settings icon
share icon
Swali

Je! Ninawezaje kutambua kanisa lenye afya?

Jibu


Mungu alianzisha kanisa kama chombo cha msingi cha kuendeleza malengo Yake duniani. Kanisa ni mwili wa Kristo ambalo ni — moyo wa Mungu, mikono, miguu, na sauti inayofikia watu ulimwenguni. Makanisa yenye afya huja katika kila umbo na kiwango. Ingawa ukuaji kiidadi unaweza kuwa ishara ya afya (Matendo 2:47; 5:14; 16: 5), ijapokuwa haidhibitishi ustawi wa kanisa. Uafya wa kanisa hupimwa kwa ukuaji wa kiroho na kibiblia badala ya idadi.

Ingawa hakuna dhehebu au kanisa ni kamilifu, Biblia inawasilisha sifa kadhaa ambazo zitatusaidia kutambua kanisa linalofanana na kiwango cha Mungu:

Kanisa lililo na afya linafunza kanuni halisi msingi wake ukiwa ukweli wote wa Neno la Mungu (Tito 1:9; 2:1; 1 Timotheo 6:3-4; 2 Timotheo 2:2). Wakati waumini wanakutana pamoja, iwe ni kwa ajili ya ibada ya pamoja au kujifunza Biblia, Biblia inafaa kuwa msingi wa mafunzo yake. Ufafanuzi aminifu na utumizi wa kila siku wa mafunzo mema yatazalisha matunda kamili ya maisha ya Kikristo (1 Timotheo 1:10; 4:6; 2 Timotheo 3:15-17). Zingatio la maandiko huhifadhi ustawi wa kanisa vile vile pamoja na uongozi wake (2 Timotheo 1: 13–14; Tito 1: 6–9). Na wakati ukweli wa kibiblia na mafundisho mazuri yanapopewa kipaumbele, kulindwa, na kufundishwa bila maelewano, basi tabia zingine zote za kanisa lenye afya zitafuata kwa urahisi.

Kanisa lenye afya linatambua sifa za viongozi wa kiroho. Kwa mfano, mtu wa Mungu hapaswi kuwa mwenye kiburi, mwepesi wa hasira, mwenye vita, mchoyo, au asiye mwaminifu, bali anapaswa kuwa mwenye kukaribisha wageni, mwenye hekima, mwenye haki, asiye na lawama, amejitunza vizuri and na kujitolea kwa Bwana (Tito 1:6-9; 1 Timotheo 3:1-7).

Kanisa lenye afya litazalisha viongozi wanaomuiga Yesu Kristo, ambaye ndiye kichwa cha kanisa (Waefeso 1: 22-23; 4:15; 5:23 Wakolosai 1:18). Yesu aliongoza kwa kutumikia (Mathayo 20: 25-28; Yohana 13: 12-17). Yesu pia alitumia muda wake mwingi wa miaka mitatu katika huduma akiwasiliana kwa karibu na wale wanafunzi kumi na wawili, akiwafundisha na kuwalea, na kuwaruhusu kuyatazama maisha yake. Viongozi wazuri hutambua na kufundisha viongozi wengine (Matendo 6: 1-7).

Viongozi wa Kibibilia ni wakurugenzi wazuri wa huduma na rasilimali ambazo wamepewa na Mungu (1 Wakorintho 4: 1-3; 9:17; 1 Petro 4:10). Ingawa hatupaswi kutarajia waangalizi wa kanisa lenye afya kuwa wakamilifu, wanapaswa kuwa viongozi wa watumishi ambao wanaoshiriki katika kulea wanafunzi, kuwafunza waumini kwa ajili ya huduma na kuwasaidia watumishi wengine wa Mungu kuwa viongozi wakomavu na wanaomcha Mungu (Waefeso 4: 11-16). ).

Kanisa lenye afya linasisitiza uanafunzi, ambao huzalisha wafuasi waaminifu ambao pia si wakamilifu, lakini ambao wanamjua na kumpenda Mungu na wanatafuta kulitii Neno Lake (Yohana 8: 31-32; 14:15; 1 Yohana 2: 3-6). Uanafunzi unahuzisha kushiriki katika maisha ya kanisa, kujenga uhusiano madhubuti na waumini wengine (Matendo 2: 42-47; 1 Wakorintho 10:17), kutumia karama za huduma na utume (Warumi 12: 4-8; 1 Wakorintho 12: 7), kukua katika utakaso (1 Wathesalonike 4: 3-4; 5:23), na kuzaa matunda (Yohana 15: 5-8).

Kanisa lenye afya linatimiza jukumu lake katika kutii Agizo la Utume Mkuu (Mathayo 28: 19-20) wa kueneza habari njema kwamba Yesu Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, alifufuka kutoka kwa wafu, na sasa anatawala ili kutoa msamaha wa dhambi, maisha mapya katika Roho, na uzima wa milele kwa wote wanaotubu na kuamini. Uinjilishaji unajumuisha kufikia wale walio ndani ya kanisa, utume kwa ulimwengu, na kushiriki injili na watu katika maisha yetu ya kila siku. Kama mabalozi wa Kristo hapa duniani, waumini wameitwa kuwa "sisi ni harufu ya mauti iletayo mauti; lakini kwa wale wanaookolewa, sisi ni harufu nzuri iletayo uzima" (2 Wakorintho 2: 15-16).

Vitambulisho vingine vya kanisa lililo na afya vinaweza kuangaliwa katika kanisa linaloanza katika kitabu cha Matendo (Matendo 2:42-47). Kanisa la kwanza lilikuwa limejitolea kwa mafundisho, kukutana pamoja kwa maombi, ibada, na kuumega mkate. Wakrito hawa wa kwanza kwa ukunjuvu walijitolea wao kwa wao huku wakiunda msingira ya upendo ambapo waumini walijali mahitaji ya kila mmoja. Kanisa lenye afya hii leo lazima lionyeshe msisimko huo kwa kuishi maisha halisi ya Kikristo na kushiriki katika makusudi na kazi ya ufalme wa Mungu hapa duniani.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Ninawezaje kutambua kanisa lenye afya?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries