settings icon
share icon
Swali

Je! Biblia inasema nini kuhusu jinsia tatanishi?

Jibu


Hali ya kuwa na jinsia tatanishi, au kuwa na hisia kwamba jinsia yako kibiolojia / maumbile / kisaikolojia haiambatani na jinsia ambayo wewe mwenyewe unajihisi kuwa nayo . Walio na jinsia tatanishi mara nyingi wanajielezea kama walio fungwa katika mwili ambao haulingani na jinsia yao ya kweli. Wao hutafuta matibabu ya homoni na / au upasuaji ili kuambatanisha Miili yao kulingana na jinsia wanayopendelea.

Bibilia haizungumzii kwa uwazi kuhusu hali ya kuhisi kuwa na jinsia tofauti au kuelezea mtu yeyote kuwa na hisia za jinsia tofauti. Hata hivyo, Biblia ina mengi ya kusema juu ya jinsia ya kibinadamu. Ya msingi ya ufahamu wetu wa kijinsia ni kwamba Mungu aliumba jinsia mbili (na mbili tu) "Mwanamume na mwanamke aliwaumba" (Mwanzo 1:27). Dhana zote za kisasa kuhusu jinsia nyingi au mabadiliko ya kijinsia ni kinyume na Biblia..

Biblia hutaja suala la hisia za jinsia tofauti kwa umbali katika laana yake ya ushoga (Warumi 1: 18-32; 1 Wakorintho 6: 9-10) na mavazi ya jinsia tofauti (Kumbukumbu 22: 5). Neno la Kigiriki linalotafsiriwa "wahalifu mashoga" au "wanaume makahaba" katika 1 Wakorintho 6: 9 linamaanisha "wanaume ambao wana mienendo ya kike." Kwa hiyo, wakati Biblia haizungumzii hisia za jinsia tofauti moja kwa moja, wakati Inaelezea matukio mengine ya kijinsia "machafuko," ni wazi kuwa ni dhambi.

Je, kuna uwezekano kwamba wale wanaosumbuliwa na hisia za jinsia tofauti wana akili inayofanya kazi kama jinsia moja huku miili yao kwa kibiolojia ni ya jinsia nyingine? Biblia kamwe haijataja uwezekano huo. Hata hivyo, Biblia haijataja hali ambayo mtu ana viungo vya uzazi vya kiume na vya kike ambayo hutokea (ingawa mara chache sana). Zaidi ya hayo, watu wanaweza kuzaliwa na kukua na kila ila aina ya kasoro mbalimbali ya ubongo au ubongo kutofanya kazi. Je, inawezekanaje kwa ubongo kike kuwa katika mwili wa kiume (au kinyume chake)?

Kama ilivyo katika hali ya jinsia mbili, hatuwezi kusema kuwa ikiwa Biblia haijataja kitu kwamba hakitatokea. Kwa hiyo, inawezekana kwa mtu kuzaliwa na ubongo ambao kwa namna fulani ambayo inachangia hisia za kuwa na jinsia. Hii inaweza pia kuwa maelezo ya baadhi ya matukio ya ushoga. Hata hivyo, kwa sababu tu kitu inaweza kuwa na sababu za kibaiolojia haina maana kukumbatia madhara ni jambo sahihi kufanya. Watu wengine wamehusisha akili zao katika hisia za juu za kimapenzi. Hiyo haifai kuwa haki kwao kushiriki katika usherati. Imedhibitiswa kisayansi kuwa wengine wana ubongo dhaifu na hukosa kudhibiti hisia zao. Hiyo haifai kuwa haki kwao kushiriki katika tabia yoyote isiyofaa ambayo huja katika akili zao.

Haijalishi kama kama kuvuruga jinsia imesababishwa na maumbile, homoni, kisaikolojia, au kiroho, inaweza kuponywa kwa njia ya imani katika Kristo na kuendelea kutegemea nguvu za Roho Mtakatifu. Yeyote anaweza kupokea uponyaji, na kushinda dhambi, na maisha inaweza kubadilishwa kwa njia ya Wokovu ambayo Yesu Hutoa, hata kama kuna vikwazo vya kibiolojia / kisaikolojia . Waumini wa Korintho ni mfano wa mabadiliko hayo: "Na baadhi yenu mlikuwa watu wa namna hii; lakini mlioshwa, lakini mlitakaswa, lakini mlihesabiwa haki katika jina la Bwana Yesu Kristo, na katika Roho wa Mungu wetu."(1 Wakorintho 6:11). Kuna matumaini kwa kila mtu, walio na jinsia tatanishi, wale wenye matatizo ya utambulisho wa kijinsia, wanaume wanaopendelea kuvaa mavazi ya kike, kwa sababu ya msamaha wa Mungu unaopatikana katika Yesu Kristo.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Biblia inasema nini kuhusu jinsia tatanishi?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries