settings icon
share icon
Swali

Kwa nini Wakristo hufanya ibada siku ya Jumapili?

Jibu


Wakristo wengi kawaida huabudu Jumapili. Ibada ya Jumapili kwa kiwango fulani inahusishwa na mafudisho ya Sabato, maoni kwamba siku moja ya juma inapaswa kutengwa kwa utunzaji na ibada ya kidini , kama inavyotakikana katika sheria za Agano la Kale kuhusu Sabato (20:8, 31:12–18).Kutoka 20:8, 31:12–18). Maoni haya hudai kwamba mwanadamu anapaswa kujiepusha na kazi zote isipokuwa ile ambayo ni muhimu kwa ustawi wa familia na jamii. Tafsiri hii ya sheria inadai kwamba ni katika siku ya Sabato halisi tu, ambayo ni siku ya saba ya juma (Jumamosi), ambapo mahitaji ya sharia yanaweza kutimizwa.

Wafuasi wa Semi-Sabataria, mapema katika karne ya nne Kabla ya Kristo, waliamini kama vile Wasabato walivyoamini, isipokuwa walihamisha matakwa yake kutoka Jumamosi kwenda Jumapili, siku ya kwanza ya juma (siku ambayo Kristo alifufuka kutoka kwa wafu). Wanatheologia wa kipindi hicho haswa katika Kanisa la Mashariki, walikuwa wanafundisha utambulisho halisi wa Sabato ya Kiyahudi (Jumamosi) na Jumapili ya Kikristo.

Interestingly, a legend recounted in the so-called Apocalypse of Peter dates back to the 2nd century AD and is generally accepted as a false writing, transfers to Sunday all of the requirements of Sabbath worship. A man named Albertus Magnus added momentum to this growing movement by suggesting semi-Sabbatarianism be divided into two parts: the moral command to observe a day of rest after laboring the previous six days, and the ceremonial symbol that applied only to the Jews in a literal sense. Thomas Aquinas elevated this proposal to the status of official Roman Catholic doctrine, which in time also gained favor with many Reformed theologians.

Cha kuvutia, hadithi inayosimuliwa katika Ufunuo wa Petro ya mnamo karne ya pili kabla ya Kristo , ambayo inakubalika kama mafundisho ya uongo, imehamisha matakwa yote ya ibada Sabato na kuyaweka katika siku ya Jumapili. Mtu mmoja aliyeitwa Albertus Magnus aliongeza maoni yake katika harakato hii inayokua kwa kupendeza kwamba Semi-Sabataabataria igawanywe mara mbili: amri ya maadili ya kutenga siku ya mapumziko baada ya kufanya kazi siku sita zilizopita, na ishara ya sherehe ambayo ilitumika kwa Wayahudi tu kwa maana halisi. Thomas Aquinas aliinua pendekezo hili kwa hadhi ya mafundisho rasmi ya Katoliki ya Kirumi, amabayo baadaye ilipata kibali kwa Wanatheolojia wengi wa Mageuzi.

Maandiko hayataji mikusanyiko yoyote ya Sabato (Jummosi) ya waumini kwa ushirika au ibada. Hata hivyo, kuna vifungu wazi ambavyo vinataja siku ya kwanza ya juma, Jumapili. Kwa mfano, Matendo ya Mitume 20:7 inasema kwamba, "siku ya kwanza ya juma tulikusanyika ilikuumega mkate." Paulo pia anawasihi waumini wa Korintho "Siku ya kwanza ya juma kila mtu kwenu na aweke akiba kwake, kwa kadiri ya kufanikiwa kwake, (1 Wakorintho 16:2). Kwa kuwa Paulo anataja dhabihu hii kama "huduma" katika 2 Wakorintho 9:12, mchango huu unaweza kuwa ulihusishwa na ibada ya Jumapili ya mkutano wa Kikristo. Kihistoria, siku ya Jumapili na wala sio Jumamosi ilikuwa ni siku ya kawaida ya mkutano wa Wakristo kanisani, na ilikuwa desturi tangu karne ya kwanza.

Wakristo hufanya ibada siku ya Jumapili kwa kusherekea ufufuo wa Yesu Kristo. Ni muhimu kukumbuka kwamba ibada ya Jumapili haijaamriwa katika Biblia, na Jumapili hajachukua nafasi ya Jumamosi na kuwa Sabato ya Kikristo. Ijapokuwa Agano Jipya linaelezea Wakristo wakikusanyika na kufanya ibada siku ya Jumapili, hamna mahali popote inasema kwamba Jumapili imechukua nafasi ya Jumamosi kama Sabato. Jambo la maana katika haya yote ni kwamba hatupaswi kuzuia ibada yetu kwa siku fulani ya juma. Tunapaswa kupumzika kwake Bwana kila siku. Tunapaswa kumwabudu Bwana kila siku.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kwa nini Wakristo hufanya ibada siku ya Jumapili?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries