settings icon
share icon
Swali

Je, ni matukio gani makuu katika maisha ya Yesu Kristo (sehemu ya 3)?

Jibu


Yanayofuata ni yaliyojiri kwenye uhai wa Kristo na nakala za Maandiko ambako yote yamechanganuliwa: (Sehemu ya 3)

Chakula cha mwisho: (Mathayo 26: 1-30, Marko 14: 12-26; Luka 22: 7-38; Yohana 13: 1-38) – Mkusanyiko huu wa hatima na wafuasi wake,aliowaenzi, wanaanza na funzo kutoka kwa Kristo. Wafuasi walinungunika kuhusu nani miongoni mwao alimzidi mwingine (Luka 22:24), wakiweka wazi hisia sizizo za kimungu. Kwa kimya Kristu akainuka na kuanza kusafisha vikanyagio vyao, jukumu kwa kawaida lilifanikishwa na wanyonge, mjakazi mdogo. Kutenda hivyo, aliwaambia kuwa wanafunzi wake ni wale waliotoa huduma kwa wengine, wala si wanaongoja kufanyiwa. Hakukoma kufafanua kwamba, kama si Mwana-Kondoo wa Mungu atoleaye mtu makosa, mja huyo hatakuwa nadhifu: "kama sitakutawadha, huna shirika nami" (Yohana 13: 8). Katika lishe la mwisho, Kristo akafahamu msaliti, Yuda, atakayemtoa kwa watawala na kusababisha kushikwa kwake. Wafuasi wake wakakasirishwa Kristo aliponena kuwa mmoja wao atamsaliti Yeye na kushangaa kuwa nani angekuwa. Waliendelea kushangaa hata pale Kristo alionyesha kuwa ni Yuda, aliyeamrisha kutoka mbio na kuharakisha alichotakiwa kutenda. Yuda alipoenda, Kristo akatimiza Agano Jipya kwenye damu yake hata kupeana sheria mpya kuwa watakaomwandama wanafaa kupendana na kuishi katika ukuu wa Roho Mtakatifu. Tunataakari kutolewa kwa Agano Jipya na Kristo mara tu tunajitosa kwenye kushiriki komunio ya Kikristo, kusherekea mwili wa Yesu uliopeanwa kwa sababu yetu na damu yake iliyomwagika kwa ajili yetu.

Kushikwa kule Gethsemane: (Mathayo 26: 36-56, Marko 14: 32-50; Luka 22: 39-54; Yohana 18: 1-12) — Yesu alitanguliza wafuasi wake kuelekea shamba la Gethsemane, walipomaliza chakula cha jioni, na pale matukio kadhaa yakatendeka. Kristo akajitoa mwiongoni mwao ili afanye kusali, kuwasihi kukesha na kusali vile vile. Ila mara nyingi aliporejea aliwapata wameshikwa usingizi, wamechoka na kushikwa na hamaki kuhusu kumpoteza Yeye. Yesu alipoendelea kusali, alimsihi Baba kumtolea kikombe cha ghadhabu alichokuwa akikinywea pale Bwanaalipommwagia dhambi zote za dunia juu yake. Ila,ilivyo mambo yote, Kristo alinyenyekea kwa makadirio ya Baba yake na akaanza kupanga kwa mauti yake, akipata nguvu kutoka kwa malaika aliyemtumwa kumfanyia nyakati zake za mwisho. Yuda aliwasili na halaiki na akamtambua Kristo kwa kumbusu, na Yesu akashikwa na kuchukuliwa kwa Kayafa kwa minajili ya mfululizo wa majaribu.

Kusulibiwa na kuzikwa: (Mathayo 27: 27-66, Marko 15: 16-47, Luka 23: 26-56; Yohana 19: 17-42) –Mauti ya Kristo msalabani yalikuwa hatima ya kazi zake ulimwenguni. Maanake alizaliwa vile vile binadamu-ili kuariki kwa minajili ya madhara ya dunia ili watakaomwamini wasipotee ila wapate uzima wa daima (Yohana 3: 16-18). Alipopatikana asiye na makosa kwa mashtaka aliyohusishwa, Yesu alipeanwa kwa Warumi ili asulubiwe. Matendo yote ya siku hiyo yamenakiliwa yakiwemo matamshi yake saba ya mwisho, matusi na kejeli kutoka kwa halaiki na askari, kupigania mavazi yake miongoni mwa askari, na saa matatu ya giza. Nyakati hizo Kristo akatoa mtima wake, kukawa na tetemeko la ardhi, na kitambaa kikubwa, kilichotenganisha patakatifu kutoka kwa mahali pengine pa hekalu likararuka mara mbili,kudhihirisha kuwa kufikia Bwana sasa kulikuwa huru kwa waliomwamini Kristo. Mwili wa Yesu ukashushwa kutoka msalabani, ukatiwa kwenye kaburi lililoombwa, na kuachwa kule hadi baada ya Sabato.

Ufufuo {Mathayo 28:1-10;Mark 16:1-12;Yohana 20:1-10}. Hakuna mengi kwenye Maandiko kuhusu ufufuo kamili kwa kina kama ilivyo kuhusu kuwa wazi kwa kaburi lake na pia kuwa Kristo alivyo fufuka. Zaidi inadokeza kujitokeza kwake miongoni mwa wengi. Tunajua kuwa Kristo ametoka kaburini pale wake walifika kaburini alikokuwa amesitiriwa kutayarisha mwili wake kwa kuzikwa. Katika Injili zote zinanakiri mambo tofauti kuhusiana na kauli hii. Kimthsari, kaburi halikuwa na chochote, wake wale wakashikwa na butwaa,ndipo malaika akaakikishia kuwa Kristu aliyashinda mauti. Ndipo Kristu akajionyesha kwao. Petro na Yohana vile vile wakahakikisha kuwa kaburi hilo halikuwa na kitu, na Kristu akajidhihirisha kwa wafuasi vile vile.

Kuonekana baada ya kufufuka: (Mathayo 28: 1-20; Marko 16: 1-20; Luka 24: 1-53; Yohana 20: 1-21: 25; Matendo 1: 3; 1 Wakorintho 15: 6) – Pamoja na nyakati za siku arobaini kati ya kusulubiwa na kupaa kwake, Kristu alijionyesha mara mingi kwa wafuasi wake 500 na wengine. Mwanzo alijionyesha kwa wake karibu na kaburini waliofika kutayarisha mwili wake ili kuzikwa, ndipo kwa Maria Magdalene, aliyemhakikishia kuwa hajapaa kwenda kwa Baba. Kristo tena akajionyesha kwa waume wawili njiani wakielekea Emau na, alipokula nao na kusema nao, wakamtambua. Waume wale wakarejea Yerusalemu, kupatana na wafuasi, na wakashuhudia kuhusu kutangamana kwao na Krtistu. Alitembea kwa ukuta na kujitokeza kwa wafuasi kule Yerusalemu ambapo "Tomasi asiyeamini" alipata hakikisho na pia Galilaya waliposhuhudia muujiza mwingine. Hata kama walivua usiku kucha na kukosa kitu, Yesu aliwaamuru kushusha nyavu zao mara nyingine, na nyavu zao zikawa na samaki wengi mno. Kristu akawatayarishia kiamsha kinywa na kuwaambia ukweli wa maana. Petro aliamrishwa kulisha wa Mungu na kujuzwa kio chako kitakavyokuwa. Mara hii pia wakapewa ukuu wa kiroho.

Kupaa: (Marko 16: 19-20; Luka 24: 50-53; Matendo 1: 9-12) – Tendo la omega la Kristu ulimwenguni lilikuwa kupaa kwake mbinguni machoni pa wafuasi wake. Alitwaliwa ndani ya mawingu alipofichwa kutoka machoni pao, ila malaika wawili wakajitokeza kuwajuza kuwa atarejea siku moja vivyo hivyo alivyochukuliwa. Ila wakati huu, Kristu amekaa kwenye kulia kwa Baba yake mbinguni. Hali hiyo ya kukaa chini inadhihirisha kuwa majukumu yake yaliisha, alivyohakikisha akiwa msalabani alivyonena, "Yameisha." Hamna la Zaidi kutendwa ili kumiliki ukombozi kwa wanaoamini Yeye. Maisha yake ulimwenguni yamekamilika, bei imelipwa, ushindi kapatikana, na mauti pia yakashindwa. Haleluya!

Ufufuo: (Mathayo 28: 1-10; Marko 16: 1-11; Luka 24: 1-12; Yohana 20: 1-10)

"Kuna na mambo mengi aliyoyafanya Yesu; ambayo yakiandikwa moja moja, nadhani hata ulimwengu usingetosha kwa vile vitabu vitakavyoandikwa."(Yohana 21:25).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, ni matukio gani makuu katika maisha ya Yesu Kristo (sehemu ya 3)?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries