settings icon
share icon

Injili ya Mathayo

Mwandishi: Injili hii inajulikana kama Injili ya Mathayo kwa sababu ilikuwa imeandikwa na mtume mwenye jina sawa. Mtindo wa kitabu hasa ni kinachotarajiwa kwa mtu ambaye alikuwa mtoza ushuru wakati mmoja. Mathayo ana nia riba katika kuandika (18: 23-24; 25: 14-15). kitabu kina utaratibu sana na kifupi. Badala ya kuandika katika mpangilio, Mathayo anapanga Injili hii kupitia majadiliano sita.

Kama mtoza ushuru, Mathayo alimiliki ujuzi ambao unafanya uandishi wake kuwa wa kusisimua zaidi kwa Wakristo. Watoza ushuru walitarajiwa kuwa na uwezo wa kuandika kwa kifupi, ambayo kimsingi ilimaanisha kwamba Mathayo angeweza kurekodi maneno ya mtu kama walipozungumza, neno kwa neno. Uwezo huu unamaanisha kwamba maneno ya Mathayo si tu yalitiwa msukumo na Roho Mtakatifu, lakini lazima yawasilishe nakala halisi ya baadhi ya mahubiri ya Kristo. Kwa mfano, Mahubiri ya Mlimani, kama yalivyoandikwa katika sura ya 5-7, ni karibu hakika rekodi ya ujumbe huo mkubwa.

Tarehe ya kuandikwa: Kama mtume, Mathayo aliandika kitabu hiki katika kipindi cha kwanza cha kanisa, pengine karibu 50 AD. Huu ulikuwa wakati ambao Wakristo wengi walikuwa Wayahudi waliokoka, hivyo lengo la Mathayo la mtazamo wa Kiyahudi katika injili hii linaeleweka.

Kusudi la Kuandika: Mathayo anatarajia kuthibitisha kwa Wayahudi kwamba Yesu Kristo ni Masihi aliyeahidiwa. Zaidi ya injili nyingine yoyote, Mathayo ananukuu Agano la Kale ili kuonyesha jinsi Yesu alitimiza maneno ya manabii wa Kiyahudi. Mathayo anaelezea kwa undani ukoo wa Yesu kutoka kwa Daudi, na anatumia aina nyingi za hotuba ambayo Wayahudi wangeridhika nazo. Upendo wa Mathayo na kuwajali watu wake ni dhahiri kupitia kwa mbinu angalifu zake kwa kuwaambia hadithi ya injili.

Mistari muhimu: Mathayo 5:17: "Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza. "

Mathayo 5: 43-44: "Mmesikia kwamba imenenwa, umpende jirani yako, na, umchukie adui yako; Lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi "

Mathayo 6: 9-13: "Basi ninyi salini hivi; Baba yetu uliye mbinguni, jina lako litukuzwe, ufalme wako uje, mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni. Utupe leo riziki yetu. Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu. Na usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu. [Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele. Amina "

Mathayo 16:26: "Kwani atafaidiwa nini mtu akiupata ulimwengu wote, na kupata hasara ya nafsi yake? Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake? "

Mathayo 22: 37-40: "Akamwambia, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote. Hii ndiyo amri iliyo kuu, tena ni ya kwanza. Na ya pili yafanana nayo, nayo ni hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako. Katika amri hizi mbili hutegemea torati yote ya manabii. "

Mathayo 27:31: "Walipokwisha kumdhihaki, wakalivua lile vazi, wakamvika mavazi yake, wakamchukua kumsulubisha."

Mathayo 28: 5-6: "malaika akajibu, akawaambia wale wanawake, msiogope ninyi; kwa maana najua ya kuwa mnamtafuta Yesu aliyesulubiwa. Hayupo hapa; kwani amefufuka kama alivyosema. Njoni, mpatazame mahali alipolazwa. "

Mathayo 28: 19-20: "Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi. Na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari. "

Muhtasari kwa kifupi: Mathayo anajadili ukoo, kuzaliwa kwake na maisha ya mapema ya Kristo katika sura mbili za kwanza. Kutoka huko, kitabu kinajadili huduma ya Yesu. maelezo ya mafundisho ya Kristo yamepangwa karibu na "mahubiri" kama vile mafundisho Mlimani katika sura ya 5 hadi 7. Sura ya 10 inahusu dhamira na lengo la wanafunzi, sura ya 13 ni mkusanyiko wa mafumbo; sura ya 18 inajadili kanisa; sura ya 23 inaanza mahubiri kuhusu unafiki na siku za usoni. Sura ya 21 hadi 27 zinajadili kukamatwa, mateso, na utekelezaji/utimizaji wa Yesu. sura ya mwisho inaelezea ufufuo na Agizo Kuu.

Mashirikisho: Kwa sababu kusudi la Mathayo ni kuwasilisha Yesu Kristo kama mfalme na Masihi wa Israeli, ananukuu kutoka kwa Agano la Kale zaidi kuliko waandishi wengine watatu wote wa injili. Mathayo ananukuu zaidi ya mara 60 kutokana na vifungu vya unabii vya Agano la Kale, na kuonyesha jinsi Yesu ameyatimiliza. Anaanza injili yake na ukoo wa Yesu, akimfuatilia hadi kwa Ibrahimu, baba ya Wayahudi. Kutoka huko, Mathayo ananukuu sana kutoka kwa manabii, mara nyingi akitumia maneno "kama lililonenwa na nabii" (Mathayo 1: 22-23, 2: 5-6, 2:15, 4: 13-16, 8: 16-17, 13:35, 21: 4-5). Mistari hii inarejelea unabii wa Agano la Kale wa kuzaliwa kwake na Bikra (Isaya 7:14) katika Bethlehemu (Mika 5: 2), kurudi kwake kutoka Misri baada ya kifo cha Herode (Hosea 11: 1), huduma yake kwa watu wa mataifa (Isaya 9: 1-2, 60: 1-3), uponyaji wake wa kiajabu wa mwili na roho (Isaya 53: 4), kuzungumza kwake kwa mafumbo (Zaburi 78: 2), na kuingia kwake kwa kishindo katika Yerusalemu (Zekaria 9: 9 ).

Vitendo Tekelezi: Injili ya Mathayo ni utangulizi mzuri kwa mafundisho ya kimsingi ya Ukristo. Mtindo wa muhtasari wenye mantiki unarahisisha kufuatilia majadiliano ya mada mbalimbali. Mathayo ni muhimu hasa kwa kuelewa jinsi maisha ya Kristo yalikuwa kutimiza kwa unabii wa Agano la Kale.

Walengwa wa Mathayo walikuwa Wayahudi wenzake, ambao wengi wao hasa Mafarisayo na Masadukayo- walisumbua kwa kukataa kumkubali Yesu kama Masihi wao. Licha ya karne nyingi za kusoma na kujifunza Agano la Kale, macho yao yalipumbazwa kwa ukweli wa Yesu alikuwa ni nani. Yesu aliwakemea kwa nyoyo zao kuwa ngumu na kukataa kwao kumtambua yule ambaye wamekuwa wakimngojea (Yohana 5: 38-40). Walitaka Masihi kulingana na matakwa yao wenyewe, yule ambaye atatimiza mahitaji yao wenyewe na kufanya kile ambacho walimtaka kufanya. Ni mara ngapi tunamtafuta Mungu kulingana na matakwa yetu wenyewe? Je, si tunamkataa kwa kumpachikia tu sifa ambazo zinakubalika kwetu, zile ambazo zinatufanya kuhisi vizuri- upendo wake, huruma, neema- ilhali tunakataa zile ambazo ni za kuchukiza- ghadhabu yake, haki, na hasira takatifu? Tusithubutu kufanya makosa ya Mafarisayo, kujenga Mungu kwa mfano wetu wenyewe na kisha kumtarajia aishi kulingana na viwango vyetu. Mungu kama huyo si kitu zaidi kuliko sanamu. Biblia inatupa zaidi ya taarifa za kutosha kuhusu asili ya kweli na utambulisho wa Mungu na Yesu Kristo kuhalalisha ibada yetu na utiifu wetu.

English

Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Injili ya Mathayo
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries