settings icon
share icon
Swali

Je! Kanuni ya utimilifu ni nini?

Jibu


Utimilifu ni mafundisho kwamba uanaume na uke umewekwa na Mungu na kwamba wanaume na wanawake wameumbwa ili kukamilishana, au kutimishana. Wakamilishaji wanaamini kwamba majukumu ya kijinsia yanayopatikana katika Biblia ni ya kusudi na ya maana tofauti ambayo kwayo, ikiwa yanatumika pale nyumbani na kanisani, yatakuza ubuheri wa kiroho kwa wanaume na wanawake. Kukumbatia majukumu yaliyowekwa na Mungu ya wanaume na wanawake huendeleza huduma ya watu wa Mungu na itaruhusu wanaume na wanawake kufikia uwezo wao waliopewa na Mungu.

Mtazamo wa ukamilisho huanza na Mwanzo 1: 26-27, ambayo inasema kwamba Mungu aliumba wanadamu, mwanamume na mwanamke, kwa mfano Wake mwenyewe. Mwanzo 2:18 ina maelezo zaidi kwamba Mungu alimuumba Hawa haswa ili kumsaidia Adam: "Si vyema huyu mtu awe peke yake. Nitamfanyia msaidizi wa kumfaa." Kwa hivyo hizo jinsia mbili ni sehemu ya uumbaji taratibu wa Mungu. Upungufu wowote wa siku hizi wa jinsia au upotovu wa majukumu ni matokeo ya Kuanguka.

Utimilifu hufuata Waefeso 5: 21-33 kama kielelezo cha familia. Mume ana jukumu la uongozi katika familia. Anapaswa kumtunza mkewe na kuongoza familia yake kwa upendo, unyenyekevu, na kwa kujitolea. Mke naye ana jukumu la kuwalea watoto wake kwa kukusudia, akijiwasilisha kwa hiari kwa uongozi wa mumewe. Wakati wote wawili mume na mke wanakamilishana kwa njia hii, Kristo anatukuka. Kwa kweli, ndoa yenyewe inakuwa vile ilivyopangwa kuwa: taswira halisi ya Kristo na kanisa (aya ya 32).

Katika anisani, utimilifu hufuata 1 Timotheo 2: 11—3: 7 na Tito 2: 2-6 kama mfano. Kibiblia, wanaume kanisani wana jukumu la kutoa uongozi wa kiroho na mafunzo. Wanawake wanapaswa kutumia vipaji vyao vya kiroho kwa njia yoyote ambayo Maandiko yanaruhusu — katazo pekee lililoko ni "Simpi mwanamke ruhusa ya kufundisha au kuwa na mamlaka" (1 Timotheo 2:12). Pindi wanaume na wanawake wanapotimiza majukumu yao waliyopewa na Mungu ndani ya kanisa, Kristo anatukuka. Kwa kweli, kanisa lenyewe linakuwa kile ilichopangwa kuwa: taswira halisi ya mwili wa Kristo (1 Wakorintho 12: 12-27).

Mtazamo unaopinga fundisho la utimilifu ni mtazamo wa usawa, ambao unafundisha kwamba, katika Kristo, hakuna tofauti za kijinsia. Wazo hili linatokana na Wagalatia 3:28. Kwa sababu waumini wote ni mwili mmoja katika Kristo, wanaoshikilia dhana ya usawa wanasema, majukumu ya wanaume na wanawake hubadilishana katika uongozi wa kanisa na katika majukumu ya familia. Mtazamo wa Usawa unaona tofauti za kijinsia kuwa matokeo ya Kuanguka na ukombozi wa Kristo kuwa wa kuondoa tofauti hizo, na kuleta umoja. Ukamilishaji huona tofauti za kijinsia kuwa hivyo kwa ajili ya matokeo ya Uumbaji na ukombozi wa Kristo kuwa wa kurejesha tofauti hizo, bila kuleta mkanganyiko. Paulo anajiunga na wafuasi wa itimilifu katika kutaja utaratibu wa uumbaji kama msingi wa mafundisho yake: "Kwa maana Adamu aliumbwa kwanza, kisha Hawa" (1 Timotheo 2:13).

Tofauti katika majukumu hailingani na tofauti ya ubora, umuhimu, au thamani. Wanaume na wanawake wanathaminiwa sawia machoni pa Mungu na katika mpango Wake. Ukamilishaji hutafuta kuhifadhi tofauti za kibiblia kati ya majukumu ya wanaume na wanawake huku ukithamini ubora na umuhimu wa jinsia zote. Matokeo ya kweli ya utimilifu ni heshima kwa Kristo na umoja kanisani na nyumbani.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Kanuni ya utimilifu ni nini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries