settings icon
share icon
Swali

Je! Ni kwa nini inaonekana kuwa vitabu vinne vya Injili vinawakilisha ujumbe tofauti wa wokovu kuliko vitabu vingine vya Agano Jipya?

Jibu


Lazima tukumbuke kuwa Biblia ilinuiwa kuchuliwa vile ilivyo yote. Vitabu vinavyofuata vitabu vine vya Injili vinatazamia, na vitabu vinavyofuata ni vya maelezo. Katika Biblia nzima, chenye Mungu anahitaji ni imani (Mwanzo 15:6; Zaburi 2:12; Habakuki 2:4; Mathayo 9:28; Yohana 20:27; Waefeso 2:8; Waebrania 10:39). Wokovu hauji kwa ajili ya matendo yetu bali kwa kuamini chenye Mungu amefanya kwa niapa yetu.

Kila mojawapo ya Injili ina msisitizo wake juu ya huduma ya Kristo. Mathayo akiwaandikia Wayahudi wasikilizaji/hadhira, alisisitiza vile Yesu alitimiza unabii wa Agano la Kale, akionyesha kuwa Yeye si Masihi ambaye anatarajiwa tena. Marko anasimulizi fupi akisimulia miujiza ya ajabu ya Yesu bila kuandika simulizi ya Yesu refu. Luka anamwonyesha Yesu kama suluhisho la maovu ya ulimwengu, akisisitiza ubinadamu wake kamili na vile anavyowajali wanyonge, wanaoteseka na kukataliwa. Yohana anasisitiza uungu wa Yesu kwa kuchagua mazungumzo na misemo mingi ya Yesu juu ya swala na pia akijuisha "ishara" ambazo zilizothibitisha kuwa Yeye ni Mwana wa Mungu.

Injili Nne zinafanya kazi kwa pamoja ili kutoa ushuhuda kamili ulio kamilika juu ya Yesu, ni taswira nzuri sana ya Mungu-Mwanadamu. Ingwa Injili zinatofautiana kidogo kimandhari, somo kiungo ni lile lile. Zote humwonyesha Yesu kama yule aliyekufa ili kuwaokoia wenye dhambi. Zote zinasimulia ufufuo Wake. Iwe waandishi zinamwonyesha Yesu kama Mfalme, Mtumishi, Mwana wa Adamu, au Mwana wa Mungu, zilikuwa na lengo moja kuwa watu wamwamini Yeye.

Sasa tutazama ndani kuichunguza teolojia ya Injili. Yohana anajumuisha kauli mbali mbali za imani na amri za kuamini. Ujumuisho huu unaingililiana na kusudi lake alilolisema, "Yesu alifanya miujiza mingine mingi mbele za wanafunzi wake, ambayo haikuandikwa katika kitabu hiki" (Yohana 20:31). Injili zingine (muhtasari) sio kuwa hazishughuliki na dhana kwamba tunamtumainia Kristo. Wito wao kwa imani hayako wazi lakini ni ya kweli.

Yesu alitangaza hitaji la uadilifu, na anatoa onyo dhadi ya adhabu ya dhambi, ambayo ni jahanamu. Walakini, kila wakati Yesu anamwonyesha Mungu kuwa kiwango cha uadilifu na Yeye mwenyewe kama njia ya haki na bili Kristo haki haiwezi patikana na basi kuzimu hakuwezi epukika. Mahubiri ya Mlimani (Mathayo 5-7) ni mfano wa uhakika:

• Yesu anaanza Mahubiri Mlimani kwa maelezo ya maisha yaliyobarikiwa (Mathayo 5:1-12). Heri haitwambii "jinsi ya" kuwa wenye haki, bali inaelezea uadilifu.

• Anajiwakilisha Mwenyewe kama timizo la sheria ya Agano la Kale (Mathayo 5:17-18). Hii ni aya kuu kwa sababu, kupata haki yetu wenyewe, lazima tutimize sheria; na hapa Yesu anasema kuwa ataitimiza sheria kwa niapa yetu.

• Yesu anasema kuwa hakuna kiwango cha metendo yetu mema yanaweza kutuingiza mbinguni (Mathayo 5:29). Hii ni kauli nyingine muhimu katika mahubiri. Mafarisayo walikuwa watu waangalifu wa dini wa siku hizo, lakini Yesu anasema hata wao sio wema kamili kuingia mbinguni. Yesu anaendelea kwa kusema kuwa sio mfumo wa dini unaweza kuokoa, bali ni Yeye mwenyewe.

• Anafanya ieleweke zaidi maana ya uadilifu na kuufafanua kulingana ni kiwango cha Mungu, badala ya vile mwanadamu wanavyoitafsiri sheria (Mathayo 5:21-48). Anaeleza kusudi la Mungu katika sheria nyingi za Agano la Kale. Kiwango kiko juu sana ambacho kinamfanya kila mmoja, hata wale wamejitolea kwa dini kuwa na hatia mbele za Mungu.

• Anaelezea shughuli tatu kuu za dini-mitende, maombi, na kufunga- kuwa ukafiri wakati yanafanywa kwa nje tu (Mathayo 6:1-18). Katika sheria ambayo aliitaja, chenye Yesu alilenga ni hali ya moyo wa mwanadamu, na sio matendo tunayoweza kuona.

• Anaonya kwamba kutakuwa na "wengi" katika siku ya hukumu ambao watakuwa wamefanya mambo makuu kwa Mung una bado watafungiwa kuingia mbinguni (Mathayo 7:21-23). Sababu amabyo imetolewa ni kuwa Yesu hakuwai "wajua." Hakukuwa na uhusiano unaotambulika, bali ni metendo "mema" ambayo hayatoshi.

• Yesu anatamatisha Mahubiri Mlimani kwa kauli kuu kuwa Yeye pekee ndiye msingi kwa mtu kujenga maisha yake ya dini (Mathayo 7:24-27). Ni wito mwamini "maneno haya Yngu" ambayo yatosha kuachana na misingi mingine yote.

Kwa muhtasari, katika Mahubiri ya Mlimani Yesu kwa uangalifu anaunda upya dini ya kifarisayo ya matendo mema, anaelekeza kwa utakatifu ulio mkuu kuliko ule wetu, na anajitoa Mwenyewe kuwa chanzo pekee cha dini. Kukubali chenye Yesu anasema katika mahubiri haya kunahitaji imani katika Utu wake.

Injili ya Mathayo inaendelea na kusisitiza imani katika aya sifuatazo: Mathayo 8:10, 13, 26; 9:2, 22, 28-29; 12:21; 13:58; 14:31; 15:28; 16:8; 17:17; na 18:6. Pia, Mathayo anajumuisha kumwasilisha Yesu kama Mwana wa Mungu katika andiko hili: "Akawauliza, "Je, ninyi mnasema mimi ni nani?" Simoni Petro akamjibu, "Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai."Naye Yesu akamwambia, "Heri wewe, Simoni Bar-Yona, kwa maana hili halikufunuliwa kwako na mwanadamu, bali na Baba yangu aliye mbinguni'" (Mathayo 16:15-17).

Injili ya Marko ina takribani marejeleo ya imani katika Kristo katika aya sifuatazo: 1:15; 2:5; 4:40; 5:34, 36; 6:6; 9:19, 23, 42; 10:52; 11:23; na 16:14. Katika Injili ya Luka tunaona angalau aya hizi zikikuza imani katika Kristo: Luka 5:20; 7:9, 50; 8:12, 25, 48, 50; 9:41; 12:28, 46; 17:19; 18:8, 42; na 24:25. Vile tunavyoendelea kuona Maandiko kama fungu nzima moja tutaona kuwa kuna ujumbe mmoja tu wa wokovu, na Injili nne zinatoa msingi wa ujumbe huo.

Nyaraka zinazofuata Injili zinaelezea juu ya mada yiyo hiyo: wokovu kwa imani katika Kristo. Mada kuu ya Warumi ni haki inayokuja kupitia Mungu na fundisho la kuthibitishwa kwa neema kupitia kwa imani. Mada kuu ya Wagalatia na Wakolosai vile vile ni kama ile ya Warumi. Kitabu cha Waebrania kinasisitiza ufahari wa Kristo na ukamilifu Wake, "mwanzilishi na mkamilishaji wa imani yetu" (Waebrania 12:2). Wakorintho wa Kwanza na Pili, Waefeso, Wafilipi, 1 na 2 Wathesalonike, barua za kichungaji za Timotheo na Tito, Filemoni, Yakobo, 1 na 2 Petro, zote zinaelezea maisha matakatifu, kibinafsi na kwa Pamoja ndani ya kanisa, na tumaini la kesho ambalo linapaswa kuwa ni matokeo ya asili ya maisha katika Kristo. Nyaraka tatu za Yohana zinarudia misingi ya imani na kuonya wale ambao watauliza maswali dhidi yake, pia mada kuu katika Yuda. Ufunuo, kitabu cha mwisho cha Agano Jipya, kinawakilisha tendo la mwisho la mpango wa Mungu kwa mwanadamu na hatima ya wale wanaoshikilia imani ile ile iliyoelezewa katika Agano Jipya nzima-imani katika Kristo pekee.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Ni kwa nini inaonekana kuwa vitabu vinne vya Injili vinawakilisha ujumbe tofauti wa wokovu kuliko vitabu vingine vya Agano Jipya?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries