settings icon
share icon
Swali

Ni nini tunaweza kujifunza nini kutoka kwa maisha ya Eliya?

Jibu


Nabii Eliya ni mmojawapo wa watu wenye kuvutia na mtu maridadi zaidi katika Biblia, na Mungu akamtumia wakati wa kipindi muhimu katika historia ya Israeli kumpinga mfalme mwovu na kuleta ufufio katika nchi. Huduma ya Eliya ilisababisha mwanzo wa mwisho wa ibada kwa Baali katika Israeli. Maisha ya Eliya yalijawa na matatizo. Wakati mwingine alikuwa mwenye ujasiri na mwenye uwezo wa kufanya uamuzi, na wakati mwingine alikuwa mcha Mungu and msikifu. Kwa upande mwingine yeye ni dhihirisho la ushindi na uhodari, ikifuatiwa na kurudisha kilichopotea. Eliya alijua nguvu zote za Mungu na kina cha msononeko.

Eliya, nabii wa Mungu ambaye jina lake linamaanisha "Mungu wangu ni Bwana," alikuwa anatoka mji wa Tishbi huko Gileadi, lakini hakuna linajulikana kuhusu familia yake au kuzaliwa kwake. Tunamwona Eliya mara ya kwanza katika 1 Wafalme 17: 1 wakati anatokea kwa ghafla ili kumkabili Ahabu, mfalme mwovu ambaye alitawala ufalme wa kaskazini kutoka mwaka wa 874 hadi 853 Kabla Yesu azaliwe. Eliya anatabiri juu ya ukame ambao ungekuja katika nchi yote kwa sababu ya uovu wa Ahabu (1 Wafalme 17: 1-7). Aliyoonywa na Mungu, Eliya anajificha karibu na kijito cha Kerithi ambako alilishwa na kunguru. Ukame na njaa zilipoongezeka katika nchi, Eliya akakutana na mjane katika nchi jirani, aliitikia kwa utiivu ombi la Eliya, Mungu akatoa chakula cha kutosha kwa Eliya, mwanamke, na mwanawe. Kimuujiza, pipa la unga la mjane na chupa la mafuta kamwe hafikuisha (1 Wafalme 17: 8-16). Somo kwa waumini ni kwamba, ikiwa tunatembea katika ushirika na Bwana na kumtii, kwa wazi tutaitikia mapenzi Yake. Na wakati tuko katika mapenzi ya Mungu, Yeye hutimiza mahitaji yetu yote, na rehema yake kwetu haikomi kamwe.

Mara nyingine tunamwona Eliya akiwa mhusika mkuu ni katika makabiliano na manabii wa uongo wa Baali kwenye Mlima Karmeli (1 Wafalme 18: 17-40). Manabii wa Baali walimwita mungu wao mchana kutwa ili azushe moto kutoka mbinguni bila mafanikio. Kisha Eliya akajenga madhabahu ya mawe, akachimba shimo kando yake yote, akaweka dhabihu juu ya kuni na akaomba maji yamwagwe juu ya dhabihu yake mara tatu. Eliya akamwita Mungu, na Mungu akateremsha moto kutoka mbinguni, ukachoma ile dhabihu, kuni, na mawe na kuvyonza maji kwenye shimoni. Mungu alionyesha kuwa alikuwa na nguvu zaidi kuliko miungu ya uongo. Ilikuwa ni wakati huo Eliya na watu waliwaua manabii wote wa uongo wa Baali, wakifuata amri ya Mungu katika Kumbukumbu la Torati 13: 5.

Baada ya ushindi mku juu ya manabii wa uongo, mvua ikaanguka tena katika nchi (1 Wafalme 18: 41-46). Hata hivyo, licha ya ushindi huo, Eliya aliingia katika kipindi cha myumbisho wa imani na msononeko (1 Wafalme 19: 1-18). Ahabu alikuwa amekwishamwambia mkewe, Yezebeli, dhihirosho la nguvu za Mungu. Badala ya kumrudia Mungu, Yezebeli aliapa kumwua Eliya. Eliyo aliposikia jambo hili, alikimbilia jangwani, ambako aliomba Mungu ayachukue maisha yake. Na badala yake Mungu alimhuhisha Eliya kwa chakula, kunywaji, na usingizi. Kisha Eliya alishika safari ya siku arobaini kwenda Mlima Horebu. Huko mlimani Eliya akaficha ndani ya pango, huku akijihurumia mwenyewe na hata kukiri kuwa yeye pekee ndiye aliyekuwa amebaki kati ya manabii wa Mungu. Hapo ndipo Bwana alimwambia Eliya asimame juu ya mlima, Bwana anapopita. Kulikuwa na upepo mkubwa, tetemeko la ardhi, na kisha moto, lakini Mungu hakuwa katika yote hayo. Kisha kukaja sauti nyororo, ambayo Eliya alimsikia Mungu na kumwelewa. Mungu akampa Eliya maagizo ya chenye atafanya baadaye, ikiwa ni pamoja na kumtia mafuta Elisa ili achukue nafasi yake kama nabii na akamhakikishia Eliya kwamba bado kulikuwa na watu 7,000 huko Israeli ambao hawakuwa wamepiga goti lao kwa Baali. Eliya alitii amri za Mungu. Elisha akawa msaidizi wa Eliya kwa muda mfupi, na hao wawili wakaendelea kukabiliana na Ahabu na Yezebeli, pamoja na mwana wa Ahabu na mrithi wake, Ahazia. Badala ya kufa kifo cha asili, Eliya alichukuliwa mbinguni kwa upepo wa kisulisuli (2 Wafalme 2: 1-11).

Huduma ya Yohana Mbatizaji ilibainishwa na "katika roho ya Eliya, na nguvu zake" (Luka 1:17), ikitimiza unabii wa Malaki 4: 5-6). Yakobo anamtumia Eliya kama mfano wa sala katika Yakobo 5: 17-18. Anasema kwamba Eliya "alikuwa mwanadamu mwenye tabia moja na sisi" lakini bado aliomba ili isinyeshe, na haikusha. Kisha akaomba inyeshe, na ikanyesha. Nguvu ya sala ii na Mungu, si katika asili yetu ya kibinadamu.

Kama ilivyokuwa kweli kwa Eliya, tunapozingatia msukosuko wa maisha katika ulimwengu huu, tunaweza kupata macho yetu kutolewa mbali na BWANA na hivyo tanakata tamaa. Mungu anajidhihirisha Mwenyewe katika nguvu za kazi yake na hukumu kama vile upepo, moto, na mtetemeko wa ardhi. Lakini pia anahusiana nasi kwa karibu na kibinafsi, kama vile mnong'ono mtulivu. Mungu hukutana na mahitaji yetu ya kimwili, hutuhimiza kuchunguza mawazo yetu na tabia zetu, inatuonya njia tutakayoifuata, na inatuhakikishia kuwa hatuko peke yetu. Wakati tunaisikiliza sauti ya Mungu na kutembea kwa kutii Neno Lake, tunaweza kupata faraja, ushindi, na tuzo. Eliya alijitahidi na udhaifu wa kawaida wa binadamu, lakini alikuwa akitumiwa kwa nguvu ya Mungu. Inaweza kuwa si kwa njia ya maonyesho ya ajabu ya nguvu, lakini, ikiwa tumejitoa kwake, Mungu anaweza kututumia kiajabu kwa ajili ya madhumuni ya ufalme wake.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ni nini tunaweza kujifunza nini kutoka kwa maisha ya Eliya?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries