settings icon
share icon
Swali

Kaini alikuwa anamhofia nani baada ya kumwua Abeli?

Jibu


Katika Mwanzo 4: 13-14, muda mfupi baada ya kumwua ndugu yake Abeli, "Kaini akamwambia Bwana, Adhabu yangu imenikulia kubwa, haichukuliki. Tazama, umenifukuza leo katika uso wa ardhi, nitasitirika mbali na uso wako, nami nitakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani; hata itakuwa kila anionaye ataniua.' "Ni nini hasa Kaini alikuwa anamhofia? Watu pekee ambao kitabu cha Mwanzo kilichotajwa hapa ni Adamu na Hawa (wazazi wa Kaini) na Abeli (ambaye alikua amekufa sasa). Nani angeweza kuwa tishio kwa Kaini?

Ni muhimu kutambua kwamba Kaini na Abeli walikuwa watu wazima wakati Kaini alimuua Abeli. Wote wawili Kaini na Abeli walikuwa wakulima ambao walikuwa waliotunza ardhi yao na kundi la mifugo yao (Mwanzo 4: 2-4). Biblia haituambii umri wa Kaini na Abeli, lakini kuna uwezekano mkubwa kuwa wangekuwa katika miaka yao ya 30 au 40. Biblia haitaji kwa uwazi Adamu na Hawa kuwa na watoto kati ya Abeli na Seti (Mwanzo 4:25). Hata hivyo, haiwezekani kwamba watu wawili kamilifu katika historia ya dunia, Adamu na Hawa, hawakuwa na watoto zaidi ya miongo kadhaa. Adamu na Hawa walikuwa na watoto wengi baada ya Seti (Mwanzo 5: 4), kwa nini hawakuwa na watoto wengine kati ya Abeli na Seti? Biblia haisemi kwamba Seti alikuwa mtoto wa kwanza wa Adamu na Hawa, au hata mwana wa kwanza, baada ya Abeli kuuawa. Badala yake, inasema kwamba Seti alizaliwa kama "mbadala" kwa Abeli. Mwanzo sura ya 5 huelezea ukoo wa Seth. Kabla ya kifo chake, Abeli alikuwa mwana "aliyechaguliwa" ambaye hatimaye atakuza Masihi (Mwanzo 3:15). Kwa maana hii Seti "amechukua nafasi" ya Abeli.

Kwa hiyo, Kaini alikuwa anamhofia nani? Kaini alikuwa na hofu ya kaka zake, dada, wapwa wake ambao walikuwa wamekwisha zaliwa na walikuwa na uwezo wa kulipiza kisasi. Ukweli kwamba Kaini alikuwa na mke (Mwanzo 4:17) ni ushahidi zaidi kwamba Adamu na Hawa walikuwa na watoto wengine baada ya Kaini na Abeli, lakini kabla ya Seti.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kaini alikuwa anamhofia nani baada ya kumwua Abeli?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries