settings icon
share icon
Swali

Je, wokovu ni kwa imani pekee, ama imani pamoja na matendo?

Jibu


Hili halina budi kuwa swali muhimu katika elimu yote ya thiologia ya kikristo. Hili ndilo swala lililoleta mabadiliko; kutengana kwa waprotestanti na wakatoliki. hapa ndipo tofauti ya ukristo wa kibiblia na “mila za kikristo.” Je, wokovu ni kwa imani pekee ama ni kwa imani pamoja na matendo? Je, ninaokolewa kwa kumwamini Yesu kristo tu ama ni kwa kumwamini Yesu kristo na pia nitende mambo Fulani?

Jambo hili la imani pekee ama imani pamoja na matendo linafanywa gumu na aya Fulani za biblia ambazo kuzipatanisha kwake ni kugumu. Linganisha warumi 3:28, 5:1 na wagalatia 3:24. wengine huona tofauti kati ya Paulo (wokovu ni kwa imani pekee) na yakobo (wokovu ni kwa imani pamoja na matendo). Kwa uhakika, Paulo na Yakobo hawakutofautiana. Lile swali watu hupingana kwalo ni juu ya imani na matendo. Paulo anazungumzia juu ya kukubalika kwa imani pekee (Waefeso 2:8-9) huku yakobo akisema ya kuwa kukubalika ni kwa imani pamoja na matendo. Yakobo anakataa yakuwa mtu anaweza kuwa na imani bila kuonyesha mtendo mema (Yakobo 2:17-18). Yakobo anasisitiza ya kwamba imani ya kweli ya Yesu itaonyesha matendo ya maisha yaliyobadilishwa na wema (Yakobo 2:20-26). Yakobo hasemi kwamba kukubalika ni kwa imani pamoja na matendo bali mtu mwenye imani ya kweli ataidhihirisha kwa matendo mema. Mtu akisema nimuumini,lakini hana matendo mema maishani mwake – basi huyo huwa hana imani halisi ya kristo (Yakobo 2:14, 17, 20, 26).

Paulo pia anasema hayo katika maandishi yake. Matunda mema ambayo waumini wanapaswa kuwa nayo maishani mwao yameoridheshwa ktika Wagalatia 5: 22-23. Baadaya kutufahamusha ya kwamba tunaoklewakwa imani pekee wala sio kwa matendo (Waefeso 2:8-9), Paulo anatuarifu ya kuwa tuliumbwa tufanye kazi njema (Waefeso 2:10 ). Paulo anatarajia maisha ya kubadilikshwa sawa na yakobo, “Kwa hivyo, mtu akiwa ndani ya Kristo, amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamekwisha, tazama yamekuwa mapya” (Wakorintho wa pili 5:17)! Paulo na yakobo hawatofautiani katika mafundisho yao juu ya wokovu. Wanalielezea jambo hilokwa njia mbali mbali. Paulo asisitiza juu ya wokovu kupitia imani pekee huku yakobo akisisitiza kuwa imani juu ya kristo huleta matendo mema.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, wokovu ni kwa imani pekee, ama imani pamoja na matendo?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries