settings icon
share icon
Swali

Je! Israeli yote itaokolewa katika nyakati za mwisho?

Jibu


Warumi 11:26 kwa wazi inasema, "Hivyo Israeli wote wataokolewa." Swali ambalo hujibuka ni: "Israeli inamaanisha nini?" Israeli ya baadaye ni halisi au ni ya kimafumbo (kwa mfano, kurejelea kabila ya Kiyahudi au inarejelea kanisa)? Wale wanaochukua namna ya kawaida kwa ahadi ya Agano la Kale wanaamini kwamba uzao wa Abrahamu, Isaka, na Yakobo watarejeshwa kwa uhusiano mzuri na Mungu na kupokea utimilifu wa maagano. Wale wanaotetea theolojia badala hasa wao huthibitisha kwamba Kanisa limechukua nafasi ya Israeli na litarithi ahadi za Mungu kwa Israeli; maagano, basi, yatatimizwa tu kwa hali ya kiroho. Kwa maneno mengine, teolojia mbadala inafundisha kuwa Israeli haitarithi ardhi halisi ya Palestina; Kanisa ndio "Israeli mpya," na kabila la Israeli milele limetengwa na ahadi-Wayahudi hawatarithi Nchi ya Ahadi kama Wayahudi peke yake.

Tuchukue mtazamo halisi. Kifungu ambacho kinazungumzia juu ya Israeli ya baadaye ni vigumu kuviangalia kwa njia ya kimafumbo kwa kanisa. Maandishi mwafaka ambayo ni (Warumi 11:16-24) yanaionyesha Israeli kuwa tofauti na kanisa: "tawai la kawaida"ni Wayahudi na "matawi ya ulimwengi" ni watu wa Mataifa. Mzeituni unarejelea watu wa Mungu wote. "Matawi ya bustani" (Wayahudi) "wamekatwa" kutoka kwa mti kwa kutoamini, na "matawi mwitu" (watu wa Mataifa walioamini) wamepandikizwa. Hii ina adhari ya kuwafanya Wayahudi kuona "wivu" na kisha kuwavuta kuja kwa imani katika Kristo, ili waweze "kupandikizwa" tena wapokee urithi wao walioahidiwa. "Matawi ya bustani" bado ni tofauti na "matawi ya mwitu," ili agano la Mungu na watu wake litimizwe halisi. Warumi 11: 26–29, ikinukuu Isaya 59: 20–21; 27: 9; Yeremia 31: 33-34, inasema:

"Hapo ndipo taifa lote la Israeli litakapookolewa, kama yasemavyo Maandiko Matakatifu: "Mkombozi atakuja kutoka Siyoni, atauondoa uovu wa wazawa wa Yakobo. Hili ndilo agano nitakalofanya nao wakati nitakapoziondoa dhambi zao." Kwa sababu wanaikataa Habari Njema, Wayahudi wamekuwa maadui wa Mungu, lakini kwa faida yenu nyinyi watu wa mataifa. Lakini, kwa kuwa waliteuliwa, bado ni marafiki wa Mungu kwa sababu ya babu zao. Maana Mungu akisha wapa watu zawadi zake na kuwateua, hajuti kwamba amefanya hivyo."

Hapa Paulo anasisitiza hali ya wito "usiovutika" wa Israeli kama taifa (angalia Warumi 11:12). Isaya alitabiri kuwa wale wa Israeli "waliobaki" siku moja waitwa "Watu Watakatifu", Watu waliokombolewa na Mwenyezi-Mungu" (Isaya 62:12). Haijalishi hali ya sasa ya Israeli kutoamini, mabaki ya baadaye hakika watatubu na kutimiza wito wao kuwa watakatifu kwa Imani (Warumi 10:1-8; 11:5). Uongofu huu utaambatana na utimilifu wa utabiri wa Musa wa urejesho wa kudumu wa Israeli katika nchi (Kumbukumbu 30: 1-10).

Wakati Paulo anasema kuwa Israeli "itaokolewa" katika Warumi 11:26, anarejelea ukombozi kutoka dhambi (Warumi 11:27) pindi wanapomkubali Mwokozi, Masihi wao katika nyakati za mwisho. Musa alisema "Bwana Mungu wako ataitahiri mioyo yenu na mioyo ya wazao wenu ili mweze kumpenda kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote ukaishi" (Kumbukumbu 30:6). Israeli kuridhi nchi ambayo Abrahamu aliahidiwa itakuwa sehemu muhimu mpango kamili wa Mungu (Kumbukumbu 30:3-5).

Je! ni namna gani "Israeli yote itaokolewa"? Maelezo mengi ya ukombozi yamejaza vifungu vya Zekaria 8-14 na Ufunuo 7-19, ambavyo vyazungumzia kuhusu Israeli ya nyakati za mwisho katika kurudi kwa Yesu. Aya kuu inayoelezea kuhusu vile mabaki wa Israeli watakavyokuja kwao kwa imani siku za baadaye ni Zekaria 12:10, "Nami nitamiminia nyumba ya Daudi na wakazi wa Yerusalemu roho ya neema na maombi. Watanitazama mimi, yule waliyemchoma. Nao watamwombolezea kama mtu anayemwombolezea mwanawe wa pekee na kusikitika kwa uchungu kama anayemsikitikia mzaliwa wake wa kwanza wa kiume." Hii inatokea mwisho mwa kipindi cha matezo ambacho kimetabiliwa katika Danieli 9:24-27. Mtume Yohana anarejelea tukio hili katika Ufunuo 1:7. Habari za waumini mabaki wa Israeli imefupishwa katika Ufunuo 7:1-8. Hawa waaminifu Bwana atawaokoa na kuwarejesha Yerusalemu "kwa uaminifu na haki" (Zakaria 8:7-8).

Baada ya Israeli kurejeshwa kiroho, Kristo ataanzisha ufalme wake wa milenia duniani. Israeli itakusanywa tena kutoka mwisho wote wa dunia (Isaya 11:12; 62:10). Mifupa "mikavu" katika maono ya Ezekieli itakusanywa pamoja, kufunikwa na mwili, na kufufuliwa kimiujiza (Ezekieli 37: 1-14). Kama vile Mungu alivyoahidi, wokovu wa Israeli utahusisha mwamko wa kiroho na nyumba ya kijiografia: "Nitatia Roho yangu ndani yenu nanyi mtaishi, nami nitawakalisha katika nchi yenu wenyewe" (Ezekieli 37:14).

Katika siku ya Bwana, Mungu "kurudisha mabaki ya watu wake" (Isaya 11:11). Yesu Kristo atarudi na kurejesha majeshi yote yaliyokusanyika kwa uasi dhidi Yake (Ufunuo 19). Wenye dhambi watahukumiwa, na mabaki waaminifu wa Israeli watatengwa milele kama watu wakatatifu wa Mungu (Zakaria 13:8-14:21). Isaya 12 itakuwa wimbo wao wa ukombozi; Zayoni itatawala mataifa yote yaliyo chini beramu ya Mfalme Masihi.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Israeli yote itaokolewa katika nyakati za mwisho?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries