settings icon
share icon
Swali

Kanisa lilianza lini?

Jibu


Kanisa lilianza siku ya Pentekoste, siku hamsini baada ya Pasaka wakati Yesu alikufa na kufufuka. Neno lililotafsiriwa "kanisa" linatokana na maneno mawili ya Kiyunani ambayo kwa pamoja yanamaanisha "kuitwa kutoka ulimwenguni kwa ajili ya Mungu." Neno hilo linatumika katika Biblia yote kutaja wale wote waliozaliwa tena (Yohana 3: 3) kupitia imani katika kifo na ufufuo wa Yesu (Warumi 10: 9-10). Neno Kanisa, likitumiwa kutaja waumini wote kila mahali, limetumiwa sawia na Mwili wa Kristo (Waefeso 1: 22-23; Wakolosai 1:18).

Neno Kanisa linaonekana kwanza katika Mathayo 16 wakati Yesu anamwambia Petro, "na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda." (Mstari wa 18). "Mwamba" haya ndio maneno ambayo Petro aliyasema, "Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye ha" (mstari wa 16). Kweli hiyo kuhusu Yesu msingi wa kanisa ambalo lime kimekua kwa zaidi ya miaka elfu mbili. Kila mtu anayefanya ukweli huo msingi wa maisha yake huwa mwanachama wa kanisa la Yesu (Matendo 16:31).

Maneno ya Yesu, "Nitajenga kanisa langu," yalikuwa ya kinabii ya kile kilichokuwa kinatendeka wakati alipomtuma Roho Mtakatifu awajaze waumini (Yohana 15: 26-27; 16:13). Yesu alilazimika kwenda msalabani ndio apate kufufuliwa. Ingawa wanafunzi walielewa kwa sehemu fulani, utimilifu wa yote ambayo Yesu alikuja kuyafanya bado hayakamilika. Baada ya kufufuliwa kwake Yesu hakuwaruhusu wafuasi wake kuanza kazi aliyokuwa amewapa, kufanya wanafunzi wa mataifa yote (Mathayo 28: 19-20), hadi pale Roho Mtakatifu alikuwa amewashukia (Matendo 1: 4-5).

Kitabu cha Matendo kinaeleza mwanzo wa kanisa na kuenea kwa miujiza kwa nguvu za Roho Mtakatifu. Siku kumi baada ya Yesu kurudi mbinguni (Mdo. 1: 9), Roho Mtakatifu ukawashukia wafuasi wa Yesu 120 ambao walisubiri na kuomba (Matendo 1:15; 2: 1-4). Wanafunzi wale ambao walikuwa wametetemeka kwa hofu ya kutambuliwa na Yesu (Marko 14:30, 50) walitolewa kwa ghafla kuhubiri Injili ya Masihi aliyefufuka, kuthibitisha ujumbe wao kwa ishara na miujiza ya ajabu (Matendo 2: 4, 38- 41; 3: 6-7; 8: 7). Maelfu ya Wayahudi kutoka sehemu zote za ulimwengu walikuwa Yerusalemu kwa ajili ya Sikukuu ya Pentekoste. Waliposikia injili katika lugha zao (Matendo 2: 5-8), na wengi waliamini (Matendo 2:41; 4: 4). Wale waliokolewa walibatizwa, na kuongezeka kila siku kwa kanisa. Wakati mateso yalipoanza, waumini walitawanyika, wakihubiri ujumbe wa injili, na kanisa likaenea haraka kwa sehemu zote za dunia tunayoijua (Matendo 8: 4; 11: 19-21).

Kuanza kwa kanisa kulihusisha Wayahudi huko Yerusalemu, lakini muda mfupi baadaye kanisa lilienea kwa makundi mengine ya watu. Wasamaria walihubiriwa na Filipo katika Matendo 8. Katika Matendo ya 10, Mungu alimpa Petro maono ambayo yamesaidia kuelewa kwamba ujumbe wa wokovu haukuwa na Wayahudi peke yake bali umefunguliwa kwa mtu yeyote anayeamini (Matendo 10: 34-35, 45). Wokovu kwa towashi wa Kushi (Matendo 8: 26-39) na mkuu wa mamlaka wa Italia Korneliyo (Mdo. 10) aliwasadikisha Wayahudi kuwa kanisa la Mungu lilikuwa pana kuliko walivyofikiri. Wito wa miujiza wa Paulo barabarani akienda Damasko (Matendo 9: 1-19) iliweka hatua kwa kuenea zaidi kwa Injili kwa Wayahudi (Warumi 15:16, 1 Timotheo 2: 7).

Maneno ya unabii ya Yesu kwa Petro kabla ya kusulubiwa yamekuwa ya kweli. Ingawa mateso na "malango ya kusimu" yamelipiga, kanisa linakua na nguvu zaidi. Ufunuo 7: 9 inatoa maelezo ya kanisa kama vile Mungu alivyolipangia liwe: "Baada ya hayo nikaona, na tazama, mkutano mkubwa sana ambao hapana mtu awezaye kuuhesabu, watu wa kila taifa, na kabila, na jamaa, na lugha, wamesimama mbele ya kile kiti cha enzi, na mbele za Mwana-Kondoo, wamevikwa mavazi meupe, wana matawi ya mitende mikononi mwao." Kanisa ambalo Yesu alianza litaendelea hadi siku ile atakaporudi kwetu (Yohana 14: 3, 1 Wathesalonike 4: 16-17) na sisi tuungana naye milele kama bibi harusi wake (Waefeso 5:27) ; 2 Wakorintho 11: 2; Ufunuo 19: 7).

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kanisa lilianza lini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries