settings icon
share icon
Swali

Karama ya kiroho ya unabii ni gani?

Jibu


Karama ya kiroho ya unabii imeorodheshwa kati ya karama za Roho katika 1 Wakorintho 12:10 na Warumi 12: 6. Neno la Kiyunani linalotafsiriwa "kutoa unabii" au "unabii" katika vifungu vyote viwili linamaanisha "kuzungumza" au kutangaza mapenzi ya Mungu, kutafsiri malengo ya Mungu, au kuifanya kwa njia yoyote ile ukweli wa Mungu ambao umepangwa kuwa na ushawishi kwa watu. Watu wengi hawaelewi karama ya unabii wanaichukulia kuwa uwezo wa kutabiri ya baadaye. Kuwa na uwezo wa kutabiri mambo yajayo, wakati mwingine huenda ukawa ni kipengele cha karama ya unabii, ilikuwa hasa karama ya kutangaza ("kutoa habari"), sio utabiri ("utangulizi").

Mchungaji / mhubiri ambaye anayetangaza Biblia anaweza kuchukuliwa kuwa "mtabiri" kwa kuwa anasema ushauri wa Mungu. Pamoja na kukamilika kwa kifungu cha Agano Jipya, unabii ulibadilishwa kutoka kutangaza ufunuo mpya hadi kwa kutangaza ufunuo uliokamilika ambao Mungu ametoa tayari. Yuda 3 inazungumzia "imani ambayo Mungu amewajalia watu wake mara moja tu kwa wakati wote" (msisitizo aliongeza). Kwa maneno mengine, imani tuliyoshikilia imetatuliwa milele, na haina haja ya kuongezewa au kusafishwa inayotokana na mafunuo ya ziada ya kibiblia.

Pia, kumbuka mabadiliko kutoka kwa nabii hadi mwalimu katika 2 Petro 2: 1: "palitokea manabii wa uongo kati ya watu, na vivyo hivyo waalimu wa uongo watatokea kati yenu" (msisitizo aliongeza). Petro anaonyesha kwamba kizazi cha Agano la Kale kilikuwa na manabii, huku kanisa litakuwa na walimu. Karama ya kiroho ya unabii, kwa maana ya kupokea mafunuo mapya kutoka kwa Mungu ili kutangazwa kwa wengine, ilikoma baada ya kukamilika kwa Biblia. Wakati huo unabii ulikuwa ni karama ya kufunuliwa, ulipaswa kutumika kwa ajili ya kujenga, kuhimiza, na faraja kwa wanadamu (1 Wakorintho 14: 3). Karama ya kisasa ya unabii, ambayo anaangazia kufundisha, bado inasema ukweli wa Mungu. Chenye kimebadilika ni kwamba kweli ya Mungu leo hii imefunuliwa kikamilifu katika Neno Lake, huku, katika kanisa la kwanza, halikuwa limefunuliwa kikamilifu.

Wakristo wanapaswa kuwa na wasiwasi sana kwa wale wanaodai kuwa na "ujumbe mpya" kutoka kwa Mungu. Ni jambo moja kusema, "Nilikuwa na ndoto ya kuvutia usiku jana." Hata hivyo, ni jambo lingine na kusema, "Mungu alinipa ndoto jana usiku, na lazima uitii." Hakuna usemi wa mtu yeyote unaopaswa kuchukuliwa kuwa sawa na au juu ya Neno lililoandikwa. Tunapaswa kushikilia Neno ambalo Mungu ametoa tayari na kujitolea wenyewe kwa maandiko ya kibilia pekee.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Karama ya kiroho ya unabii ni gani?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries