settings icon
share icon
Swali

Je, ni makosa kuhusudu mtu?

Jibu


Katika chumba kilicho jaa watu, yuko hapo, mtu pekee unayemwona ni mtu wa ndoto yako. Moyo wako unapiga kwa kasi, viganja vya mikono vinatoka jasho, mdomo unakauka, na wakati huo huo unatamani na pia kuogopa kukutana naye. Umehusudu mtu huyo Je! hisia kama hizo ni mbaya? Je! Ni vizuri kuhusudu mtu?

Kuhusudu mtu, au kupumbazika inaweza kuwa yenye mhemko, lakini hazidumu kwa muda mrefu. Tunanza kutamani mtu fulani katika shule za chekechea, na tamaa hio inaweza kuendelea mara kwa mara katika utu uzima. Watu wengi wanatawaliwa na hisia hizo ilhali hakuna anayeweza kueleza kikamilifu kwa nini tunampendelea mtu fulani huku tukiwapuuza wengine. Homoni zinazosababisha hisia za kimapenzi, kuvutiwa na jinsi mtu anavyoonekana, na jinsi mtu anavyonukia, anavyocheka, au kutabasamu vyote vinawezachangia kuhusudu mtu. Hisia zinazoambatana na husudu zinaweza kulemea mtu.

Husudu yapaswa kutofautishwa na upendo wa kweli. Husudu inaweza kuanza kama vile upendo huanza, lakini upendo ni zaidi ya kuvutiwa na jinsi mtu anavyoonekana na ni zaidi ya hisia na huhusisha hatua ya utumishi wa dhabihu. Mungu hakumtuma Mwanawe afe kwa ajili ya husudu; ilikuwa ni kwa sababu ya upendo wa kweli (Yohana 3:16; 10:11; 1 Yohana 4:9). Husudu ni mwitikio wa hisia kwa kitu tunachoona kinavutia kuhusu mtu mwingine, ilhali upendo hujitolea thabiti kwa ustawi wa mtu huyo (1 Wakorintho 13:4-8).

Tunaweza kuhusudu watu ambao hatuwajui, kama vile watu mashuhuri, watu maarufu, au walimu. Mtandao umeanzisha aina mpya ya kuhusudu, mahusiano ya mtandaoni yanaongezaka, na mawasiliano yetu pekee na watu hao ni kupitia scrini. Miaka ya ujana huathirika kwa upesi kwa husudu. Homoni hubadilika-badilika, na miili iko katika hatua mbalimbali za ukomavu. Mara nyingi hatufahamu tofauti kati ya upendo na husudu, hasa tukiwa wachanga, kwa hivyo tunakuwa katika hatari ya kuingia katika mahaba au uhusiano wa kimapenzi ambao huacha majeraha ya muda mrefu.

Kuwa na husudu sio makosa maadamu hatujiruhusu kufanya maamuzi ya dhambi kwa sababu ya husudu. Husudu inawezakuwa hali isiyoepukika katika kuwa mwanadamu, kwa hivyo tunapaswa kuitambua jinsi ilivyo na sio kufanya maamuzi juu ya hisia hizo. Ni lazima tujikinge dhidi ya kuruhusu husudu sisizo na hatia kugeuka kuwa mawazo ya ngono. Yesu alisema, “Lakini mimi nawaambia kwamba, yeyote amtazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake” (Mathayo 5:28). Tunapowaza juu ya kutenda kitu ambacho Mungu anakiita dhambi, tayari tunafanya dhambi mioyoni mwetu (Wakolosai 3:5; 1 Wakorintho 6:18; Warumi 1:26-27). Kudhibiti husudu ni muhimu: “Kama vile mji ambao kuta zake zimebomoka ndivyo alivyo mtuambaye hawezi kujitawala mwenyewe” (Mithali 25:28).

Biblia inatupa mfano wa mtu ambaye alitawaliwa na husudu sana kwamba hatimaye kulimgharimu maisha yake (Waamuzi 14:1-2). Samsoni alichaguliwa na Mungu na kutengwa kwa ajili ya huduma (Waamuzi 13:2-5). Hata hivyo, alipoteza mambo mengi ambayo Mungu alitaka kufanya kupitia yeye kwa sababu aliruhusu husudu yake iamue matendo yake. Tukichunguza makosa aliyofanya, tuanweza kuepuka mitego hiyohiyo. Kwanza kabisa, Samsoni alizoea kufanya karamu na makafiri. Alitembelea maeneo ambayo hakupaswa kuenda kamwe. Kosa lake la pili lilikuwa kutotambua udhaifu wake mwenyewe. Alivutiwa na wanawake wadanganyifu, wasiomcha Mungu na, badala ya kujilinda (Warumi 13:14), alijiingiza katika udhaifu huo. Tatu, hakujifunza kutokana na makosa yake (Waamuzi 16:1-4). Alikosea kwa kuchukulia husudu iliyoongozwa na tamaa kuwa upendo unaomheshimu Mungu mara na tena, na hii ikamgharimu kila kitu (Waamuzi 16:21, 29-30). Tunaweza kujiepusha na maumivu mengi ikiwa tutaepuka makosa ya Samsoni.

Kama Wakristo, tunapaswa kufanya kila kitu kwa utukufu wa Mungu (1 Wakorintho 10:31). Tunapopambana na husudu, tunapaswa kufanya hivyo kwa utukufu wa Mungu. Tunaanza kwa kuwa waaminifu kwa Bwana kuhusu hisia zetu, kama watunga-zaburi walivyokuwa (Zaburi 6:6; 39:9). Tunamwomba atusaidie kuweka mawazo yetu kuwa safi na matendo yetu yakimpendeza (Zaburi 19:14). Tunaweza pia kusali kwa ajili ya yule mtu ambaye ametuvutia. Omba kwamba atamtafuta Bwana na kwamba Mungu atatimiza kusudi Lake ndani ya mtu huyo. Ikiwa husudu hiyo ni kwa mtu ambaye kuna uwezekano atakuwa mwenzi wa ndoa, tunaweza kumwomba Bwana kwa ujasiri nafasi za kumjua vizuri zaidi. Bila shaka, ni lazima kila mara tutoe maombi yetu katika roho ya maneno ya Yesu “Lakini si kama nipendavyo, bali mapenzi yako yatendeke” (Luka 22:42).

Mungu anataka kuhusika katika kila sehemu ya maisha yetu, hata katika husudu yetu. Anataka tuwe walinzi walio macho juu ya mioyo yetu ili husudu isiwe sanamu (Mithali 4:23). Tukijikuta tunafikiria mchana na usiku kuhusu mtu mmoja, huenda tumevuka mipaka kutoka kwa husudu ya kawaida hadi kwenye tamaa isiofaa. Kutafuta nyakati za karibu za ushirika na Mungu kunaweza kusaidia kuwa na mtazamo sahihi wa husudu. Ingawa husudu inaweza kuonekana kuwa jambo la ajabu, hakuna mtu anayeweza kujaza pengo mioyoni mwetu kama vile Mungu. Msisimko wa husudu inatukumbusha kwamba mioyo yetu ina uwezo mkubwa wa upendo, furaha, msisimko, na matumaini. Yote yataridhika kabisa siku moja tutakapokuwa milele katika uwepo wa Bwana (Zaburi 16:11; 23:6; Ufunuo 21:2).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, ni makosa kuhusudu mtu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries