settings icon
share icon
Swali

Je, kuna Mungu? Je, kuna ushahidi wa kuthibitisha kuweko kwa Mungu?

Jibu


Je, kuna Mungu? Ninaona ni jambo la kusisimua ya kwamba umakini mwingi umepawa mjadala huu. Katika takwimu zetu hivi sasa zasema ya kuwa zaidi ya asilimia 90 ya watu duniani wanaamimi kuweko kwa Mungu au Mamlaka ya kiwango cha juu. Jukumu linabaki kwa wenye kuamini kuthibitisha ukweli wa kuweko kwake. Mimi nafikiri ingewapasa wale hawaamini watuthibitishie.

Kuweko kwa Mungu hakuwezi kutothibitishwa wala kuthibitishwa. Bibilia inasema inatupasa kukubali kwa imani kuwa Mungu yuko, “Na pasipo imani haiwezekani mtu kumpendeza Mungu, kwa kuwa kila ajaye kwake sharti aamini kuwa yuko na ya kuwa huwapa vitu wale wamtafutao kwa bidii” (Waebrania 11:6). Kama Mungu alingetaka iwe, angejitokeza tu mbele ya ulimwengu wote kuwajulisha wote kuwa yeye yuko. Lakini, angefanya hivyo hakungekuwa na haja ya imani. “Tena Yesu kamwambia, ‘kwa kuwa umeniona, umeamini; heri wale ambao hawakuniona na wameamini” (Yohana 20:29).

Hiyo haimaanishi ya kuwa hakuna idhibati ya kuweko kwa Mungu. Biblia inasema, “Mbingu zatangaza utukufu wa Mungu; anga zatangaza kazi za mikono yake. Siku baada ya siku zamimina hotuba zake; usiku baada ya usiku zaonyesha ufahamu. Hakuna hotuba au lugha ambayo haisikiki. Sauti zao hutapakaa duniani kote, maneno yao mpaka mwisho wa dunia” (Zaburi 19:1-4). Ukitazama nyota, ukijaribu kufahamu kina cha anga, na kutazama maajabu ya kiasili, huku ukiona urembo wa kutua kwa jua - haya yote yanaashiria kuweko kwa Mungu muumbaji. Kuna ushahidi wakuweko kwa Mungu ndani ya mioyo yetu. Mhubiri 3:11 inatuambia, “….ameweka pia umilele ndani ya mioyo ya wanadamu…” Kuna kitu ndani yetu kinachotujulisha ya kuwa kuna kitu zaidi baada ya maisha haya tunayoishi na mwingine zaidi yetu nje ya dunia hii. Hata tukipuuza bado kuna uwepo wa Mungu maishani mwetu. Biblia inatuonya ya kuwa kuna wengine watakuwapo watakaokataa kuwepo kwa Mungu, “Mjinga amesema moyoni mwake hakuna Mungu” (Zaburi 14:1). Kwa kuwa zaidi ya asilimia 98 ya watu wa tamaduni mbali mbali katika vizazi vilivyopita ndani ya mabara yote duniani ni waumini wa kuwepo kwa Mungu wa aina Fulani – lazima kuwe kuna mtu ama kitu Fulani kinachohisi na kusababisha imani hii.

Kuongezea, kuna maoni mbali mbali ambayo hutumika kuthibitishia pia. Maoni ya kwanza yasema kwa kuwa Mungu ni kile ambacho zaidi yake hakuna. Basi uwezekano wa kuwepo kwake ni mwingi. Na kama Mungu hayuko basi hakungekuwa na ambacho zaidi yake hakuna. Maoni ya pili ni kwamba kwa kuwa ulimwengu unaonyesha kazi nzuri ya ustadi iliyofanyika basi lazima kuweko na aliyeifanya. Kila kitu kina fanya kazi vyema kwa wakati wake na kwa kipimo mwafaka. Kama hewa yetu ingeharibika tu kidogo viumbe vyote vingekufa.

Maoni ya tatu ni kwamba kwa chochote kufanyika lazima kuweko na mwenye au chenye kusababisha. Kwa vile ulimwengu upo lazima kuwe na aliyeusababisha uweko na huyo ndiye Mungu. Maoni ya nne ni kwamba katika kila utamaduni, mila na desturi za watu duniani kuna aina Fulani ya mfumo wa sheria ya kuelekeza; yenye kutambua mema na mabaya. Kuua, uongo, wizi na uchafu wa kitabia ni mambo yanayokataliwa ulimwenguni kote. Hali hii ya kutambua meme na mabaya ilitoka wapi Kama si kwa Mungu Mtakatifu?

Biblia inatuambia, watu watakataa ukweli wa kuweko kwa Mungu na kuamini roho za uongo. Warumi 1:25 inasema, “walibadilisha ukweli wa Mungu na kutumikia uongo hata kuiabudu na kuitumikia miungu waliyoiumba kwa mikono yao kinyume na Mungu aliyewaumba –ambaye daima husifiwa. Amina.” Biblia pia inasema, watu hawana sababu ya kutomwamini Mungu, “Kwa kuwa tangu kuumbwa kwa ulimwengu siri za uwepo wake – Nguvu zake za milele na utisho wake umethibitika na kufahamika kutokana na yale aliyoyatenda kwa hivyo wanadamu hawana kisingizio” (Warumi 1:20).

Watu husema hawamwamini mungu kwa sababu si kisayansi ama hakuna kithibitisho cha kuweko kwake. Sababu halisi ni kwamba kwa kukubali yuko,mtu anahitajika kuwajibika mbele zake na kuomba msamaha (Warumi 3:23; 6:23). Kama Mungu yuko basi tunawajibika kwa matendo yetu. Kama hayuko, basi tunaweza kufanya mapenzi yetu wenyewe bila kujali hukumu. Huenda ikawa hii ndiyo sababu ya watu wengine kushikilia mawazo ya kuwa dunia ilifanyika tu kwa njia ya vitu tofauti tofauti kubadilika umbo polepole kupitia mabadiliko ya kimazingira ili waepukane na ukweli wa kuna Mungu muumbaji wa yote. Mungu yuko na kila mmoja anajua hivyo. Mwenye kubishana ni mbishani tu lakini huwa hata yeye anajua yuko.

Je, nitajuaje kuwa Mungu yuko? Najua Mungu yuko kwa kuwa nazungumza naye kila siku. Simsikii masikioni akinijibu lakini ninahisi uwepo wake, nahisi kuongoza kwake, najua upendo wake ninatamani neema yake.Mambo yaliyotendeka maishani mwangu hayana maelezo mengine ila Mungu. Mungu ameniokoa kimiujiza na kuyabadilisha maisha yangu mpaka sasa nimebaki tu kumtukuza. Maelezo haya yote hayawezi kumfanya mtu anayetaka kukataa kuwepo kwa Mungu akubali. Muhimu ni kumkubali kwa imani (Waebrania 11:6). Imani kwa Mungu si bure kama kubahatisha gizani bali ni sawa na kutembea salama ndani ya chumba chenye nuru ambamo asilimia 90 ya watu waliomo wamesimama.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, kuna Mungu? Je, kuna ushahidi wa kuthibitisha kuweko kwa Mungu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries