Injili ya Yuda ni gani?


Swali: "Injili ya Yuda ni gani?"

Jibu:
Wakati fulani mnamo mwaka 1970, kwenye pango kule Misri, sehemu ya nakala ya"Injili ya Yuda" ilipatikana. Mazingira yaliyopelekea kupatikana kwake yameelezewa kuwa tatanishi na yaliyokosa msingi, huku waliomiliki sehemu ya maandiko hayo wakitaka pesa mingi ndivyo waweze kuitambulisha na kuipeana. Kwa karne kadhaa, hakuna shirika lililokuwa tayari kuinunua kwa maana ilikuwa na msingi duni. Mwishowe sehemu ya injili hiyo ilinunuliwa na shirika moja la kutoka Uswizi. Baadae kuweko kwa sehemu ya Injili ya Yuda iliwekwa wazi kwa umma mwaka wa 2004, ila kutolewa kikamilivu kwa nakala hiyo ilicheleweshwa mara kwa mara, baadaye ikatolewa Aprili 2006. Tarehe ya uandishi halisi wa Injili ya Yuda inafikiriwa kuwa AD 150, huku ikitambulika na Wamisri kuwa katika mwisho wa karne ya 3. Kulingana na semi tofauti, kufikia thuluthi ya andiko hilo linakosa ama halina umuhimu.

Kabla ya ugunduzi huu, marejeleo ya kipekee kwa Injili ya Yuda yalikuwa kwenye maandishi ya mkiristo wa karne 2 aliyeitwa Irenaeus. Irenaeus kimsingi alikuwa ameandika kuwa Injili ya Yuda ilikuwa "imetolewa kwenye historia" ya kutokana na waliochukia na kupinga Mungu. Umuhimu wa Injili ya Yuda ulikuwa kwamba Yesu alimtaka Yuda amusaliti yeye kwa sababu ilikuwa ya maana ili kutimiza mipango ya Yesu. Kama ilikuwa mipango ya Yesu Yuda kumusaliti, mbona Yesu alimuita Yuda kuwa "mwana wa upotevu" [Yohana 17:12] na kusema kuwa ingekuwa afadhali Yuda asingali zaliwa [Mathayo 26:24]? Kama Yuda alikuwa tu akifuata masharti ya Yesu,mbona alijitia kitanzi punde tu alipoona Yesu kachukuliwa kuteswa [Mathayo 27:5]

Injili ya Yuda ni kusanyiko la injili, linalodhihirisha kusanyiko la maono ya wakristo. Injili ya Yuda ni kusanyiko lisilo la kweli, sawia na Injili ya Thomaso, Injili ya Maria, na pia Injili ya Filipo. Jinsi tu Yuda alimkana Yesu na Kumsaliti kupitia kwa busu, injili ya Yuda inapinga injili ya kweli na ukweli wa Mungu kutokana na maonyesho yanayojidhihirisha.

English


Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Injili ya Yuda ni gani?

Jua jinsi ya ...

kutumia milele na MunguPata msamaha kutoka kwa Mungu