settings icon
share icon
Swali

Tunapaswa kujifunza nini kutokana na maisha ya Elisha?

Jibu


Elisha, ambaye jina lake linamaanisha "Mungu ni wokovu," alikuwa mrithi wa Eliya katika ofisi ya unabii katika Israeli (1 Wafalme 19:16, 19-21; 2 Wafalme 5: 8). Aliitwa kumfuata Eliya katika 1 Wafalme 19:19, na alitumia miaka kadhaa iliyofuata kama mwanafunzi wa nabii, hadi pale Eliya alichukuliwa mbinguni. Wakati huo, Elisha alianza huduma yake, ambayo ilidumu miaka 60, ikijumuisha utawala wa wafalme Yehoramu, Yehu, Yehoahazi na Yoashi.

Wito wa kwanza wa Elisha ni wa maelekezo. Baada ya Mungu kuonyesha nguvu yake dhidi ya manabii wa Baali na urejesho wa mvua baada ya ukame wa muda mrefu, Malkia Yezebeli alitafuta kumwua Eliya. Kwa kuogopa, nabii alitorokea maisha yake. Alifarijiwa na malaika na akajitayarisha kwa safari ya siku arobaini kwenda Mlima Horebu. Akiwa huko, Eliya alikiri kwamba alikuwa ameamini kuwa yeye ndiye nabii pekee ambaye aliyebaki. Mungu alimwambia Eliya kurudi nyumbani, kumtia mafuta Hazaeli mfalme wa Aramu, Yehu mfalme wa Israeli, na Elisha kumridhi yeye kama nabii. Mungu akasema, "Na itakuwa atakayeokoka na upanga wa Hazaeli, Yehu atamwua; na atakayeokoka na upanga wa Yehu" (1 Wafalme 19:17). Pia alimhakikishia Eliya kwamba kulikuwa na watu 7,000 waliosalia ambao hawakuwa wamepiga goti lao kwa Baali.

Eliya alitii neno la Mungu na akampata Elisha ambaye alikuwa akilima kwa ndume wawili wakati huo. Eliya akaweka vazi lake karibu na Elisha-ishara ya kuwa majukumu ya Eliya yalipeanwa kwa Elisha, na Elisha akaacha ng'ombe wake na kumkimbilia nabii. Elisha alimsihi aende awapigie jamaa yake kwaheri na kisha atarudi kwa Eliya. Elisha akarudi, akawachinja ng'ombe zake na kuteketeza vifaa vyake, akawapa watu nyama, kisha akamfuata Eliya kama mtumishi wake. Elisha aliitikia wito huo mara moja. Alijitenga kabisa kutoka kwa maisha yake ya zamani-hasa katika kuandaa karamu na kuwa bila fursa yeye mwenyewe ya kurudia ng'ombe wake. Elisha hakuyaacha maisha yake ya zamani pekee yake tu, alikuwa mtumishi katika maisha yake mapya (1 Wafalme 19:21).

Elisha alionekana kumpenda Eliya kama vile mtu anavyompenda baba. Alikataa kumwacha Eliya kabla Eliya achukuliwe mbinguni, hata ingawa Eliya alimwambia Elisha kubaki nyuma. Eliya alimruhusu Elisha kuishi naye, naye akamwuliza mwanafunzi wake chenye angetaka kufanyiwa kabla aondoke. Elisha aliomba mara mbili ya sehemu ya roho wa Eliya. Hili halikuwa ombi la uchoyo bali linaonyesha kuwa Elisha alitaka kuchukuliwa kama mwana wa Eliya. Eliya akamwambia Elisha kwamba, ikiwa angeona Eliya akichukuliwa mbinguni, basi roho wake mara dufu ingekuwa sehemu yake. Elisha kwa kweli aliona gari la moto na farasi wa moto ambao waliwatenganisha watu, naye akamwona Eliya akichukuliwa mbinguni katika kisulisuli. Elisha akachukua vazi la Eliya na akwenda hadi Mto Yordani. Elisha akayapiga maji kwa vazi lile, na maji yakagwaganyika, kama vile alivyomfanyikia Eliya. Manabii wengine ambao waliona hili walitambua kwamba roho ya Eliya sasa iliwekelewa juu ya Elisha. Kama Mungu vile Mungu alikuwa amekwisha tangaza, Elisha sasa angekuwa nabii Wake kwa watu (2 Wafalme 2: 1-18).

Kama vile Mungu alikuwa amemwambia Eliya katika mlimani, ilikuwa ni wakati wa huduma ya Elisha ambayo ilisababisha ibada ya Baali kuondolewa (2 Wafalme 10:28). Katika huduma yake Elisha alitembea mahali kwingi sana na alitumika kama mshauri wa wafalme, rafiki wa watu wa kawaida, na rafiki wa Waisraeli na wageni.

Kuna matukio mengi yanayojulikana ya huduma ya Elisha kama nabii. Aliponya maji ya Yeriko (2 Wafalme 2: 19-21) na alishangiliwa na vijana aliowalaani na kusababisha kifo chao kwa kuuliwa na dubu (2 Wafalme 2: 23-25). Alizidisha mafuta ya mjane (2 Wafalme 4: 1-7). Alitabiri kuwa mwana wa tajiri mmoja familia ya Shunemu ambaye alimkaribisha na baadaye alimfufua mwana huyo huyo (2 Wafalme 4: 8-37). Elisha pia aliondoa sumu kutoka cha nyama (2 Wafalme 4: 38-41) na kuzidisha mikate ishirini ya shayiri ili kulisha watu mia moja (2 Wafalme 4: 42-44). Alimponya Naamani aliyekuwa na ukoma (2 Wafalme 5) na akakifanya shoka iliyokuwa imekopeshwa kuelea (2 Wafalme 6: 1-7). Miujiza nyingi ambayo Elisha alifanya kwa sehemu ni kwa ajili ya vitendo vya manufaa na baraka. Ishara zingine hufanana sana na zile ishara za Kristo, kama kuzidishwa kwa chakula (Mathayo 16: 9-10) na uponyaji wa ukoma (Luka 17: 11-19).

Elisha alimpa ushauri mfalme wa Israeli. Tukio moja linaelezea Elisha akimuonya mfalme kuhusu pilkapilka za mfalme wa Aramu. Wakati mfalme wa Aramu alipongundua kwamba Elisha alikuwa akiharibu mipango yake, alijaribu kumkamata nabii. Wakati mtumishi wa Elisha, Gehazi, alipoona Waaramu waliokuwa wamewajia, aliogopa. Lakini Elisha alimwambia asiogope kwa sababu "wale walio pamoja nasi ni zaidi ya wale walio pamoja nao."Elisha akamwomba, "Fungua macho yake, Bwana, ili apate kuona." Kisha Bwana akafumbua macho ya mtumishi, naye akaangalia na kutazama vilima vilivyojaa farasi na magari ya moto karibu na Elisha "(2 Wafalme 6: 16-17). Tunapata kukumbuka jinsi Elisha alivyoona magari sawa ya moto wakati Eliya alipelekwa mbinguni. Elisha kisha akaomba kwa kuwa Waaramu wapigwe kwa upofu. Elisha aliwaongoza kwenda Samaria, mji mkuu wa Israeli, kabla ya kumwomba Bwana kufungua macho yao. Mfalme wa Israeli aliwaza ikiwa angewaua wafungwa, lakini Elisha alimshauri kuwaandalia chakula badala yake. Walipomaliza sikukuu, Waaramu walirudi kwa bwana wao, na Aramu iliacha kushambulia Israeli. Elisha pia alitabiri matukio mengine ya muhimu kwa taifa na mataifa kuhusu Israeli na Shamu.

Mfalme Yehoashi, au Yoashi, alikuwa akitawala wakati wa kifo cha Elisha. Mfalme alitembelea Elisha wakati nabii huyo alipokuwa mgonjwa na kumlilia. Elisha aliamuru Yoashi kutwaa upinde na mishale na kuupiga nje ya dirisha. Yoashi alipofanya hivyo, Elisha akamwambia huo ulikuwa mshale wa Mungu wa ushindi juu ya Aramu. Elisha akamwambia mfalme apige chini mishale, lakini Yoashi akaipiga chinimara tau, akaacha. Elisha alikasirika. Yehoashi piga chini mara tano au sita, angeangamiza kabisa Aramu lakini sasa angewashinda mara tatu tu (2 Wafalme 13: 14-19).

Kitabu cha 2 Wafalme 13:20 inasema tu, "Elisha alikufa na kuzikwa." Lakini kifungu hicho kinaendelea kuzungumza juu ya washambuliaji wa Moabu ambao walikuja Israeli majira ya chipuko: "Ikawa, walipokuwa wakimzika mtu, angalia, waliona kikosi; wakamtupa yule mtu kaburini mwa Elisha; mara yule maiti alipoigusa mifupa ya Elisha, alifufuka, akasimama kwa miguu. "(2 Wafalme 13:21). Inaonekana kwamba Mungu alichagua kuonyesha nguvu zake kupitia nabii huyo hata baada ya kifo chake.

Yesu alizungumzia Elisha katika Luka 4:27. Watu walikuwa wamemkataa Yesu huko Nazareti na akawaambia kwamba "hakuna nabii anayekubalika katika mji wake mwenyewe" (Luka 4:24). Yesu alisema kulikuwa na wakoma wengi katika Israeli wakati wa Elisha, lakini ni Namani tu, mjeshi wa Siria aliyeponywa.

Utafiti wa maisha ya Elisha unaonyesha unyenyekevu wa nabii huyo(2 Wafalme 2: 9; 3:11), upendo wake wazi kwa watu wa Israeli (2 Wafalme 8: 11-12), na uaminifu wake katika huduma ya kila siku. Elisha alikuwa mtiifu kwa wito wa Mungu, alifuata Eliya kwa uaminifu. Elisha aliamini Mungu na kusadiki. Elisha alimtafuta Mungu, na kupitia kwake Mungu alifanya kazi imara.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Tunapaswa kujifunza nini kutokana na maisha ya Elisha?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries