settings icon
share icon
Swali

Je, kutakuwa na kitu kama jinsia mbinguni?

Jibu


Mathayo 22:30 inazungumzia watu baada ya ufufuo ambao hawatahusika katika ndoa — huwa "kama malaika." Hata hivyo, hii haimaanishi ni watu wasio na jinsia.Mara nyingi malaika wameelezewa kuwa na jinsia ya kiume (na yeye alikuwa kama ... kuonekana kwake ilikuwa kama, nk). Kwa hiyo hakuna dalili halisi kwamba malaika ni viumbe wasio na jinsia.

Hakuna kitu katika Biblia kinachoonyesha kuwa watu watapoteza au kubadilisha jinsia yao mbinguni. Katika kitabu cha Ufunuo (sura ya 21-22), inaonekana kwamba Mungu anafanya mambo si kama ilivyokuwa katika bustani ya Edeni, lakini hata zaidi. Kumbuka kwamba jinsia sio mbaya — kwa kweli ni jambo jema. Mungu aliumba Hawa kwa sababu Adamu alihitaji mtu wa kumsaidia. Ndoa (haiwezekani bila jinsia tofauti), uhusiano wa mfano kati ya mwanaume na mwanamke, ni picha ya Kristo na kanisa. Kanisa ni Bibi arusi na Kristo ni Bwana arusi (Waefeso 5: 25-32)..

Ingawa haifundishwi waziwazi katika Biblia, inaonekana uwezekano mkubwa wa kuwa watu wanahifadhi jinsia yao baada ya kifo. Jinsia yetu ni sehemu yetu. Jinsia ni zaidi ya kimwili-ni sehemu ya asili yetu na sehemu ya njinsi tunavyohusiana na Mungu. Kwa hiyo, inaonekana kwamba jinsia itakuwa kamilifu na kutukuzwa kwa milele. Pia ni muhimu sana kwamba Yesu alishikilia jinsia yake baada ya kifo na ufufuo wake.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, kutakuwa na kitu kama jinsia mbinguni?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries