settings icon
share icon
Swali

Je! Imani katika Mungu ni nini?

Jibu


Imani katika Mungu ni kumwamini kwa msingi wa ufahamu kamili wa yule aliko, vile imefunuliwa katika Biblia. Imani katika Mungu inajumuisha kukubali kiakili juu ya ukweli kuhusu Mungu na mbadiliko wa maisha unaotegemea ukweli huo.

Imani katika Mungu ina sehemu nyingi. Ya kwanza ni kuamini kuwa Yeye yupo. Walakini, kuamini tu kuwa Mungu yupo hakutoshi. Vile Yakobo 2:19 inavyoeleza, hata mapepo vile vile wanaamini kuwepo kwa Mungu.

Baada ya kukubali kuwa Mungu yupo, sehemu ya pili ya imani katika Mungu ni kujitolea nafsi. Imani ambayo haizai matendo in Imani iliyokufa, sio imani ya kweli (Yakobo 2:26).

Ingawa, hata ile imani ambayo hututia moyo kutenda haitoshi. Kwa kuwa imani katika Mungu ndio iwe ya kweli, ni lazima tumkubali Yeye jinsi amejidhihirisha katika Maandiko. Haturuhusiwi kuzikubali tabia za Mungu zile tuzipendazo na kukata zile hatuzipendi. Ikiwa hatumkubali Mungu jinsi alivyo, basi tunaiweka imani yetu katika mungu wa uwongo ambaye tumejitengenezea wenyewe. Madhehebu mengi yanafanya haya, lakini dini yeyote ambayo haiamini Biblia ni dini ya kubuni iliyo na mungu wa kubuni. Kwa kuwa imani katika Mungu kwa kwanzia, lazima iwe katika Mungu wa kweli. Kwa mfano, Mungu wa Biblia ni wa Utatu, kwa hivyo imani ya kweli katika Mungu lazima ikubali uungu wake na tabia ya Mwana, na Roho Mtakatifu sawa sawa na Baba.

Kuna mchanganyiko leo hii juu ya asili ya imani. Wengine hufikiria kwamba imani ni "kuamini kile unajua si kweli." Wengi wa "wasioamini kuwa kuna Mungu" huweka imani yao dhidi ya sayansi na Ushahidi. Huwa wanaseam Wakristo wana imani kuwa Mungu yupo lakini wasioamini kuwa kuna Mungu wanayo Ushahidi dhabiti wa kisayansi. Wao husema kuwa Wakristo wana imani, lakini wanasayansi wana maarifa. Ulinganisho huu hauelewi asili ya imani katika Mungu.

Imani kwa Mungu sio kubalio pofu bila kufikiria lisilo na ushahidi wowote, au mbaya zaidi, kinyume na ushahidi. Imani ni kuamini tu. Mkristo anamtegemea Mungu. Mwanasayansi asiyeamini Mungu ana Imani yake katika sayansi. Ikiwa mtu asiyeamini kuweko kwa Mungy anatumia mtindo wa sayansi ili kufumbua dawa na kisha kuichukua dawa hiyo, hivyo ni kuweka imani katika vitendo. Anaamini Habari (data), na anaamini kuwa dawa hiyo itamponya, bali si sumu. Watu wengine wanaweza kuchukua dawa bila ufahamu wowote jinsi dawa hiyo ilivyotengezwa au ni nani aliifumbua. Wengine wanaweza kuitumia dawa hiyo baada ya kufanya uchunguzi wa kina wa kila nyanja ya utatifiti iliyotumika. Mtu mmoja anaweza kuitumia kwa ujasiri mkubwa huku mtu mwingine akiijaribu. Kwa uchanganuzi wa mwisho, mtu yeyote anayeitumia dawa hiyo atakuwa ikiweka imani yake katika dawa. Hatimaye, sio uwezo wa imani ambao unaamua ikiwa dawa itafanya kazi, bali ni matokeo ya dawa. Imani kubwa kwa dawa mbaya haiwezi mponya mtu. Ni madhumuni ya imani, n asio nguvu ya imani ambayo hujalisha. Kutokuwa na uhakika kuhusu dawa nzuri hakuwezi kumzuia obora wake, maadamu ichukuliwe jinsi ilivyoelezewa. Imani si kinyume cha shaka; kwa kweli, shaka inaweza kuwa hata katika moyo wa aliye na imani (ona Marko 9:24). Mtu anaweza kuwa na imani (kuamini na kujitolea) huku wakati huo huo asiwe na uhakika kuhusu jambo au mtu ambeye amejitolea kwake. Mtu wakati mmoja alifafanua shaka kuwa "imani inayotafuta ufahamu."

Wetu wengine wanaweza kumtumainia Mungu kwa sababu inaonekana kuhisika. Huenda walilelewa katika familia ya Ukristo na kufunzwa Biblia kutoka wakati wanaweza kukumbuka. Wamemwona Mungu akifanya kazi maishani mwa watu wengine, na kumwamini Yeye. Wengine huenda walikuja kwa imani baada ya kutadhimini ushahidi wa kuwepo kwa Mungu. Iwe uamuzi wa kumwamini Mungu wa Biblia ni ule wa kuhisi au wa hiari, ni kigezo cha imani ya kweli.

Mkanamungu vile vile anaeza kuja kwa ukanaji Mungu kwa kung'amua au baada ya kutafakari kwa uangalifu. Mwishowe, anakuwa na imani kwamba Mungu hayupo kwa sababu anaamini hisia zake au uchangunizi wake na kujitolea yeye mwenyewe kuishi njia ambayo inaambatana na chenye anaamini. Kunyue na kauli mbiu ya wakanamungu wapya, kila mtu ana kiwango cha Imani-kila mtu anaamini kitu Fulani. Ni vigumu kuishi bila kuamini katika kitu, hata kama ni kutegemea hisia zetu tano. Dhaminio la imani yetu ndio hufanya tofauti.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Imani katika Mungu ni nini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries