settings icon
share icon
Swali

Adamu alikuwa nani katika Biblia?

Jibu


Adamu alikuwa mwandamu wa kwanza aliye wai ishi (Mwanzo 1:27; 1 Wakorintho 15:45). Aliumbwa na Mungu kama mwanadamu wa kwanza na kuwekwa katika bustani mwa Edeni iliyoundwa kwa ajili ya manufaa yake (Mwanzo 2: 8, 10). Adamu ndiye baba wa watu wote; kila mwanadamu ambaye amewahi ishi ni mzao wa moja kwa moja wa Adamu, na ni kupitia kwa Adamu kila mwanadamu amerithi asili ya dhambi (Warumi 5:12).

Mungu alizungumza neno na kila kitu kikawa ulimwenguni (Mwanzo 1). Lakini siku ya sita Mungu akafanya kitu tofauti. Alichukua udongo na akamfanya Adamu kutoka udongo (jina Adamu ni linahusiana na adamah, neno la Kiebrania linalotumika kwa "ardhi" au "udongo"). Mungu kisha akapumua pumzi yake mwenyewe katika pua za mwanadamu, "na mtu akawa nafsi iliyo hai" (Mwanzo 2: 7). Pumzi ya Mungu ndiyo inayowatofautisha wanadamu kutoka kwa ufalme wa wanyama (Mwanzo 1: 26-27). Tukianzia kwa Adamu, kila mwanadamu aliyeumbwa tangu wakati huo ana roho isiyoweza kufa kama vile Mungu ilivyo. Mungu aliumba kiumbe kama Yeye ili mwanadamu aweze kufikiria, kutafakari, hisia, na kufanya uamuzi wake mwenyewe.

Mwanamke wa kwanza ambaye ni Hawa, aliumbwa kutoka kwa ubavu mmoja wa Adamu (Mwanzo 2: 21-22). Mungu akawaweka katika ulimwengu wake mkamilifu, na sharti moja tu: hawakupaswa kula kwa mti wa ujuzi wa mema na mabaya (Mwanzo 2: 16-17). Chaguo la Adamu la kutotii lilikuwapo, kwa sababu bila uwezo huo wa kufanya uamuzi, mwadamu basi hangekuwa huru kabisa. Mungu aliwaumba Adamu na Hawa kama viumbe wa kweli, na aliwaruhusu kuwa na uhuru wa kufanya uamuzi.

Mwanzo 3 inaeleza kwa upana uamuzi wa kutenda dhambi wa Adamu. Adamu na Hawa wote waliasi amri ya Mungu na wakala kutoka mti ambao Bwana aliwakataza (mstari wa 6). Kwa sababu ya hilo tendo la kutotii, walileta dhambi ulimwenguni ambao Mungu aliuumba mkamilifu. Kupitia kwa Adamu, dhambi iliingia ulimwenguni, na kupitia dhambi kifo kikaja ulimwenguni (Mwanzo 3:19, 21; Warumi 5:12).

Tunajua kwamba Adamu alikuwa mtu halisi, sio mfano, kwa sababu anajulikana kwetu kama mtu halisi katika Biblia yote (Mwanzo 5: 1; Warumi 5: 12-17). Luka, mwanahistoria mkuu, anafuatilia ukoo wa Yesu kwenda nyuma hadi kwa huyu mtu mmoja (Luka 3:38). Zaidi ya Adamu kuwa mtu halisi, Adamu pia ni mfano wa watu wote watakaokuja. Manabii, makuhani, na wafalme, walizaliwa na asili ya dhambi, wote walikuwa watoto wa Adamu wa kwanza. Yesu, mzaliwa na bikira na asiye na dhambi, ni "Adamu wa pili" (1 Wakorintho 15:47). Adamu wa kwanza alileta dhambi ulimwenguni; Adamu wa pili alileta uzima ulimwenguni (Yohana 1: 4). Yesu, Adamu wetu wa pili, hutupa nafasi ya kuzaliwa upya (Yohana 3: 3) iliyo na asili mpya na maisha mapya kwa yeyote anayemwamini (2 Wakorintho 5:17; Yohana 3: 16-18). Adamu aliipoteza paradiso; Yesu atairejesha tena.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Adamu alikuwa nani katika Biblia?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries