settings icon
share icon
Swali

Ni nini kitakachotokea katika hukumu ya mwisho?

Jibu


Kitu cha kwanza kuelewa kuhusu hukumu ya mwisho ni kwamba haiwezi kuepukwa. Haijalishi jinsi tunaweza kutafsiri unabii unaohusu wakati wa mwisho, tunaambiwa kuwa "Basi kama vile kila mtu hufa mara moja tu, kisha husimama mbeley ya hukumu ya Mungu" (Waebrania 9:27). Sisi wote tuna uteuzi wa kiungu na Muumba wetu. Mtume Yohana aliandika maelezo fulani kuhusu hukumu ya mwisho:

"Kisha, nikaona kiti cha enzi kikubwa cheupe, na youle aketiye juu yake. Dunia na mbingu vikatoweka mbele ya macho yake, na havikuonekana tena. Kisha nikwaona watu wakubwa na wadogo, wamesimama mbele ya kiti cha enzi, na vitabu vikafunguliwa. Halafu kitabu kingine, yaani kitabu cha uhai, kikafunguliwa pia. Wafu wakahukumiwa kadiri ya matendo yao, kama ilivyoandikwa ndani ya vitabu hivyo. Bahari ikawatoa nje wafu waliokuwa ndani yake; kifo na Kuzimu vikawatoa nje wafu waliokuwa ndani yao. Kila mmoja akahukumiwa kufuatana na matendo yake. Kisha kifo na Kuzimu vikatupwa ndani ya ziwa la moto. Ziwa hili la moto ndiocho kifo cha pili. Mtu yeyote ambaye jina lake halikupatikan limeandikiwa katika kitabu cha uhai, aliptupwa katika ziwa la moto "(Ufunuo 20: 11-15).

Kifungu hiki cha ajabu kinatueleza hukumu ya mwisho-mwisho wa historia ya mwanadamu na mwanzo wa hali ya milele. Tunaweza kuwa na hakika ya hili: hakuna makosa yatakayofanywa katika kusikizwa kwa kesi yetu kwa sababu tutahukumiwa na Mungu mkamilifu (Mathayo 5:48, 1 Yohana 1: 5). Hii itajidhihirisha katika ushahidi mwingi ulio wa kuaminika. Kwanza, Mungu atakuwa wa huru na haki (Mdo. 10:34; Wagalatia 3:28). Pili, Mungu hawezi kudanganywa (Wagalatia 6: 7). Tatu, Mungu hawezi kudhibidhiwa na uongo wowote, usababu au uongo (Luka 14: 16-24).

Kama Mungu Mwana, Yesu Kristo atakuwa hakimu (Yohana 5:22). Wote wasioamini watahukumiwa na Kristo katika "kiti kikuu cheupe cha enzi," nao wataadhibiwa kulingana na matendo yao. Biblia ii wazi sana kwamba wasioamini wanajihifadhia ghadhabu juu yao wenyewe (Warumi 2: 5) na kwamba Mungu "atalipa kila mmoja kulingana na matendo yake" (Warumi 2: 6). (Waumini watahukumiwa pia, kwa hukumu tofauti inayoitwa "kiti cha hukumu cha Kristo" (Warumi 14:10), lakini tangu haki ya Kristo imetiwa ndani yetu na majina yetu kuandikwa katika Kitabu cha Uzima, tutapata thawabu , sio adhabu, kwa mujibu wa matendo yetu.) Katika hukumu ya mwisho hatima ya wasiookoka itakuwa mikononi mwa Mungu mwenye kujua mambo yote ambaye atahukumu kila mtu kulingana na hali ya nafsi yake.

Kwa sasa, hatma yetu iko katika mikono yetu wenyewe. Mwisho wa safari ya nafsi yetu itakuwa aidha katika mbinguni ya milele au katika kuzimu ya milele (Mathayo 25:46). Tunapaswa kuchagua mahali ambapo tutakuwa kwa kukubali au kukataa dhabihu ya Kristo kwa niaba yetu, na lazima tufanyie uchaguzi huo kabla ya maisha yetu ya kimwili katika dunia hii kufika mwisho. Baada ya kifo, hakuna chaguo tena, na hatma yetu ni kusimama mbele ya kiti cha enzi cha Mungu, ambapo kila kitu kitakuwa wazi na kuekwa peupe mbele zake (Waebrania 4:13). Warumi 2: 6 inasema kwamba Mungu "atalipa kila mtu kulingana na matendo yake."

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ni nini kitakachotokea katika hukumu ya mwisho?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries