settings icon
share icon
Swali

Je, Mkristo anapaswa kutumia kadi ya mkopo?

Jibu


Vocha za mikopo katika fomu fulani zimewahi kuwepo tangu miaka ya 1800, lakini katika uwezo binafsi, uwezo mdogo. Kadi za mkopo za plastiki kama tunavyozijua zimetumika tu tangu miaka ya 1960. Mnamo 1946, mwenye benki mmoja aitwaye John Biggins alivumbua kadi ya benki inayoitwa "Charg-It," lakini ilitumiwa tu ndani ya benki yake mahali pale. Mnamo 1950 Klabu ya Diners ilianzisha kadi ambayo ilikuwa kadi ya mkopo ya kwanza na yenye matumizi pana. Kuanzia wakati huo, mabenki mengine na taasisi za mikopo zilijiunga na umati ya wale wanaotaka kukopesha pesa na riba. Kadi za mkopo zinaweza kumsaidia mtu kupata wakati wa matatizo ya kifedha, lakini pia zinaweza kuunda madeni yasiyothibitika ikiwa hazitumiki kwa makini. Kwa kuwa, kwa Mkristo, Mungu anapaswa kuwa na udhibiti wa kila eneo la maisha, ikiwa ni pamoja na fedha, je, Mkristo anapaswa kumiliki kadi ya mkopo?

Kama au la Mkristo anapaswa kumiliki na kutumia kadi za mkopo hutegemea uthibiti wa binafsi wa mtu, hekima, na ufahamu wa nguvu kwamba kadi za mkopo zinapaswa kutumiliki sisi. Tatizo moja kubwa na taasisi za mikopo na makampuni ya kadi ya mkopo ni kwamba wanafanya utajiri wao mkubwa kutoka kwa watu wenye matumizi yasio na hekima na wale walio maskini sana kulipa madeni yao. Wakati Mungu alitoa sheria Yake kwa Waisraeli, alieleza kwamba hawapaswi kukopesha pesa na riba kwa watu wenzao (Mambo ya Walawi 25:36; Kutoka 22:25). Kikwazo hakikuwa dhidi ya kudai riba yoyote kabisa kwa mtu yeyote ambaye wanaweza kukopesha fedha, lakini badala yake kudai riba kubwa mno kwa Waisraeli wenzao ambao hawangeweza kulipa. Tofauti na, Zaburi 15:5 inaelezea mtu anayekaa mbele ya Mungu kama mtu ambaye, kati ya mambo mengine, "kukopesha maskini fedha bila riba."

Watu wengi wamegundua kwamba hawawezi kujiamini wenyewe na kadi za mkopo. Wao huziona kama "fedha za bure" kwa kuwa gharama halisi haikuji kwa wiki, na hata wakati huo malipo ya chini yanahitajika. Wanaweza kuwa na mashua ya $ 2,000 leo na kuilipia tu dola mia chache kwa muda kwa miezi kadhaa. Kile hawataki kufikiria ni kwamba mashua mpya ya $ 2,000 inakuwa mashua ya $ 4,000 iliyotumika kwa wakati ambapo hatimaye wao wameilipia, kwa malipo ya chini kila mwezi. Kufuja fedha kwa riba sio usimamizi mzuri wa rasilimali ambazo Mungu ametukabidhi sisi (tazama 1 Timotheo 6:10; Mithali 22:7). Matumizi ya hekima inamaanisha tunajitahidi kuishi chini ya uwezo wetu ili kila wakati tuwe na pesa za dharura na za kutosha kushirikiana na wale wanaohitaji.

Kupata riba kwa uwekezaji wetu, badala ya kulipa riba kwa matumizi yetu, ni njia ya hekima ya kushughulikia fedha. Katika Mathayo 25, Yesu anatoa mfano wa watumishi watatu, wawili kati yao waliwekeza kile alichokabidhiwa na bwana na kuifanya mara mbili ya awali. Mtumishi wa tatu, hata hivyo, hakuwekeza. Katika mstari wa 27, bwana anamwambia, "Sawa basi, ilikupasa kuiweka fedha yangu kwa watoao riba; name nikija nimgalipata iliyo yangu na faida yake."

Kadi za mkopo sio mbaya katika zenyewe. Zinaweza kuwa za manufaa, kufaa, na hata ya kupunguza gharama kwa mtu ambaye anajua jinsi ya kuitumia kwa busara. Wakati tunawajibikia fedha zetu, badala ya fedha zetu kutuajibikia sisi, hatufanyi sanamu nje ya vitu tunaweza kununua. Wala hatutumii fedha zetu kudhibiti watu wengine. Watumiaji wa busara wa kadi ya mkopo wanaepuka riba kubwa mno iliyowekwa kwenye manunuzi yao kwa kulipa masalio kamili kwenye kadi mwishoni mwa kila mzunguko wa bili.

Tunapoangalia kadi za mkopo kama fedha, tunaendelea katika udhibiti wa matumizi yetu. Hatudai kile ambacho hatuwezi kumudu na kwa hivyo usimalizie na mshtuko wa kuduwaza wakati gharama inapokuja. Kudai tu kile tunachoweza kulipa hutusaidia kutii Waebrania 13:5, "Msiwe na tabia ya kupenda fedha; mwe radhi na vitu mlivyo navyo. ..." Wakati tunakataa mvuto wa matumizi kwa mkopo, tunajifunza kufanya kuridhika (1 Timotheo 6:6). Kupitia kuridhika, tunaendeleza tabia ya kimungu na kuona fedha zetu kama njia ya kubariki wengine na kumheshimu Mungu (Zaburi 37:26, Mithali 11:24-25; 2 Wakorintho 9:7).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, Mkristo anapaswa kutumia kadi ya mkopo?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries