settings icon
share icon
Swali

Tunajiunza yapi kutoka kwa uhai wa Esta?

Jibu


Esta ni kijakazi waKiyahudi hatimaye akawa malkia wa Uajemi na kuwaokoa jamii yake dhidi ya madhara yaliyolenga kuwakamilisha. Simulizi lake limenakiriwa kwenye nakala za Agano la Kale inayojulikana kwa anwani. Sherehe za Kiyaudi za Purimu huidhinishwa nyakati za kuokoa Wayahudi.

Simulizi za Esta zinaanzia na tunuku za mfalme. Mtawala Ahasuero (pia atambulikaye kama Ahasuero) alikuwa kijana wa mtawala mtajika wa Kiajemi Darius I, atambulikaye kwenye Ezra 4:24; 5: 5-7; 6: 1-15; Danieli 6: 1, 25; Hagai 1:15; na 2:10. Mwaka wa tendo lile miongoni mwa Esta na Mtawala Ahasuero mnamo 483 kk. Utawala wa mtawala Ahasuero ulisitaajabisha; hakika, ulizidi wowote uliopata kujulikana ulimwenguni. Uapersia ukachukua mahali panapotambulika kuwa Uturuki, pakiwemo pia Iraki, Irani, Pakistan, Jordan, Lebanoni, na Israeli; kadhalika kuhusisha maeneo ya Misri ya kisasa, Sudan, Libya na Saudi Arabia.

Jinsi idhihirikavyo kwenye waasi wa watawala wa Kitaifa wa enzi hizo, Mtawala Ahasuero alipendelea kutia hadharani utajiri wake na ukuu, iliyojumuhishwa sherehe mara nyingi zilizofanyika hata takribani Zaidi ya 180. Bila shaka, nyakati za sherehe zinazozungumziwa kwenye Esta 1: 10-11, mtawala akamsihi bibiye, Malkia Vashti, kuja hadharani kwa kusanyiko la watawala ili kujionyesha urembo aliokuwa nao kwa kujivisha vazi lake la utawala. Kadirio ni kuwa Mtawala Ahasuero alikadiria Vashti kujionyesha akivalia tu taji. Malkia Vashti alikaidi agizo la mtawala, na ndipo akajazwa hamaki. Mtawala Ahasuero alitauta ushauri kwa wanatorati waliosema kuwa Vashti alikosea taifa lote. Walijawa woga kwamba wake wa Persia watapata taaria ilekuhusu Vashti kukaidi mume wake na wakose kuwatii waume zao. Walitoa ombi mtawala kutoa pendekezo kwa taifa lote kuwa Vashti hasiweze kujileta machoni mwake tena. Mtawala akatii hilo, akieneza tangazo hilo kwa majimbo yaote kwa lugha tofauti.

Kwa kuachwa kwa Vashti, mtawala akawa bila malkia. Wafuasi wa Ahasuero walitoa pendekezo kutafuta bikira mwingine kwenye taifa lote ili kupata malkia. Josephus, mwanahistoria wa Kiyahudi, ananakiri kuwa mtawala Ahasuero alipendekeza wake 400 kuwania nafasi hiyo na kuchukua nafasi ya malkia mpya (Esta 2: 1-4). Wake hao walifaa kupitia uthamini wa urembo kwa mwaka mmoja kabla ya kuonana na mtawala (mstari wa 12). Esta, mke wa Kiyahudi aliyetambulika kama Hadasa kwa Kiebrania, alipendekezwa kuwa miongoni mwa wanawake hao mabikra(mstari wa 8).

Mpaka nyakati wale wake walipelekwa kwa mtawala,wakachukuliwa faraghani chini ya ulinzi wa Hegai (Esta 2: 8); kisha, kukutana kwao, kwa maana hawakuwa wakunga tena, walichukuliwa kwa mahali palipotengwa kuwahifadhi — au wanawake – walipotiwa kwenye ulinzi wa mlinzi mwingine aliyetambulika kama Shaashigaz (mstari wa 14).

Esta alipiga kambi kitongjini Susa, alipoishi pia mtawala. Akiwa binamu wa Mbenjamini atambulikaye kama Mordekai, na vile vile mlezi wake, akiwa amemtunza sawia na mtoto wake nyakati zile wakati wazazi wake walipokata roho. Mordekai naye alimiliki cheo maalum kwenye utawala wa Kiajemi (Esteri 2:19). Pale Esta alipotambulika kama mgwania wa umalkia, Mordekai alimwarifu asijitambulishe kuwa na asili ya Kiyahudi (mstari wa 10). Vile vile alienda kwenye mazingira ya mtawala ili kumwona Esta alivyokuwa akiendelea (mstari wa 11).

Zamu ya Esta ya kukutana na mtawala ilipowadia, kuja, "yeye hakutaka kitu ila vilivyoagizwa na Hegai msimamizi wake mfalme mwenye kuwalinda wanawake. naye Esta alikuwa amepata kibali machoni pa wote waliomwona" (Esta 2:15). ). Kadhalika akapata kibali na neema machoni pa mtawala: "mfalme akampenda Esta zaidi kuliko wanawake wote," na akamkamilisha kuwa malkia (Esta 2:17). Inakisiwa kuwa Esta, fauka ya kuwa na "umbo mzuri na uso mwema" (mstari wa 7), pia alijishusha katika kupata mwelekeo kutoka kwa washauri wenye busara na mcheshi kwa kila namna. Simulizi iendeleavyo,inadhihirika kuwa Bwana alikuwa kazini kwa matukio hayo yote.

Muda baadaye, Mordekai alikuwa akikaa mlangoni pa mtawala la mfalme na alipata habari ya kuangamizwa kwa Ahasuero. Akamjuza Malkia Esta, aliyepeleka ripoti hiyo kwa mtawala na pia Mordekai akatuzwa. Njama hizo ziliangamizwa, ila kitendo chenyewe kikasahaulika vikubwa (Esta 2: 21-23). Tunapata kwenye tendo hili kujuana kwa Esta na Mordekai vile vile kujiweka kwake. Mordekai na Esta pamoja wakamuenzi mtawala na wakaamua kumkinga dhidi ya maasimu wake.

Fauka ya hayo, mtawala akamteua mtu wa uovu kusimamia mambo yake. Alijulikana kama Hamani, na aliwaonea Waisraeli. Hamani alitoka kwenye uzao wa Agagi, mtawala wa Waamaleki, watu waliokuwa maasimu wa jadi wa Israeli (Kutoka 17: 14-16), na ubaguzi na hasira juu ya Israeli ilikuwa imekita mizizi kwenye roho isiyosafi ya Hamani. Kwa kiburi chake, Hamani aliwaambia wakaazi kwenye malango ya mtawala kupiga magoti na kumsujudu, ila Mordekai alikaidi. Maafisa wa kitawala wakamjuza Hamani kuhusu hilo, wakiwa bila sitasita kumwarifu Hamani kuwa Mordekai alikuwa Myahudi. Hamani si tu aliazimia kumpa adhabu Mordekai bali "alitaka kuwaangamiza Wayahudi wote, watu wake Mordekai, waliokuwa wakikaa katika ufalme wote mzima wa Ahasuero" (Esta 3: 6). Mtawala Ahasuero akamkubalia Hamani kutenda alivyoona vema kwenye neno hilo, na agizo likaenezwa kwa majimbo yote kuwa siku maalumu, iliyoteuliwa na wengi, watu walikuwa" kuwaangamiza Wayahudi wote, kuwaua, na kuwafisha, vijana kwa wazee, watoto wachanga na wake pia siku moja "(Esta 3:13). Watu walifadhaika na kukawa na kulia na kuomboleza miongoni mwa Wayahudi (Esta 3:15; 4: 3).

Malkia Esta alikuwa hana habari kuhusu mipango hiyo kwa Wayahudi, ila alijua pale vijakazi wake na wasimamizi walipomjuza kuwa Mordekai alikuwa kwa huzuni. Esta akamwambia mjumbe kwenda kwa Mordekai ndipo amjuze taabu zake. Mordekai akatuma binamu yake nakili ya andiko la mbiu ya kuwaangamiza na kumsihi "tena amwagiza aingie kwa mfalme kumsihi na kuwaombea watu wake" (Esta 4: 8). Hivo,kulikuweko na amri dhidi ya kuenda machoni pa mfalme bila mwaliko,na Esta alikuwa hajapata mwaliko na mtawala takribani siku thelathini zilizopita. Kupitia kwa mpatanishi wake, Esta alitoa taaria kwa Mordekai kwa kutoweza kuwa wa msaada. Akajibu, "wewe usijidhanie kuwa wewe utaokoka nyumbani mwa mfalme Zaidi ya Wayahudi wote. kwa maana wewe ukinyamaza kabisa wakati huu ndipo kutakapowatokea Wayahudi msaada na wokovu kwa njia nyingine; ila wewe utaangamia pamoja na mlango wote wa baba yako;walakini ni nani ajuaye kama wewe hukuujia ufalme kwa ajili ya wakati kama huo?" (Esta 4: 13-14). Kwa kudhihirisha kiwango kikubwa cha imani, Esther aliitikia. Aliwaagiza Wayahudi kumfunga kwa siku tatu naye pia na vijakazi wake wakaunga. "kisha nitaingia kwa mfalme, kinyume cha sheria," akanena, "name nikiangamia, na niangamie" (Esta 4:16).

Esta alipoenda kwa mtawala, alikuwa uhai wake kwenye hatari. Ila Ahasuero "yeye akapata kibali machoni pake naye akamnyoshea Esta fimbo ya dhahabu aliyokuwa nayo mkononi," onyesho kwamba alikubalia kuweko kwake pale (Esta 5: 2). Akamkaribisha Ahasuero na Hamani kwenye maakuli siku hiyo. Mtawala akamwariu Hamani kuja kwenye karamu ya divai na kusema dua yake, "hata nusu ya ufalme utafanyiziwa" (mstari wa 6). Esta aliwaalika waume wawili kushiriki sherehe alfu iliyofuata na hapo ataweka wazi azimio lake (mstari wa 8). Waume wakaitikia.

Ahasuero alipata taabu kupata usingizi usiku ule na kuagiza rekodi ya uongozi wake asomewe. La ajabu, nakala aliyoisikia ni kuwa njama ya Mordekai kuweka wazi njama ya mashambulizi na kukinga uhai wa mtawala. Hata ivo, Hamani alienda maskani, akawakukasanya wandani wake na bibiye, na kuwajuza namna alivyotambuliwa. Ila alimwona Mordekai njiani kwenda maskani, iliyozusha roho yake sana.Bibiye na wandani wake wakaonelea Hamani kujenga mahali pa kumteketezea Mordekai (Esta 5: 9-14). Hamani aliitikia ushauri huo na kujenga eneo.

Jinsi ilivyo kwa mtawala Ahasuero alivyoasi namna alivyokosa kumheshimu Mordekai katika njama ya kulinda uhai wake, Hamani aliingilia kati kuongelea jambo la kumuangamiza Mordekai. Mtawala akatafuta maoni ya namna ya kumfanyizia mtu ambaye "mfalme apenda kumheshimu" (Esta 6: 6). Hamani, akidhani kwamba Ahasuero alimaanisha yeye, akapendeza yule ambaye mfalme apenda na aletewe mavazi ya mfalme na farasi ambaye mtawala humpanda mwenyewe,na kupiga mbiu mbele yake, "hivyo ndivyo atakavyofanyiziwa mtu yule ambaye mfalme apenda kumheshimu." (Esta 6: 9). Ahasuero akamwambia Hamani kumtendea vile Mordekai mara moja.

Hamani akamhitikia mtawala na kumtumikia mwanaume aliyechukizwa naye Zaidi. Baadaye akamjuza bibiye na wandani wake matendo yale. Kwa mtazamo mkubwa kuliko walivyotarajia, watu wake wenye hekima na Zereshi mkewe wakamwambia, 'Ikiwa huyu Mordekai, ambaye umeanza kuanguka mbele yake, ni wa uzao wa Wayahudi, wewe hutamuweza bali kuanguka utaanguka mbele yake' "(Esta 6:13). Wasimamizi wa nyumba ya mtawala walifika wakahimiza kumleta Hamani katika sherehe iliyoandaliwa na Esta (mstari wa 14). Hapo, Esta alimjuza mtawala kuwa watu wake walitolewa kwa kuteketezwa. Akidhihirisha kujishusha na kunyenyekea, Esta alisema wangekuwa wameuza kwa utumwani, angenyamaza, ila hata hivyo msiba wetu haulinganishwi na hasara ya mfalme" (Esta 7: 4). Mtawala akasitaajabu kuwa kuna angefanya mambo kama hayo kwa jamii ya malkia wake (mstari wa 5). Esta alimweka hadharani mtu mwenye iyo mipango kuwa ni "Hamani huyu mkaidi" (mstari wa 7). Ahasuero aliondoka shereheni akijawa na hamaki. Hamani akasalia nyuma kumbembeleza Esta kwa sababu ya uhai wake. Mtawala aliporejea chumbani na kuona vile,akafikiria Hamani alikuwa akimghadhabisha Esta na akamaamuru Hamani kunyongwa kwa maeneo aliyomtengenezea Mordekai (mstari wa 8-10).

Hamani alipokufa, Ahasuero akampatia Esta utajili wote wa Hamani na kumpatia Mordekai pete yake, kisha kumpatia Mordekai nguvu sawia katika utawala aliokuwa nao mbeleni. Agizo hilo lilienea kutoka kwa Hamani, ingawa, haingebadilishwa. Esta alimsihi mtawala mara ingine ili kujihusisha hapo tena. Ahasuero aliamuru tena nakili kuandikwa dhidi ya ile ya awali: na hii iliwaruhusu Wayahudi uhuru wa kujikinga dhidi ya watakao washambulia. Hatimaye kukajawa na shangwe kote kwa majimbo yote. Hata wengi kutokana na woga wakakuwa Wayahudi. Maasidi wengine walishambulia siku iliyotengwa kirasmi, ila Wayahudi walipata ushindi dhidi yao (Esta 8).

Busara na imani thabiti ya Esta kwa Bwana ziko agano la kuaminika kuwa mke huyu alimiliki kwa Bwana anayeishi. Maisha yake ni funzo kwenye utawala wa Mungu dhidi ya viumbe vyake. Mungu hugeuza kila nafasi ya uhai wa watu, utawala na mashirika kwwa mpango wake na mathumuni. Huenda tusijue yale Bwana anatenda kwa muda fulani, ila wakati utafika tutangamua mbona tumepatana na masaibu fulani ama kupatana na waja fulani ama kuishi kwa sehemu fulani, ama kununua vitu duka maalum ama kuenda safari fulani. Muda utafika kila kitu kitajumuishwa, na tuangalie nyuma, vile vile, ilikuwa kwa sehemu ifaayo kwa wakati mwafaka, kama tu Esta alivyokuwa. Alikuwa kwenye harem "kwa wakati kama huo." Alifanyizwa kuwa malkia "kwa wakati kama ule." Alipata nguvu na kutayarishwa kwa kuwaombea jamii yake "kwa nyakati kama zile" (Esta 4:14). ). Na akawa mwaminifu kushika amri. Esta alimwamini Mungu na kwa kujishusha katika utumizi, pasipokuzingatia kitakachompata. Esta kwa hakika ni kumbusho la aliyoahidi Mungu, kulingana na Warumi 8:28: "Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema,yaani,wale walioitwa kwa kusudi lake."

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Tunajiunza yapi kutoka kwa uhai wa Esta?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries