settings icon
share icon
Swali

Biblia inasema nini juu ya kamari? Je, kamari ni dhambi?

Jibu


Kamari ni “pesa zinazohatarishwa katika jaribio la kuzizidisha kwa njia isiyo ya kawaida.” Bibilia haipingi moja kwa moja kamari,bahati nasibu na kadhalika. Biblia hutuonya tujiepushe na tamaa ya pesa. (Timotheo wa kwanza 6:10; waebrania 13;5). Maandiko pia husisitiza tuepukane na nia ya kutaka kujitajirisha haraka haraka (Methali 13:11; 23:5; Mhubiri 5:10). Kamari imekithiri katika msingi wa tamaa ya pesa na hutia watu katika majaribu ya kutaka kuwa tajiri upesi.

Kamari ina ubaya gani? Inapofanywa mara kwa mara ina asili ya matumizi mabaya ya pesa si lazima yenyewe iwe ni dhambi. Ijapokuwa kuna mambo mengi ambayo yanaweza kuleta matumizi mabaya ya pesa kama kununua chakula cha ghali bila sababu ya maana au kununua vitu visivyofaa lakini isiwe sababu ya kuhalalisha kamari. Pesa zisifujwe. Pesa ni zihifadhiwe kwa matumizi mazuri ya baadaye lakini sio kamari.

Kamari katika Biblia: ijapokuwa biblia haitaji moja kwa moja michezo ya kamari, huzungumzia michezo Fulani ya bahati nasibu kama kupiga kura katika Mambo ya Walawi kuchagua baina ya mbuzi wa sadaka na mbuzi wa lawama. Yoshua alipigia kura ugawaji wa ardhi kwa makabila mbali mbali. Nehemia alipiga kura kutambua nani atakayeishi ndani ya nyua za Yerusalemu na nani asiishi ndani yake. Mitume walipiga kura kuchagua atakaye chukua nafasi ya Yuda. Methali 16:33 inasema, “ kura hupigwa mapajani lakini uamuzi hutoka kwa Bwana.” Hakun mahali katika Biblia kubahatisha kumetumika kwa starehe ama kuendelezwa kama jambo halali la wafuasi wa Mungu.

Kasino na bahati nasibu: Kasino hutumia mbinu nyingi kuhamasisha wacheza kamari kuendelea kupoteza pesa nyingi zaidi. wakati mwingine hutoa vileo kwa bei nafuu au hata bure kinachorahisisha kulewa ili mtu asiweze kufanya uamuzi tena wa busara kwa kuwa amelewa sana. Kila kitu ndani ya kasino kimeundwa kuchukua pesa za watu kwa wingi bila kurudishia chochote mwenye kutoa pesa hizo. Michezo ya bahati nasibu husingiziwa kuwa ni ya kusaidia kuchangia elimu au huduma za kijamii. Lakini wenye kucheza michezo hii ni wale wenye pesa za kununulia kadi hizi za bahati nasibu. Tamaa ya kutajirika haraka huwashika wenye kushiriki hivyo basi wanapokosa kufanikiwa huwabakisha katika hali mbaya zaidi ya ile ya awali. Hapa ndipo maisha ya wengi husambaratika.

Kwa nini mapokeo kutoka kwa bahati nasibu hayamridhishi Mungu: wengi husema wanacheza michezo hiyo ili watoe pesa hizo kwa kanisa au kufanyia jambo Fulani zuri. Hili ni jambo zuri. Lakini uchunguzi umedhihirisha mara nyingi si kwa ajili ya mambo haya. Mungu hahitaji pesa zetu kuendeleza kazi zake duniani. Methali 13:11 inasema, “ pesa mbaya hutoroka zenyewe, lakini yule akusanyaye pesa chache chache huzifanya kukua na kuwa nyingi.” Mungu ni muweza na atagharimia mahitaji ya kanisa kwa njia za halali. Je, Mungu angeheshimiwa kwa kupokea mchango wa pesa zilitokana na biashara ya madawa ya kulevya au zilizoibwa benki? Hata hivyo Mungu hahitaji pesa zilizoibwa kwa maskini katika jaribio la kutaka kuwa matajiri haraka.

Timotheo wa kwanza 6:10 inatuambia, “maana shina moja la mabaya ya kila namna ni kupenda fedha; ambayo wengine hali wakiitamani hiyo wamefarakana na imani, na kujichoma kwa maumivu mengi.” Waebrania 13:5 inasema, “ msiwe na tabia ya kupenda fedha mwe radhi na vitu mlivyo navyo;kwa kuwa yeye mwenyewe amesema, sitakupungukia kabisa, wala sitakuacha kabisa.” Mathayo 6:24 inasema, “ hakuna awezaye kuwatumikia mabwana wawili. Kwa maana atamchukia huyu na kumpenda huyu; ama atashikamana na huyu na kumdharau huyu.hmwezi kumtumikia Mungu na mali.”

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Biblia inasema nini juu ya kamari? Je, kamari ni dhambi?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries