settings icon
share icon

Injili ya Yohana

Mwandishi: Yohana 21: 20-24 inaeleza mwandishi kama "mwanafunzi ambaye Yesu alimpenda," na kwa sababu ya kihistoria na ndani hii inaeleweka kuwa Yohana Mtume, mmoja wa wana wa Zebedayo (Luka 5:10).

Tarehe ya kuandikwa: Ugunduzi wa baadhi ya vipande vya mafunjo yaliyoandikwa karibu AD 135 zinahitaji kitabu kuwa huenda kiliandikwa, kunakiliwa, na kusambazwa kabla ya hapo. Na wakati baadhi ya watu hufikiri kiliandikwa kabla ya Yerusalemu kuharibiwa (AD 70), AD 85-90 ni muda unaokubalika zaidi kwa ajili ya kuandika kwake.

Kusudi la Kuandika: Yohana 20:31 inatoa lengo kama ifuatavyo: "Lakini hizi zimeandikwa ili mpate kuamini kwamba Yesu ni Kristo, Mwana wa Mungu, na kwa kuamini mpate kuwa na uzima kwa jina lake." Tofauti na muhtasari tatu ya Injili, lengo la Yohana si kuwasilisha masimulizi ya kihistoria ya maisha ya Kristo, lakini kuonyesha uungu wake. Yohana hakuwa anatafuta tu kuimarisha imani ya waumini wa kizazi cha pili pamoja na kuleta imani kwa wengine, lakini pia alitaka kurekebisha mafundisho ya uongo ambayo yalikuwa yanaenea. Yohana alisisitiza Yesu Kristo kama "Mwana wa Mungu," Mungu kamili na mwanadamu kamili, kinyume na yale mafundisho ya uongo ambayo yaliona "roho ya Kristo" kuwa ilikuja kwa Yesu binadamu katika ubatizo wake na kumwondoka katika kusulubiwa.

Mistari muhimu: "Hapo mwanzo kulikuwako na Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu ... Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba, amejaa neema na kweli "(Yohana 1: 1,14).

"Siku ya pili yake amwona Yesu anakuja kwake, akasema, 'Tazama mwana kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu!" (Yohana 1:29).

"Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe Pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele" (Yohana 3:16).

"Yesu akajibu, akawaambia, 'Hii ndiyo kazi ya Mungu, mmwaamini yeye aliyetumwa na yeye" (Yohana 6:29).

"Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu. Mimi nilikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele" (Yohana 10:10).

"Nami nawapa uzima wa milele, wala hawatapotea kamwe, wala hakuna mtu atakayewapokonya katika mkono wangu" (Yohana 10:28).

"Yesu akamwambia, Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi; naye kila aishiye na kuniamini hatakufa kabisa hata milele. Je, unayasadiki hayo?" (Yohana 11: 25-26).

"Hivyo watu wote watatambua ya kuwa ninyi mmekuwa wanafunzi wangu, mkiwa na upendo ninyi kwa ninyi" (Yohana 13:35).

"Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi" (Yohana 14: 6).

"Yesu akamwambia, mimi nimekuwapo pamoja nanyi siku hizi zote, wewe usinijue, Filipo? Aliyeniona mimi amemwona Baba; basi wewe wasemaje, Utuonyeshe Baba'" (Yohana 14: 9).

"Uwatakase kwa ile kweli. Neno lako ndiyo kweli" (Yohana 17:17).

"Basi Yesu alipokwisha kuipokea ile siki, alisema, Imekwisha! Akainama kichwa, akaisalimu roho yake "(Yohana 19:30).

"Yesu akamwambia, wewe, kwa kuwa umeniona, umesadiki; wa heri wale wasioona, wakasadiki." (Yohana 20:29).

Muhtasari kwa kifupi: Injili ya Yohana inachagua miujiza saba tu kama ishara ya kuonyesha uungu wa Kristo na kuelezea huduma yake. Baadhi ya ishara hizi na hadithi hupatikana tu katika Yohana. Yake ni Injili ya kiteolojia zaidi kuliko Injili zingine nne na mara nyingi inatoa sababu zilizofichwa katika matukio yaliyotajwa katika Injili zingine. Anashiriki mengi kuhusu huduma ya Roho Mtakatifu inayokaribia baada ya kupaa kwake. Kuna baadhi ya maneno au misemo ambayo Yohana mara nyingi anatumia kuonyesha mada zake zinazo rudiwa katika Injili yake; amini, shahidi, Msaidizi, uzima - mauti, mwanga - giza, mimi ... (kama kwamba Yesu ndiye "Mimi ndimi"), na upendo.

Injili ya Yohana inatanguliza Kristo, si kutoka kuzaliwa kwake, lakini kutokana na "mwanzo" kama "Neno" (Nembo) ambao, kama Uungu, anashiriki katika kila nyanja ya uumbaji (1: 1-3) na ambaye baadaye anakuwa mwili (1 : 14) ili aweze kuchukua dhambi zetu kama asiye na doa, sadaka ya Mwanakondoo (Yohana 1:29). Yohana anachagua mazungumzo ya kiroho ambayo yanaonyesha kwamba Yesu ni Masihi (4:26) na kueleza jinsi mtu anaokolewa kwa kifo chake msalabani kwa sababu ya watu (3: 14-16). Anawakasirisha viongozi wa Wayahudi mara kwa mara kwa kuwarekebisha (2: 13-16); uponyaji siku ya Sabato, na kudai sifa zinazostahili Mungu (5:18; 8: 56-59; 9: 6,16; 10:33). Yesu anawaandaa wanafunzi wake kwa kifo chake kinachokuja na kwa ajili ya huduma zao baada ya ufufuo wake na kupaa (Yohana 14-17). Yeye kisha kwa hiari anakufa msalabani kwa ajili yetu (10: 15-18), na kulipa deni la dhambi zetu kikamilifu (19:30) ili atakayemwamini kama Mwokozi wao kutoka dhambini ataokolewa (Yohana 3: 14-16). Kisha Yeye anaamuka kutoka kwa wafu, kumshawishi hata mwenye mashaka zaidi wa wanafunzi wake kuwa yeye ni Mungu na Mwalimu (20: 24-29).

Mashirikisho: Yohana kuonyesha Yesu kama Mungu wa Agano la Kale kunaonekana zaidi kwa msisitizo katika "Mimi Ndimi" kauli saba za Yesu. Yeye ni "Mkate wa uzima" (Yohana 6:35), uliotolewa na Mungu kulisha roho za watu wake, kama alivyotoa mana kutoka mbinguni kulisha waisraeli katika jangwa (Kutoka 16: 11-36). Yesu ni "Nuru ya ulimwengu" (Yohana 8:12), Nuru ile ile ambayo Mungu aliahidi watu wake katika Agano la Kale (Isaya 30:26, 60: 19-22) na ambayo itapata kilele chake katika Yerusalemu mpya wakati Kristo Mwanakondoo atakuwa Mwanga wake (Ufunuo 21:23). Kauli mbili za "Mimi Ndimi" zinarejelea Yesu kama "Mchungaji mwema" na “Mlango wa kondoo zake" Hapa kuna marejeleo kwa Yesu kama Mungu wa Agano la Kale, Mchungaji wa Israeli (Zaburi 23: 1 , 80: 1; Yeremia 31:10, Ezekieli 34:23), na kama Mlango tu wa kipee wa kuingia katika zizi la kondoo, njia ya pekee ya wokovu.

Wayahudi waliamini katika ufufuo, na kwa kweli, kutumika mafundisho kujaribu kumshawishi Yesu atoe kauli ambazo wangeweza kutumia dhidi yake. Lakini kauli yake katika kaburi la Lazaro "Mimi ndiye ufufuo na uzima" (Yohana 11:25) lazima iliwashsngaza sana. Alikuwa anadai kuwa chanzo cha ufufuo na mmiliki wa uwezo juu ya uzima na mauti. Hakuna mwingine zaidi ya Mungu mwenyewe anaweza kudai jambo kama hilo. Vile vile, madai yake kuwa "njia, ukweli na uzima" (Yohana 14: 6) lilimshirikisha bila kukosea kwa Agano la Kale. Yake ni "Njia ya Utakatifu" iliyotabiriwa katika Isaya 35: 8; Alianzisha Mji wa kweli wa Zekaria 8: 3 wakati Yeye, ambaye ni "ukweli" wenyewe, alikuwa katika Yerusalemu na ukweli wa Injili ulihubiriwa huko na Yeye pamoja na Mitume wake, na kama "Uzima," Yeye anathibitisha uungu wake, Muumba wa uzima, Mungu katika mwili wa binadamu (Yohana 1: 1-3). Hatimaye, kama "Mzabibu wa kweli" (Yohana 15: 1, 5) Yesu anajitambulisha mwenyewe na taifa la Israeli walioitwa shamba la mizabibu la Bwana katika vifungu vingi vya Agano la kale. Kama Mzabibu wa kweli wa shamba la mizabibu la Israeli, anajionyesha mwenyewe kama Bwana wa "Israeli ya kweli" wale wote watakaokuja kwake imani, kwa sababu "... si wote ambao wanatoka Israeli ambao ni Israeli" (Warumi 9: 6).

Vitendo Tekelezi: Injili ya Yohana inaendelea kutimiza madhumuni yake ya kuwa na habari nyingi muhimu kwa ajili ya uinjilisti (Yohana 3:16 huenda ndio mstari unaojulikana zaidi, hata kama haueleweki kikamilifu na wengi) na mara nyingi unatumika katika masomo ya kiuinjilisti ya Bibilia. Katika kukutana kulionakiliwa kati ya Yesu na Nikodemo na mwanamke kisimani (sura 3-4), tunaweza kujifunza mengi kutoka kwa mtindo wa Yesu wa uinjilisti wa kibinafsi. Maneno yake ya faraja kwa wanafunzi wake kabla ya kifo chake (14: 1-6,16, 16:33) bado ni ya faraja kubwa katika nyakati ambazo kifo kinawachukua wapendwa wetu katika Kristo, kama ilivyo yake "maombi ya kikuhani mkuu" kwa waumini katika sura 17. Mafundisho ya Yohana kuhusu uungu wa Kristo (1: 1-3,14; 5: 22-23; 8:58; 14: 8-9; 20:28, nk) ni msaada sana katika kupambana na mafundisho ya uongo ya baadhi ya madhehebu ambayo huona Yesu kuwa hatoshi kuwa Mungu kamili.

English

Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Injili ya Yohana
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries