settings icon
share icon
Swali

Je! Kuna toafuti gani kati ya kanisa linaloonekana na lile lisilo oonekana?

Jibu


Biblia kamwe haitumii neno kanisa linaloonekana na lisilo onekana. Lakini dhana ya kanisa linaloonekana dhidi ya lile lisilo onekana kawaida ni matokeo ya kukosa kuelewa kanuni ya wokovu. Kanisa linalo onekana, ni dhihirisho la Ukristo ambao watu wanaweza kuona: mkutaniko na matendo ya mtu binafsi katika majengo mbali mbali ya kanisa siku ya Jumapili. Kanisa lisiloonekana ni kanisa la kweli, ambalo ni Mungu tu anayeweza kuliona: waumini waliozaliwa mara ya pili, wa zamani, wa sasa, na wa baadaye. Kwa sababu sio kila mtu anayehudhuria kanisa au anayefanya matendo ya kidini ameokoka, kanisa linaloonekana linajumuisha wasioamini. Kanisa lisiloonekana linajumuisha waliokombolewa na kutiwa muhuri na Mungu.

Kwa njia zingine, dhana ya kanisa linaloonekana/lisiloonekana zinahusiana na dhana ya kanisa la mtaa/ulimwengu. Tofauti ni kwamba kanisa la mtaa linamaanisha kusanyiko moja linalokusanyika katika jengo moja; kanisa linaloonekana linajumuisha makanisa yote ya eneo moja, kila mahali.

Kanisa linaloonekana hutambulika kwa urahisi kwa vitambulisho vyake vya kidini: majengo ya kanisa, wahudumu au makasisi, kalenda, maagizo, sherehe, madhehebu, n.k. Wakati mtu anasema, "Huwa ninahudhuria Kanisa hili," anamaanisha kanisa linaloonekana. Wakati mtu anaendesha gari karibu na ziwa na kuona watu fulani wakibatizwa, wanaangalia sehemu ya kanisa linaloonekana.

Kujitambulisha na kanisa linaloonekana ni kukubali anwani ya "Mkristo," lakini, bila mabadiliko ya kiroho yaliyoanzishwa na Roho wa Mungu, na hiyo ndio anwani pekee. Ukristo wa jina tu hujaza sehemu kubwa ya kanisa linaloonekana. Dema alimwacha Paulo "kwa sababu aliupenda ulimwengu huu" (2 Timotheo 4:10); Dema alikuwa sehemu ya kanisa linaloonekana kwa muda, lakini hakuwa sehemu ya kanisa lisiloonekana, na mwishowe alionyesha hilo (angalia 1 Yohana 2:19).

Kanisa lisiloonekana, linajumuisha wale wote waliokombolewa, ni la kiroho na la kimbingu na sio la ulimwengu huu (Yohana 18:36). Kama Yesu alivyoelezea, "Ufalme wa Mungu hauji kwa kuchunguza kwa bidii, 21wala watu hawatasema, 'Huu hapa,' au 'Ule kule,' kwa maana Ufalme wa Mungu umo ndani yenu." (Luka 17: 20-21).

Kanisa linaloonekana haliitaji vikorokoro ambavyo huifanya kanisa linaloonekana lionekane. Ikiwa utaondoa liturujia kutoka kwa kanisa linaloonekana, kanisa lisiloonekana litabaki. Sherehe za kidini hazileti tofauti kwa kanisa lisiloonekana: "Kwa maana katika Kristo Yesu, kutahiriwa au kutokutahiriwa si kitu, bali kule kuwa kiumbe kipya ni kila kitu!" (Wagalatia 6:15). Ikiwa mtu anateketeza jengo la kanisa, waumini bado wanabaki kuwa kanisa.

Vitu vinavyoonekana vya dunia hii, ni pamoja madhehebu ya makanisa, majengo ya makanisa, tenzi, vitabu vya maombi na viti, vyote vitapita kwa sababu ni vya muda (1 Wakorintho 7:31). Vitu vya Mungu visivyoonekana haviwezi pita kwa sababu ni vya milele kama vile mbinguni ni ya milele (Luka 12:33).

Katika Yohana 4:20 mwanamke Msamaria pale kisimani, "Baba zetu waliabudu kwenye mlima huu, lakini ninyi Wayahudi mnasema ni lazima tukaabudu huko Yerusalemu." Kwa maneno yetu, mwanamke msamaria alikuwa anasungumzia kanisa linaloonekana. Yesu alimjibu kwa kufafanua kanisa lisiloonekana: "Yesu akamjibu, "Mwanamke, niamini, wakati unakuja ambapo hamtamwabudu Baba katika mlima huu, wala huko Yerusalemu… Lakini saa yaja, tena ipo, ambapo wale waabuduo halisi, watamwabudu Baba katika roho na kweli. Watu wanaoabudu namna hii, ndio Baba anawatafuta. Mungu ni Roho na wote wanaomwabudu imewapasa kumwabudu katika roho na kweli" (Yohana 4:21-24).

sisi wote tunapaswa kumfanya Mungu "aonekane" kwa ulimwengu ambamo tunaishi, "kwa maana Mungu ndiye atendaye kazi ndani yenu, kutaka kwenu na kutenda kwenu kwa kulitimiza kusudi lake jema" (Wafilipi 2:13). Kufanya hivyo, ni lazima tuwe sehemu ya kanisa lisiloonekana, "alitufanya…hai pamoja na Kristo Yesu…kutuketisha pamoja naye katika ulimwengu wa roho" (Waefeso 2:5-6).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Kuna toafuti gani kati ya kanisa linaloonekana na lile lisilo oonekana?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries