settings icon
share icon
Swali

Kanoni ya maandiko ni gani?

Jibu


Neno "kanoni" linatokana na utawala wa sheria ambayo ilitumika kuamua kama kitabu kimepimwa hadi kiwango kamili. Ni muhimu kutambua kwamba uandishi wa maandiko ulikuwa wa kisheria wakati yaliandikwa. Biblia ilikua maandiko wakati kalamu iliiguza ngozi. Hii ni muhimu sana kwa sababu Ukristo haujaanza kwa kufafanua Mungu ni nani, au Yesu Kristo, au wokovu. Misingi ya Ukristo hupatikana katika mamlaka ya Maandiko. Kama tunaweza kutambua kile maandiko yanasema, basi tunaweza vizuri kutofautisha ukweli wowote kiteolojia kutoka katika makosa.

Ni kipimo au kiwango gani kilitumiwa kuamua ni vitabu gani lazima viwekwe katiak kundi la maandiko? Mstari muhimu katika kuelewa utaratibu na nia, na labda muda wa utoaji wa maandiko, ni Yuda 3 ambayo inasema kwamba imani ya Kikristo ya "ili niwaonye kwamba mwishindanie imani waliyokabidhiwa watakatifu mara moja tu." Tangu imani yetu inaelezwa na maandiko, Yuda kimsingi anasema kwamba maandiko yalipeanwa mara moja kwa manufaa ya Wakristo wote. Je, si ni ajabu kujua kwamba hakuna siri au kumbukumbu ambzo zimepotea na zitapatikana bado, hakuna vitabu vya siri ambavyo vinajulikana tu na wachache, na hakuna watu hai ambao wana ufunuo maalum unaotuhitaji sisi tufasiri hadi mlima wa Himalayani ili kuwa mwanga? Hatuwezi kuwa na uhakika kwamba Mungu hakutuacha sisi bila ushahidi. Nguvu hiyo hiyo isiyo ya kawaida Mungu alitumia kuzalisha neno lake pia imekuwa imetumika kwa kulihifadhi.

Zaburi 119:160 inasema kwamba ukamilifu wa neno la Mungu ni kweli. Kuanzia na ile nguzo, tunaweza kulinganisha maandiko nje ya ile kanoni ambayo imekubaliwa ya maandiko ili kuona kama itahitimu mtihani. Kwa mfano, Biblia inadai kwamba Yesu Kristo ni Mungu (Isaya 9:6-7, Mathayo 1:22-23; Yohana 1:1, 2, 14, 20:28; Matendo 16:31, 34; Wafilipi 2: 5-6, Wakolosai 2:9, Tito 2:13; Waebrania 1:8, 2 Petro 1:1). Hata hivyo maandiko mengi ya ziada ya Biblia hudai kuwa maandiko, yanasema kuwa Yesu si Mungu. Wakati utata wazi upo, Biblia imara ni ya kuaminiwa, na kuacha zingine nje ya nyanja ya maandiko.

Katika karne ya kwanza ya kanisa, Wakristo walikuwa wakati mwingine wanauwawa kwa kuwa na nakala ya maandiko. Kwa sababu ya mateso haya, swali haraka likatokea punde, "Je, vitabu ni vya thamani ya kukufia?" Baadhi ya vitabu vinaweza kuwa na maneno ya Yesu, lakini yaliongozwa kama ilivyoelezwa katika 2 Timotheo 3:16? Mabaraza ya kanisa yalikuwa na jukumu katika kutambua hadharani kanuni ya maandiko, lakini mara nyingi kanisa binafsi au vikundi vya makanisa yalitambua kitabu kuwa na pumzi ya Mungu kutokana na uandishiw wake (kwa mfano, Wakolosai 4:16, 1 Wathesalonike 5:27). Katika karne za mwanzo za kanisa, vitabu chache vilipingwa milele na orodha ikazuluhishwa mwaka wa AD 303.

Wakati ilifikia Agano la Kale, kanuni tatu muhimu zilitiliwa maanani: 1) Agano Jipya lanukuu kutoka au hutambua Agano la Kale mbali na vitabu viwili. 2) Yesu kwa ufanisi alihithinisha kanoni ya Kiebrania katika Mathayo 23:35 wakati Alitoa mfano wa mojawapo ya simulizi kwanza na mojapo ya mwisho katika maandiko ya siku yake. 3) Wayahudi walikuwa wa kina katika kuhifadhi Agano la Kale, na walikuwa na mabishano kidogo sana juu ya ni sehemu gani inastahili au isiyo stahili kuwa katika Biblia. Kanoni ya Kikatoliki haikuweza kujipima na ikaanguka nje ya ufafanuzi wa maandiko na haijawahi kukubaliwa na Wayahudi.

Maswali mengi kuhusu ni vitabu gani vinastahili kuwa katika Biblia ilishughulikiwa na uandishi wa tangu wakati wa Kristo na baadaye. Kanisa la kwanza lilikuwa na baadhi ya vigezo maalum sana ili vitabu kuchukuliwa kama sehemu ya Agano Jipya. Hii ni pamoja na: Je, kitabu kiliandikwa na mtu ambaye alikuwa shahidi wa Yesu Kristo? Je, kitabu kilipita "mtihani wa ile kweli"? (mfano, kilikubaliana na wengine, tayari vilishakubaliwa kuwa katika maandiko?). Vitabu vya Agano Jipya wao walivikubali sasa vimehitimu mtihani wa muda na usahihi wa Kikristo umelikubali jambo hili, pamoja na changamoto kidogo, kwa karne nyingi.

Hujasiri katika tarehe maalumu ya vitabu iliyokubaliwa ilianza karne ya kwanza walioupokea ushahidi wa kwanza kuwa kama uthabiti wao. zaidi, mwisho Mada ya kitabu cha Ufunuo, na kupiga marufuku ya kuongeza neno katika kitabu cha Ufunuo 22:18, inahoji sana kwamba kanuni ulifungwa wakati wa kuandikwa kwake (takribani AD 95).

Kuna hoja muhimu ya kiteolojia ambayo haipaswi kukoswa. Mungu ametumia neno lake katika milenia kwa kusudi moja la kimsingi kujitangaza mwenyewe na kuwasiliana na mwanadamu. Hatimaye, si baraza la kanisa liliamua kama kitabu kilistahili katika maandiko; kwamba kiliamuliwa wakati mwandishi binadamu alichaguliwa na Mungu kukiandika. Ili kufanikisha matokeo ya mwisho, ikiwa ni pamoja na utunzaji wa neno lake katika karne, Mungu Aliliongoza mabaraza la kanisa kwa kuitambua kanoni.

Upatikanaji wa elimu kuhusu mambo kama, asili ya kweli ya Mungu, asili ya ulimwengu na maisha, kusudi na maana ya maisha, maajabu ya wokovu, na matukio ya baadaye (ikiwa ni pamoja na hatima ya wanadamu) ni zaidi ya uchunguzi wa asili na uwezo wa kisayansi wa mwanadamu. Neno tayari limekwisha tolewa na Mungu, ylnye thamani ya binafsi na kutumiwa na Wakristo kwa karne nyingi, ni ya kutosha kutueleza sisi kila kitu tunahitaji kujua kuhusu Kristo (Yohana 5:18; Matendo 18:28, Wagalatia 3:22; 2 Timotheo 3: 15) na kutufundisha, kuturekebisha, na kutuongoza katika mambo yote ya haki (2 Timotheo 3:16 ).

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kanoni ya maandiko ni gani?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries