settings icon
share icon
Swali

Injili ya Maria Magdalene ni nini?

Jibu


Injili ya Maria Magdalene iligunduliwa katika maandiko ya Akhmim kule Kairo Misri,mnamo 1896. Ilikosa kuwekwa wazi kwa umma hadi 1955, wakati ilichapishwa kufuatia umaarufu wa maktaba ya Nag Hammadi. Iliandikwa katika Kigiriki na Kikoptiki na Injili hiyo ya Maria Magdalene kupewa tarehe za karne ya 3 [Kigiriki] na karne 5 [Kikoptic]. Injili ya Maria Magdalene ilitajwa kwenye baadhi ya maandishi ya wazee wa kanisa la kwanza mapema hadi karne ya 3. Katika nakala ya kipekee inayojulikana, kurasa kama kumi kamilifu zingali zinakosa, pamoja na kurasa za kwanza sita. Kwa hivyo ni ngumu kupeana mwelekeo wa kiukweli na wa kueleweka kwa nakala hiyo yote.

Injili ya Maria Magdalene ingekuwa mwafaka kupewa kichwa kama "Injili ya Maria" kwa kuwa Maria anayetajwa kwenye Injili hajatajwa popote kama Maria Magdalene. Katika Agano Jipya, kuna wanawake sita wanaoitwa Maria, na watatu kati yao wakiwa maarufu katika maisha ya Yesu: Maria, mama wa Yesu; Maria Maagdalene; na Maria wa Bethani. Ni kitamaduni tu ambapo Maria kwenye Injili ya Maria inahashiria Maria Magdalene. Kwa ajili ya uwazi, tutakizia kuwa Maria Magdalene ndiye Maria katika Injili ya Maria.

Wenye wazo kinzani ya kudhania wamedhihirisha na kuleta kutoelewana kati ya wapinga Ukristo inavyowekwa wazi na Petero] na ukristo wa kweli [unaoelezewa na Maria]. Nakala la Da Vinci inaelezea hilo wazo pinzani la kudhania kwa kiwango kingine cha juu zaidi kwa kuonyesha kuwa kanisa la wakristo linaficha uhusiano wa Yesu na Maria Magdalene na kukataa kuwa Yesu alimchagua Maria Magdalene kuwa kiongozi wa kanisa. Shida iliopo katika maelezo haya ni kuwa hakuna dhihirisho la kutetea maneno hayo, sio hata katika Injili ya Maria. Injili ya Maria haijataja popote kuwa Yesu alimchagua Maria kuwa kiongozi wa kanisa. Injili ya Maria haijanukuu popote Yesu na Maria walikuwa na uhusiano wa kimapenzi.

Injili ya Maria haikuandikwa na Maria Magdalene wala Maria yeyote yule kwenye Bibilia. Mikusanyiko ya mafundisho yanayopatikana katika Injili ya Maria yanairejelea katika mwisho wa karne ya 2 AD ikiwa mapema. Kwa sababu hiyo, hakuna hakikisho la ukweli kwa mafundisho yake. Sawia na Injili ya Thomaso, Injili ya Filipo na Injili ya Yuda, injili ya Maria ni kusanyiko yanayokosa ukweli na ya kubuni, inayotumia jina la mhusika kutoka kwa Bibilia kama jaribio la kuipa ukweli kwa mafunzo hayo yasiyo ya kweli. Umuhimu wa kipekee wa kuisoma Injili ya Maria ni kwa kujifunza kuhusu uongo wa kubuni uliokuwa katika karne za kwanza za kanisa la kristo.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Injili ya Maria Magdalene ni nini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries