settings icon
share icon
Swali

Je, Yesu alikuwa wa dini gani?

Jibu


Yesu alizaliwa katika familia ya Wayahudi iliyofuata sheria za Kiyahudi (Luka 2:27). Ukoo wa Yesu ni kutoka kabila ya Yuda, mojawapo ya kabila kumi na mbili za Israeli. Alizaliwa katika mji wa Wayahudi wa Bethlehemu na kulelewa huko Nazareti. Yesu alikuwa amejawa na tamaduni za Kiyahudi, utaifa na dini.

Yesu aliiga dini ya Uyahudi ya Karne ya kwanza. "Alizaliwa chini ya sheria" (Wagalatia 4:4) na alikua akijifunza Torati na kufuata maagizo yake. Alitii kabisa Sheria ya Musa-amri zote, maagizo na siku kuu (Waebrania 4:14-16). Hakutii sheria tu; bali aliitimiza, pamoja na kutimiza matakwa yake (Mathayo 5:17-18; Warumi 10:4)

Yesu na wafuasi wake waliadhimisha pasaka (Yohana 2:13, 23; Luka 22:7-8) na Sikukuu ya Vibanda (Yohana 7:2, 10). Aliadhimisha Sikukuu ya Wayahudi katika Yohana 5:1. Aliudhuria ibada na kufundisha katika masinagogi (Marko 1:21; 3:1; Yohana 6:59; 18:20). Aliwashauri wengine kufuata sheria ya Musa na kutoa dhabihu (Marko 1:44). Alichochea kuheshimu sheria jinsi ilivyokuwa inafundishwa na waandishi na Mafarisayo wa wakati wake (Mathayo 23:1-3). Alinukuu Tanakh mara kwa mara ( Kwa mfano, Marko 12:28-31; Luka 4:4, 8, 12). Katika haya yote, Yesu alionyesha kuwa dini yake ilikuwa Uyahudi.

Yesu alipokuwa akiongea na kundi la Wayahudi, aliwapa changamoto: "Ni nani miongoni mwenu anishuhudiaye yakuwa nina dhambi?" (Yohana 8:46). Ikiwa Yesu angekuwa ameacha kufuata mafundisho ya Uyahudi, maadui wake wangechukua fursa hii kumhukumu. Yesu alikuwa na ustadi wa wa kuwanyamazisha wakosoaji wake (Mathayo 22:46).

Yesu alikuwa na maneno mengi makali kwa viongozi wa dini yake. Ni muhimu kukumbuka kwamba hukumu ya Yesu kwa Wafarisayo, waandishi, na Masadukayo (Mathayo 23) haikuwa hukumu ya Sheria ama ya Uyahudi wa wakati huo. Matamshi ya Yesu kwa wanafiki, maafisa wa ufisadi, waliokuwa wanajiona watakatifu yalikua tofauti na pongezi kwa wale waliojitolea mbele za Mungu na waliishi kwa Imani yao kwa uaminifu (Tazama Luka 21:1-4). Yesu alizungumza dhidi ya viongozi wa dini kwa sababu "walifundisha mafundisho yaliyo maagizo ya wanadamu" (Mathayo 15:9). Mara mbili, Yesu aliwatoa waliokuwa na unyang'anyi, wenye dhambi (Yohana 2:14-17; Mathayo 21:12-13). Vitendo hivi havikuundwa kuangamiza Uyahudi bali kuutakasa.

Yesu alikuwa Myahudi mwangalifu aliyefuata Sheria. Kifo chake kilitamatisha Agano la kale ambalo Mungu alikuwa amefanya na Israeli-hii ilidhibitishwa kwa kupasuka kwa pazia la hekalu (Marko 15:38)-na kuanzisha Agano Jipya (Luka 22:20). Kanisa la kwanza lilikuwa na msingi wa Uyahudi, na imani ya Uyahudi, na wengi wa waumini wa kwanza walikuwa Wayahudi. Lakini waumini walipomtangaza Yesu aliyefufuka kama Masihi, Wayaudi wasioamini waliwakataa basi wakalazimika kuondoka kutoka kwa Uyahudi.

Yesu ndiye Masihi ambaye Wayahudi walikuwa wanatazamia. Alizaliwa katika dini ya Uyahudi, alikamilisha dini ya Uyahudi na wakati watu wake walimkataa, Yeye alitoa maisha yake kama dhabihu ya dhambi za ulimwengu. Damu yake ilidhibitisha Agano Jipya na mara baada ya kifo chake, Uyahudi ulipoteza hekalu, ukuhani na dhabihu zake.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, Yesu alikuwa wa dini gani?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries