settings icon
share icon
Swali

Apolo alikuwa nani?

Jibu


Apolo alikuwa mwinjilisti, mtetezi wa dini, kiongozi wa kanisa, na rafiki wa Mtume Paulo. Apolo alikuwa Myahudi kutoka Iskanderia, Misri, anaelezewa kuwa "mwenye usemi," hodari katika Maandiko, "mwenye nguvu kiroho" na "alifundishwa njia ya Bwana" (Matendo 18:24). Katika AD 54, alisafiri Efeso, ambako alifundisha kwa ujasiri katika Hekalu la Kiyahudi. Ingawa, wakati huo, uelewo wa Apololi wa injili haukuwa umekamilika, kwa sababu alikuwa "naijua ubatizo wa Yohana pekee" (Matendo 18:25). Hii ina maana kwamba Apolo alitangaza toba na imani katika Masihi-pengine aliamini kwamba Yesu wa Nazareti alikuwa Masihi-lakini hakuwa uzito wa kifo na ufufuo wa Yesu. Akila na Prisila, marafikize Paulo, walitumia muda wao pamoja na Apolo na kujaza pengo la upungufu wa ufahamu wake wa Yesu Kristo (Matendo 18:26). Apolo, ambaye sasa alikuwa na ujumbe kamili, mara moja alianza huduma ya kuhubiri na alitumiwa na Mungu kama mtetezi wa wa injili (Matendo 18:28).

Apolo alisafiri kupitia Akaya na hatimaye akapata kufika mji wa Korintho (Mdo. 19: 1), ambako "alikuwa mnyunyizi" wa mbegu ambayo Paulo alikuwa "amepanda" (1 Wakorintho 3: 6). Hili ni la muhimu kumbuka wakati wa kusoma barua ya kwanza ya Wakorintho. Apolo, pamoja na karama yake ya asili, alikuwa amevutia umati katika kanisa la Korintho, lakini mvutio huo rahisi uliekea kuigawanya kanisa. Kunyume na matarajio ya Apolo, kulikuwa na kikundi Korintho kilichomchukulia kuwa baba yao wa kiroho, huku wakikosa kumtambua Paulo na Petro. Paulo anashugulikia mgagwanyiko huu katika 1 Wakorintho 1: 12-13. Kristo hagwaganyiki, wala hatupaswi kugawanyika. Hatuwezi kupenda utu dhidi ya ukweli.

Kutajwa kwa kwa Apolo kwingine katika Biblia kunatokea katika barua ya Paulo kwa Tito: "Zena, yule mwana-sheria, na Apolo, uwasafirishe kwa bidii, wasipungukiwe na cho chote" (Tito 3:13). Kwa wazi, Apolo alikuwa anasafiri kupitia krete (ambapo Tito alikuwa) wakati huu. Kwa wazi, Paulo bado alimchukulia Apolo kuwa mshirika wa thamani na Rafiki katika huduma.

Wengine wanaamini kwamba Apolo hatimaye alirejea Efeso kutumikia kanisa pale. Inawezekana kuwa kwamba alirejea, ijapokuwa hatuna uthibitisho wa kibiblia wa maelezo haya. Pia, wengine humtambua Apolo kama mwandishi asiyejulikana wa kitabu cha Waebrania; tena, hamna uungwaji wa Kibiblia kwa utambulisho kama huo. Mwandishi wa Waebrania bado hajulikani.

Kwa ufupi, Apolo alikuwa mtu aliyesafirisha barua na aliyekuwa na bidii kwa Bwana na karama ya kuhubiri. Alijitolea katika kazi ya Bwana, akisaidia huduma ya mitume na kwa uaminifu aliimarisha kanisa. Maisha yake yanapaswa kutuhamasisha kila mmoja wetu "kueni katika neema, na katika kumjua Bwana" (2 Petro 3:18) na kutumia karama zetu za Mungu ili kukuza ukweli.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Apolo alikuwa nani?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries