settings icon
share icon
Swali

Je, Yesu aliumbwa?

Jibu


Biblia inatufunza kwamba Yesu hakuumbwa bali ndiye alikuwa Muumbaji. "Katika [Yesu Kristo] vitu vyote viliumbwa…kwa kuwa katika Yeye kila kitu kiliumbwa" (Wakolosai 1:16). Fundisho la umilele wa Kristo ni mojawapo wa alama zinazotofautisha za Ukristo wa Biblia.

Yesu anaheshimiwa sana na Waislamu, ilhali Wamomoni, Mashahidi wa Yehova na wengineo wa imani mbalimbali za theologia hufundisha kwamba Yesu alikuwa kiumbe. Uthibitisho wa dini asili wa Uungu wa Kristo na asili yake isiyo ya kuumbwa hufanya Ukristo kuwa tofauti na dini na falsafa zingine. Dini mbalimbali za ulimwengu zinaweza kukubaliana kuhusu maswala kadhaa muhimu kama vile kuwepo kwa maadili ambayo ni bora,na thamani ya maisha familia imara, lakini jibu la swali "Yesu Kristo ni nani?" hutenganisha kwa haraka wale ambao hufuata Ukristo wa Biblia na wale wasiofuata.

Bila shaka imani za kwanza za kanisa zinafundisha kwamba Yesu hakuumbwa lakini Yeye ni wa Mtu wa umilele, Mwana wa Mungu. Waislamu wanafunza kwamba Yesu alikuwa nabii binadamu aliyezaliwa na bikra lakini alikuwako kama mtu mwingine yeyote. Wamomoni ambao hufuata mafundisho ya uzushi huamini kwamba Yesu alikuwa na mwanzo kama vile Mungu Baba alikuwa na mwanzo. Mashahidi wa Yehova husema kwamba Yesu alikuwa kiumbe wa kwanza wa Yehova na hapo awali alijulikana kama mikaeli malaika mkuu. Kwa hivyo, Yesu yuko katika upande gani wa muumbaji/Kiumbe? Je, Yesu ni kiumbe, na vilevile yuko katika utaratibu wa uumbaji? Ama Yeye yuko pamoja na Baba na Roho Mtakatifu, Muumbaji wa vyote vilivyoumbwa? Je, Yesu ni wa asili tofauti na Baba kama vile Arius wa Karne ya nne alivyodai; ama Yesu na Baba ni wa asili moja kama vile Athanasius alivyoshikilia na kama vile Baraza la Nicea lilivyoamuru?

Hamna mtu bora kutazama bali Yesu mwenyewe tunapojaribu kujibu swali "Je, Yesu aliumbwa?" Yesu alichukua sifa za kiungu katika huduma yake hadharani. Yeye alionyesha haki ambazo hazingefaa kiumbe aliyeumbwa. Yeye alisema kwamba alikuwa "Bwana wa Sabato" (Marko 2:28), na kwa kuwa Sabato ilianzishwa na Mungu, madai yake Yesu kuwa Yeye ndiye "Bwana" wa Sabato yalikuwa madai ya kudhibitisha uungu. Yesu aliongea kuhusu ufahamu wake wa kipekee wa Baba (Mathayo 11:27) pamoja na utukufu alioshiriki na Baba "kabla ya ulimwengu kuwako" (Yohana 17:5). Yesu alikubali kuabudiwa na wengine (Mathayo 14:32-33) na akaelezea jinsi atakapohukumu mataifa yote. Luka anatuambia Yesu alisamehe dhambi za mwanamke -Jambo ambalo Mungu tu anaweza kutenda- na kusema kuwa msamaha huo ulikuwa kwa sababu ya imani mwanamke huyo kwake.

Wanafunzi wa Yesu vilevile walikuwa wazi katika imani yao katika uungu wa Yesu na hali yake isiyo ya kuumbwa. Yohana anatuambia kwamba "hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu" (Yohana 1:1). Baada ya kukutana na Yesu aliyefufuka, mtume Tomaso alimwuliza, "Bwana wangu na Mungu wangu!" (Yohana 20:28). Mtume Paulo alimtaja Kristo kama "Mungu aliye juu ya yote" (Warumi 9:5) na kusema kwamba "ndani yake Kristo katika ubinadamu wake umo ukamilifu wote wa Mungu" (Wakolosai 2:9). Katika siku za kwanza za kanisa, Yesu maombi ilielekezwa kwake Yesu (Matendo ya Mitume 7:59) na katika jina lake msamaha wa dhambi ulitangazwa (Matendo ya Mitume 2:38; 10:43). Baada ya kuwahoji wakristo chini ya tishio la kifo, Pliny Mdogo ambaye alikuwa mtawala wa Kirumi, katika barua yake kwake mfalme Trajan (takribani AD 110) kwamba "[Wakristo]" walikuwa na mazoea ya kukusanyika katika siku walizotenga kabla kupambazuke wakiimba tenzi kwa Kristo kama, sawia na miungu" (barua 10.96).

Yesu ambaye ni, Mungu Mwana, hakuumbwa. Amekuwepo tangu; hana mwanzo wala mwisho. Mwana alitwaa mwili wa nyama wakati fulani katika historia ya mwanadamu (Yohana 1:14). Wakristo hurejelea tukio hili kama Utwalizi ("tendo la kufanyika mwili"). Tendo hili lilingizwa kwa wokovu wetu (Wagalatia 4:4-5; 2 Wakorintho 5:21; Waebrania 9:22). Kutoka Utwalizi na kuendelea, Mwana aliye wa milele na mwenye hakuumbwa Yeye ni Mungu tena mwanadamu. Lakini hakukuwa na wakati Mwana hakuwepo. Yeye hakuumbwa. Yesu kila wakati alikuwa na milele atabaki kuwa "Mungu wetu mkuu na Mwokozi" (Tito 2:13).

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, Yesu aliumbwa?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries