settings icon
share icon
Swali

Nitazingatia nini ninapotafuta kanisa?

Jibu


Ili kujua nini cha kuangalia katika kanisa la mtaa, lazima kwanza tuelewe kusudi la Mungu kwa kanisa-mwili wa Kristo-kwa ujumla. Kuna mambo mawili ya kweli juu ya kanisa. Kwanza, "kanisa la Mungu aliye hai [ni] nguzo na msingi wa kweli" (1 Timotheo 3:15). Pili, Kristo peke yake ndiye kionozi wa kanisa (Waefeso 1:22; 4:15; Wakolosai 1:18).

Kwa kweli, kanisa la mtaa ni mahali ambapo Biblia (Kweli wa Mungu pekee) una mamlaka kamili. Biblia ndiyo kanuni pekee ya imani na matendo(2 Timotheo 3: 15-17). Kwa hiyo, tunapotafuta kanisa ya kushiriki, tunapaswa kutafuta moja ambapo, kwa mujibu wa viwango vya kibiblia, injili inenezwa, dhambi imekataliwa, ibada inatoka moyoni, mafundisho ni ya kibiblia, na fursa ya kuwahudumia wengine kuwepo. Fikiria mfano wa kanisa la kwanza linalopatikana katika Matendo 2: 42-47, "Hawa wote waliunda kujifunza kutoka kwa mitume, kuishi pamoja kindugu, kumega mkate na kusali." Walimtukuza Mungu, wakapendwa na watu wote. Kila siku Bwana aliwaongezea idadi ya watu waliokuwa wakiokolewa."

Kuhusu ukweli wa pili juu ya kanisa, Wakristo wanapaswa kuhudhuria ushirika wa ndani ambao hutangaza uongozi wa Kristo katika mambo yote ya mafundisho na matendo. Hakuna mtu, kama mchungaji, kuhani, au papa, ndiye kiongozi wa kanisa. Wanadamu wote wanakufa. Kanisa lililo hai la Mungu aliye hai linawezaje kuongozwa na aliyekufa? Haiwezi. Kristo ni mamlaka kuu ya kanisa, na uongozi wote wa kanisa, karamu, utaratibu, nidhamu, na ibada huteuliwa kwa njia ya uhuru wake, kama inavyoonekana katika Maandiko.

Mara misingi hizi za ukweli zinapowekwa, mambo mengine (majengo, miundo ya ibada, shughuli, mipango, eneo, nk) ni suala la upendeleo wa kibinafsi. Kabla ya kuhudhuria kanisa, utafiti fulani ni muhimu. Taarifa za kidini, kauli za kusudi, kauli za utume, au chochote kinachoweza kutoa ufahamu juu ya kile ambacho kanisa linaamini kinapaswa kuchunguzwa kwa makini. Makanisa mengi yana tovuti ambazo mtu anaweza kuchunguza wanachoamini kuhusu Biblia, Mungu, Utatu, Yesu Kristo, dhambi, na wokovu.

Baada ya hayo, inapaswa kutembelea makanisa ambayo yanaonekana kuwa na msingi mwema. Kuhudhuria huduma mbili au tatu katika kila kanisa kutasaidia. Machapisho yoyote wanayo kwa ajili ya wageni inapaswa kuchunguzwa, wakichunguza kwa makini mafundisho ya imani. Tathmini ya Kanisa inapaswa kutegemea kanuni zilizotajwa hapo juu. Je! Biblia inahusika kama mamlaka pekee? Je! Kristo ameinuliwa kama kiongozi wa kanisa? Kanisa linazingatia ufuasi? Je, uliongozwa kumwabudu Mungu? Ni aina gani za huduma ambazo kanisa linajihusisha? Ilikuwa ujumbe wa kibiblia na wa kiinjili? Ushirika ulikuwaje? Pia unahitaji kujisikia vizuri. Je! Umefanywa kujisikia kuwa umekaribishwa? Je, kusanyiko linajumuisha waabudu wa kweli?

Hatimaye, kumbuka kuwa hakuna kanisa lililo kamili. Kwa bora, bado ni linajazwa na wenye dhambi waliookolewa ambao mwili na roho imo vitani. Pia, usisahau umuhimu wa sala. Kuomba juu ya kanisa ambayo Mungu angetaka ushiriki ni muhimu katika mchakato wa kufanya maamuzi.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Nitazingatia nini ninapotafuta kanisa?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries