settings icon
share icon
Swali

Je, ninawezaje kumjua Mungu bora?

Jibu


Kila mtu anajua kwamba Mungu yupo. "Maana Mungu mwenyewe ameyadhihirisha" kwamba Yeye ni halisi, " Tangu Mungu alipoumba ulimwengu, uwezo wake wa milele na uungu wake, ingawa havionekani kwa macho, vinafahamika wazi. Watu wanaweza kuyajua Mambo hayo kutokana na vitu hivyo alivyoumba Mungu. Kwa hivyo hawana njia yoyote ya kujitetea" (Warumi 1:19-20). Watu wengine hujaribu kukandamiza maarifa kuhusu Mungu; wengine hujaribu kuongezea. Mkristo ana hamu kubwa ya kumjua Mungu bora (Zaburi 25:4)

Katika Yohana 3 tunasoma kuhusu mtu ambaye alitaka kumjua Mungu bora na alisoma zaidi kuliko wengine kuhusu mambo ya Mungu. Jina lale lilikua Nikodemo na alikuwa Mfarisayo, mtawala wa Wayahudi. Nikodemo huyu alijua kwamba Yesu alikuwa ametoka kwa Mungu na alikuwa na hamu ya kujua mengi kuhusu Yesu. Yesu alielezea Nikodemo kwa uvimilivu jinsi anapaswa kuzaliwa mara ya pili (Yohana 3:3-15). Ili kumjua Mungu bora, Nikodemo alikuwa amekuja kwa mtu sahihi-"Maana, ukamilifu wote wa kimungu umo ndani ya Kristo" (Wakolosai 2:9). Kwa kweli Yesu ni Mwana wa Mungu aliyefanyika mwili (Yohana 1:14). Yesu alidhihirisha Mungu kupitia maneno na kazi zake. Hata alisema kwamba hakuna anayekuja kwa Baba ila tu kupitia kwake Yesu (Yohana 14:6). Ikiwa unataka kujua Mungu ni nani, basi mtazame Yesu.

Kwa hivyo lazima tuanze na Imani. Hatua ya kwanza ya kunjua Mungu bora ni kumjua Yesu Kristo, aliyetumwa kutoka kwa Mungu ( Yohana 6:38). Mara tu tunapozaliwa mara ya pili kwa nguvu ya Roho Mtakatifu, kwa kweli tunaweza kuanza kujua mengi kuhusu Mungu, tabia yake na mapenzi yake. "Roho huchunguza kila kitu, hata mabo ya ndani ya Mungu" ( 1Wakorintho 2:10). Kwa upande mwingine, "mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Roho wa Mungu, wala hawezi kuyafahamu kwa kuwa yanatambuliwa kwa msaada wa Roho" ( 1 Wakorintho 2:14). Kuna tofauti kati ya mtu wa "asili" na mtu wa "kiroho".

Warumi 10:17 inasema, "Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo." Haiwezi kusisitizwa vya kutosha jinsi kusoma neno la Mungu, Biblia, ni muhimu kwa kumjua Mungu bora. Lazima, "kama watoto wachanga, kuyatamani maziwa halisi ya kiroho, ili kwa nguvu yake mpate kukua na kukombolewa, kwa kuwa mmegundua ya kwamba Bwana ni mwema" (1 Petro2:2-3). Neno la Mungu linapaswa kuwa "furaha" kwetu (Zaburi 119:16,24).

Wale ambao wanajifunza zaidi juu ya Mungu ni wale pia hutii amri ya kujazwa na Roho Mtakatifu. Waumini walio zaliwa kwa mara ya pili huwa na Roho Mtakatifu, lakini Waefeso 5:5-21 inatufundisha kutembea katika roho na kujisalimisha kwa mapenzi yake.

Maombi pia ni muhimu katika kumjua Mungu bora. Tunapoomba tunamsifu Mungu kwa silika yake na kwa yale ametenda. Tunatumia wakati naye na kutegemea nguvu zake na kumruhusu Roho kutuombea "kwa kuugua kusikowezwa kutamkwa" (Warumi 8:26).

Fikiria pia kwamba mtu anaweza kumjua Mumgu bora kwa kushirikiana na waumini wengine. Kusudi la maisha ya Kikristo sio kuishi peke yako. Tunajifunza zaidi juu ya Mungu kupitia mahubiri ya Neno la Mungu na ushauri wa kimungu wa wale wanaotembea pamoja naye. Nufaika na maarifa kanisani, shughulika, fanya mafunzo ya Biblia katika vikundi vidogo, nenda kushuhudia na waumini wenzako. Kama vile gogo linalochomeka hupoa linapotolewa na kuwekwa kando, vile vile tunapoteza bidii yetu kwa Mungu ikiwa hatutashirikiana na waumini wengine. Unapoweka gogo hilo kwa moto tena pamoja na magogo menginge litawaka moto tena.

Kwa muhtasari tu kuhusu kumjua Mungu bora: 1) Mpokee Kristo kama Mwokozi wako. 2) Soma Neno lakeā€¦ni hai (Waebrania 4:12). 3) Kila wakati, jazwa na Roho Mtakatifu. 4) Mtafute Mwana kupitia maombi. 5) Shiriki na kuishi maisha yako na watakatifu (Waebrania 10:25).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, ninawezaje kumjua Mungu bora?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries