settings icon
share icon
Swali

Je! Ni kwa nini imani pekee ni ya muhimu?

Jibu


Sola fide, inamaanisha "Imani peke yake," ni ya muhimu kwa sababu ni mojawapo ya sifa zainazotofautisha au mambo muhimu ambayo yanatenganisha Injili ya kweli ya kibiblia na ile injili ya uwongo. Kilicho hatarini ni Injili yenyewe ni kwa hivyo ni suala la uzima wa mile au kifo. Kuipokea Injili vyema kwa muhimu sana kwamba Mtume Paulo angeandika katika Wagalatia 1:9, "Tulikwisha sema, na sasa nasema tena: Kama mtu yeyote anawahubirieni injili ya aina nyingine, tofauti na ile mliyokwisha pokea, huyo na alaaniwe!" Paulo alikuwa anajibu swali lile lile ambalo sola fide inaangazia-ni kwa msingi gani wanadamu wametangazwa na Mungu kuwa waadilifu? Je! Ni kwa Imani peke yake au kwa imani pamoja na matendo? Paulo anaiweka wazi katika Wagalatia na Warumi kwamba wanadamu "tupate kufanywa waadilifu kwa njia ya imani yetu kwa Kristo, na si kwa kuitii sheria" (Wagalatia 2:16), na sehemu zingine za Biblia zinakubaliana.

Sola fide ni moja wapo ya sola tano ambazo zilikuja kufafanua ni kutoa muhtasari wa masuala mihimu ya Mageuzi ya Kiprotestanti. Kila moja ya misemo hii ya Kilatini inawakilisha sehemu fulani ya mafundisho ambayo yalikuwa suala la mabishano kati ya Wanamageuzi na kanisa la Katoliki la Roma, na hii leo bado inatumika kama muhtasari wa mafundisho muhimu ya Injili na kwa maisha na mazoea ya Kikristo. Neno la Kilatini sola linamaanisha "peke yake" au "pekee" na mafundisho muhimu ya kikristo yanayowakilishwa na misemo hii tano ya Kilatini kwa ustadi inatoa muhtasari wa mafundisho ya kibiblia katika masualo hayo mihumu: sola scriptura- Maandiko peke yake, sola fide-imani peke yake, sola gratia-neema pekee, sola Christus- Kristo pekee, na sola gloria- kwa utukufu wa Mungu pekee. Kila moja wapo ni fundisho muhimu, na matokeo karibu kila wakati yatakuwa injili ya uwongo amboyo haina nguvu ya kuokoa.

Sola fide au Imani pekee ni hoja kuu ya tofauti ya sio kwa Waprotestanti tu na Wakatoliki bali kati ya Ukristo wa kibiblia na karibu dini zingine zote na mafundisho yao. Fundisho kwamba tumetangazwa kuwa wenye uadilifu na Mungu (tumehesabiwa uadilifu) kwa misingi ya Imani pekee na sio kwa matendo ni fundisho kuu la biblia na alama ambayo huwatofautisha madhehebu kutoka Ukristo wa kibiblia. Wakati dini nyingi madhehbu yanawafundisha watu matendo watakayo yafanya ili waokolewe, Biblia inafunza kuwa hatuokolewe kwa matnedo, bali kwa neema yake Mungu kupitia kwa karama yake ya imani (Waefeso 2:8-9). Ukristo wa Kibiblia ni tafauti sana kutoka kwa dini zingine kwa kuwa umejikita kwa kile Mungu alikamilisha kupitia kwa kazi ya Kristo ilimalizika, huku dini zingine zote zinategemea mafanikio ya wanadamu. Ikiwa tutaiacha fundisho la kuhesabiwa uadilifu kwa imani, basi tunaacha njia pekee ya wokovu. "Basi mtu afanyapo kazi, mshahara wake hauhesabiwi kwake kuwa ni zawadi, bali ni uadilifu yake anayostahili. Lakini kwa mtu ambaye hafanyi kazi na anamtumaini Mungu, yeye ambaye huwahesabia waovu uadilifu, imani yake inahesabiwa kuwa uadilifu" (Warumi 4:4-5). Biblia inafundisha kwamba wale wanaomtumaini Yesu Kristo kwa kuhesabiwa uadilifu kupitia kwa imani pekee wamefanywa uadilifu ya Mungu (2 Wakorintho 5:21), huku wale wanaojaribu kuanzisha uadilifu yao wenyewe au kuchanganya Imani na matendo watapokea adhabu inayowangoja wale wote wanaopungukiwa na kiwango kimilifu cha Mungu.

Sola fide/Imani pekee- fundisho la kuhesabiwa uadilifu kwa imani pekee mbali na matendo- ni kutambua kile kinachofunzwa mare kwa mara katika Maandiko-kwamba kwa wakati fulani Mungu huwatangaza wenye dhambi wasio wake kuwa wenye uadilifu kwa kuwahesabia uadilifu ya Kristo (Warumi 4:5; 5:8, 19). Hii hufanyika mbali na matendo yeyote na kabla ya mtu aanze kuwa mwenye uadilifu. Hii ni tofautisho muhimu sana kati ya theolojia ya Katoliki ambayo inafundisha kuwa matendo mema ni yanatunuku wokovu na theolojia ya Kiprotestanti inathibitisha mafundisho ya kibiblia kuwa matendo mema ni matokeo na uthibitisho wa mtu ambaye amezaliwa mara ya pili ambaye amehesabiwa uadilifu na Mungu na ameuhishwa na nguvu ya Roho Mtakatifu.

Je! sola fide ni muhimu namna gani? Ni ya muhimu sana kwa ujumbe wa Injili na ufahamu wa kibiblia juu ya wokovu ambao Martin Luther alielezea kama "nakala ambayo kwayo kanisa linasimama." Wale wanaokataa sola fide wanaikataa Injili ambayo inaweza kuwaokoa na kwa lazima wanaikubali injili potovu. Hiyo ndio maana Paulo anawalaumu sana wale waliofundisha utunzaji wa sheria au kazi zingine za matendo ya uadilifu katika Wagalatia 1:9 na vifungu vingine. Hata leo hii fundusho hili muhimu bado linapingwa vikali sana. Mara nyingi sola fide hudunishwa kiumuhimu na kuwekwa la pili badala ya kutambuliwa kuwa fundisho kuu la Ukristo ambalo lii

"Chukueni kwa mfano habari za Abrahamu: Yeye alimwamini Mungu, naye Mungu akamkubali kuwa mwadilifu. Sasa basi, jueni kwamba watu wenye kumwamini ndio walio watoto halisi wa Abrahamu. Maandiko Matakatifu yalionesha kabla kwamba Mungu atawafanya watu wa mataifa kuwa waadilifu kwa njia ya imani. Hivyo Maandiko Matakatifu yalitangulia kumtangazia Abrahamu Habari Njema: "Katika wewe mataifa yote yatabarikiwa." Basi, wale walio na imani wanabarikiwa pamoja na Abrahamu aliyeamini.Lakini wote wanaotegemea tu kutimiza yanayotakiwa na sheria, wako chini ya laana. Maana, Maandiko Matakatifu yasema: "Yeyote asiyeshika na kutimiza yote yaliyoandikwa katika kitabu cha sheria, yuko chini ya laana." Ni dhahiri kwamba sheria haiwezi kumfanya mtu kuwa mwadilifu; maana Maandiko yasema: "Mwadilifu kwa imani ataishi." (Wagalatia 3:6-11).

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Ni kwa nini imani pekee ni ya muhimu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries