingilia kati wakati sahihi na kuendeleza mpango wake

Mungu ameshughulika sana katika maisha yetu kama vile alivyokuwa katika maisha ya Ezra, na kama vile Ezra, wakati mwingine tunawezeshwa kufanya jambo lisilowezekana. Ezra alifanya jambo lisilowezekana, kwa sababu mkono wa Bwana Mungu wake ulikuwa pamoja naye (Ezra 7: 9). Kila mwamini ni hekalu lililo hai (1 Wakorintho 6:19) ambapo Roho Mtakatifu anaishi. Nguvu za kupinga katika siku za Ezra zilikuwa ni watu wenye uovu mioyoni mwao. Nguvu za kupinga katika maisha yetu ya Kikristo leo ni shetani mwenyewe, ambaye amekuja kutuangamiza na kuharibu hekalu la Mungu (Yohana 10:10). Malengo yetu yanapaswa kustahili machoni pa Mungu kama vile yetu wenyewe. Majuto ya jana yanaweza kuwa mafanikio ya leo ikiwa mkono wa Bwana u pamoja nasi. Lengo la Ezra lilikuwa lafaa machoni pa Mungu, na alitumia vizuri maumivu ya Wayahudi waliokuwa wanarudi kwa mafanikio ya kujenga mji wa Mungu na kurejesha ibada.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Tunapaswa kujifunza nini kutoka kwa maisha ya Ezra?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries