settings icon
share icon
Swali

Je! Mtu anapaswa kuhudhuria kanisa ndio aende mbinguni?

Jibu


Wokovu hupatikana katika Kristo. "Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele" (Yohana 3:16). Mungu alitoa Mwanawe ili tuweze kuwa na uzima wa milele, hivyo kuharibu haja yetu ya kufanya kazi njema, ikiwa ni pamoja na kwenda kanisa, kwenda mbinguni. Uzima wa milele hupatikana kwa imani pekee katika Kristo pekee. "Yeye aliye naye Mwana, anao huo uzima; asiye naye Mwana wa Mungu hana huo uzima" (1 Yohana 5:12). Wale wanaomwamini Kristo, ambao wamekubali dhabihu yake kuwa ililipa dhambi zao, watakuwa na milele mbinguni. Wale wanaomkataa hawatakuwa.

Hakuna kiasi cha kuhudhuria kanisa kinaweza kumpatia mtu mbinguni milele. Hakuna kukosekana kwa mahudhurio ya kanisa kutasababisha kupoteza wokovu. Hata hivyo, kukosa kuhudhuria kanisa hakuwezi mfanya mtu apoteze woko wake. Ingawa, kuhudhuria kanisa ni muhimu. Kanisa la ulimwengu mzima, ambalo linaundwa na wote wanaomwamini Kristo kwa utukufu wa Mungu Baba, ni mwili wa Kristo (Wakolosai 1:18) pamoja na Bibi arusi (Ufunuo 21: 2). Kanisa ni mahali pa ushirika wa Kikristo. Aidha, kama wanachama wa mwili wa Kristo, tuna zawadi fulani za Roho, na tunapaswa kutumia vipawa hivyo kwa ajili ya utukufu wa Mungu na kuimarisha mwili wote. Ili mwili wa kanisa ufanye kazi vizuri, sehemu zake zote za mwili zinahitajika kuwepo (1 Wakorintho 12: 14-20).

Wakristo wamefanywa "viumbe vipya" katika Kristo (2 Wakorintho 5:17) na kuwa na hamu ya kuhudhuria kanisa kwa sababu wanafahamu kuwa kufanya hivyo ni muhimu kwa maendeleo yao ya kiroho na ukuaji. Kusita sita katika mahudhurio ya kanisa kunaweza kuonyesha ukosefu wa ukuaji wa kiroho au kukosa ukweli kwa "dini iliyoandaliwa." Kwa kweli kuna makanisa ya uwongo leo hii, na hakuna kanisa kamilifu, lakini kuna miili ya waumini katika jamii nyingi. Kanisa la kweli, la ulimwenguni pote linaiga mkutaniko ambao mafundisho yake yanategemea maandiko, yanayomheshimu Kristo katika vitu vyote, wanaomwabudu Mungu pamoja, na ambao uhudumiana. Ingawa mahudhurio ya kanisa hayatahakikishia uzima wa milele, ingawa kutafuta kanisa la mtaa nzuri ni muhimu kwa Wakristo.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Mtu anapaswa kuhudhuria kanisa ndio aende mbinguni?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries