settings icon
share icon
Swali

Ina maana gani kumwabudu Bwana kwa roho na kweli?

Jibu


Dhana ya kumwabudu Bwana "kwa roho na kweli" inatoka kwenye mazungumzo ya Yesu na mwanamke kwenye kisima katika Yohana 4: 6-30. Katika mazungumzo, mwanamke alikuwa anazungumzia mahali pa ibada na Yesu, akisema kuwa Wayahudi waliabudu huko Yerusalemu, na Waasamaria waliabudu kwenye Mlima Gerizimu. Yesu alikuwa ameshuhudia kwamba alijua kuhusu wanaume wake wengi, pamoja na ukweli kwamba mwanamme ayeishi naye wakati huo hakuwa mume wake. Hii ilimtia wasiwasi, kwa hiyo alijaribu kupotosha mawazo Yake kutoka kwa maisha yake binafsi na kuzungumzia mambo ya dini. Yesu alikataa kupotoshwa kutoka kwa somo lake kuhusu ibada ya kweli na akalizungumzia kwa kina: " Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu. "(Yohana 4:23).

Somo la jumla juu ya kumwabudu Bwana kwa roho na kweli ni kwamba ibada ya Mungu haifai iwe kwenye sehemu moja ya kijiografia na sio lazima iwe chini ya sheria za Agano la Kale. Kwa kuja kwa Kristo, utengano kati ya Myahudi na Mataifa haukukuwa muhimu tena, wala ukumbi wa hekalu katika ibada. Kwa kuja kwa Kristo, watoto wote wa Mungu walipata fursa sawia kwa Mungu kupitia kwake. Kuabudu ikawa suala la moyo, sio vitendo vya nje, na kuongozwa na ukweli badala ya sherehe.

Katika Kumbukumbu la Torati 6: 5, Musa anawaelezea Waisraeli jinsi wanapaswa kumpenda Mungu wao: "Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote na kwa nafsi yako yote na kwa uwezo wako wote". Kumwabudu kwetu kunachochewa na upendo wetu kwake ; kama tunavyopenda, basi tunamwabudu. Kwa sababu dhana ya "nguvu" kwa Kiebrania linaonyesha kwa ukamilifu, Yesu aliongeza maana ya neno hili kuwa "akili" na "nguvu" (Marko 12:30; Luka 10:27). Kumwabudu Mungu kwa roho na kweli kunahusisha kumpenda kwa moyo, roho, akili na nguvu.

Kuabudu kweli lazima iwe "kwa roho," yaani, kushirikisha moyo wote. Pasipokuwa kuna shauku halisi kwa Mungu, basi hamna ibada katika roho. Wakati huo huo, ibada lazima iwe "kwa kweli," ambayo ni sahihi. Isipokuwa tunajua Mungu tunayeabudu, hakuna ibada kwa kweli. Yote ni muhimu katika ibada ya kuridhisha na ya heshima kwa Mungu. Roho bila ukweli husababisha hisia isiyo ya kina ambayo inaweza kulinganishwa na kuasi. Mara baada ya hisia kukamilika, wakati shauku inapotea, pia ibada inapotea. Ukweli bila roho unaweza kusababisha ushujaa kavu, usio na shauku ambayo sio halali. Mchanganyiko bora wa mambo yote mawili ya ibada husababisha shukrani ya furaha kwa Mungu iliyochochewa na Maandiko.Tunavyojua zaidi kuhusu Mungu, tunamthamini zaidi. Tunaposhukuru zaidi, ihaina budi kuwa na ibada kwa kina. Tunapozidi kuabudu, Mungu hutukuzwa zaidi.

Mchanganyiko huu wa roho na kweli katika ibada umeelezewa kwa kina na Jonathan Edwards, mchungaji wa karne ya 18 wa Marekani na mwanateolojia. Alisema, "Ni lazima nidhani nafsi yangu kwa njia ya wajibu wangu kuinua [hisia] za wasikilizaji wangu kwa kadiri iwezekanavyo , isipokuwa wanaathiriwa na chochote isipokuwa ukweli." Edwards alitambua kwamba ni ukweli pekee unao shawishi vizuri hisia kwa njia inayoleta heshima kwa Mungu. Ukweli wa Mungu, kuwa na thamani isiyo na kipimo, unastahiki shauku isiyo na mwisho.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ina maana gani kumwabudu Bwana kwa roho na kweli?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries