settings icon
share icon
Swali

Tunaweza kujifunza nini kutokana na maisha ya Ezekieli?

Jibu


Ezekieli, ambaye jina lake linamaanisha "kuimarishwa na Mungu," alikulia huko Yerusalemu, alihudumu kama kuhani katika hekalu na alikuwa katika kundi la pili la wafungwa waliopelekwa Babeli pamoja na Mfalme Yehoyakini. Bado akiwa Babeli akawa nabii wa Mungu; yeye ndiye mwandishi wa kitabu cha Agano la Kale ambacho kimechukua jina lake. Huduma ya Ezekieli ilianza kwa kuihukumu na kulikemea taifa la Yuda. Baada ya Yerusalemu kuharibifu, unabii wa Ezekieli unazungumzia tumaini la wakati ujao. Ezekieli alitaka kuwasaidia watu kujifunza kutokana na makosa yao. Alitangaza hukumu iliyoingojea mataifa yaliyoizunguka Yuda na kuanzisha tumaini la kurejeshwa kwa Israeli. Maono yake ya bonde la mifupa mikavu (Ezekieli 37) inaonyesha maisha mapya yatakayopuliziwa taifa, ambayo lyatatimia katika Ufalme wa kizazi kipya cha utawala wa Kristo duniani.

Maono ya kwanza ya Ezekieli ilikuwa ya kiti cha enzi cha Mungu ambacho kilikuwa na viumbe hai vinne na magurudumu yaliyosunguka. Ezekieli pia alikuwa na maono ya kina ya hekalu jipya (Ezekieli 40-43), Yerusalemu iliyorejeshwa (Ezekieli 48: 30-35), milenia (sura ya 44), na nchi ambayo watu wa Mungu watakaa (Ezekieli 47: 13- 23). Israeli na Yuda zitarejeshwa tena kwa umoja toka mwishoni mwa pembe za dunia utukufu wa Mungu unaporejea pia na Mungu ataishi kati ya watu Wake. Maono haya mazuri ya Ezekieli yanayohusu mipango wa wakati huo na wakati ujao wa Mungu. Ezekieli aliwasilisha ujumbe wa Mungu kwa lugha inayoeleweka ambayo kila mtu angeweza kumwelewa, hata kama walimsikiza au siyo (Ezekieli 2: 7). Ezekieli mwenyewe alipokea onyo kutoka kwa Mungu kwamba, ikiwa hangewaonya kwa uaminifu kuhusu adhabu ya kutomfuata Mungu, angewajibika kwa damu ya wale wangekufa katika dhambi zao (Ezekieli 33: 8-9). Hakusita katika utume wake na aliyafuata maelekezo ya Mungu kwa uangalifu. Ezekieli alikuwa na mtazamo wa huruma kwa hukumu na matumaini, na alionyesha huzuni ya Mungu mwenyewe juu ya dhambi za watu.

Nabii alipatwa na upinzani mkubwa wakati wa maisha yake mwenyewe, lakini alionyesha wazi kwamba Mungu alitamani kuwa waovu wasife bali wageuke kutoka njia zao mbaya na kuishi. Ugugumizi wake wa mara kwa mara wakati wa miaka yake ya utoto ulikatika wakati Mungu alimpa uwezo wa kuzungumza, na kinywa chake kilifunguliwa kuzungumza kifungu kirefu zaidi cha matumaini endelevu katika Biblia. Kuungua, kukatika, na kusambaratika kwa nywele zake kuliwakilisha kuanguka kwa Yerusalemu na kurejeshwa kwa wateule wa Mungu (sura ya 5). Kilele cha maneno yenye matumaini katika ahadi ya milki ya milele ya nchi, na mtawala mkuu wa uzao wa Dawudi, agano la milele, na patakatifu pa milele katika Israeli (Ezekieli 11: 16-21). Atavuna mapema kabla ya muda baada ya Israeli kurejeshwa kutoka kwa wavamizi wa siri kutoka kaskazini ambao utaletwa na Bwana kwa Israeli, lakini kisha baadaye utashindwa kabisa. Hii inaonyesha kuwa hakuna taifa adui litaivamia tena Nchi Takatifu tena kwa mafanikio, na utukufu wa Mungu kwa Israeli utarudi, ukipitia lango la mashariki la hekalu ambalo Ezekieli aliona katika maoni.

Ezekieli ameonyesha Wakristo wote kwamba tunapaswa kuwa watiifu kwa wito wa Mungu katika maisha yetu. Mungu alimwambia Ezekieli kuomboleza kwa moyo uliovunjika na kuhuzunika kwa uchungu kwa hukumu inayokuja, na katika kitabu chake kikubwa, Ezekieli anatuambia jambo hilo hilo. Hukumu hii inakuja! Kwa hakika itafanyika, asema Bwana Mwenye Enzi Kuu! Sisi pia, tunaweza kuwaonya wengine na kushiriki nao habari njema ya wokovu katika Yesu Kristo.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Tunaweza kujifunza nini kutokana na maisha ya Ezekieli?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries