settings icon
share icon
Swali

Je, huduma ya Kikristo ni nini?

Jibu


"Huduma" inatoka kwa neno ya Kiyunani diakoneo, lianalomaanisha "kutumikia" au douleuo,kumaanisha "kutumikia kama vile mtumwa." Katika Agano Jipya, huduma inaonekana kuwa utumishi kwa Mungu na watu wengine katika jina Lake. Yesu alitoa mfano wa huduma ya Kikristo- Alikuja, sio kutumikiwa lakini kutumika(angalia Mathayo 20:28; Marko 10:45; Yohana 13:1-17).

Mkristo anapaswa kuhudumu kwa kukidhi mahitaji ya watu kwa upendo na unyenyekevu kwa niaba ya Kristo (Ona Mathayo 20:26; Marko 10:43; Yohana 2: 5,9; Matendo 6: 3; Warumi 1: 1; Wagalatia 1:10; Wakolosai 4:12). Wakristo wanapaswa kuhudumia wengine kwa kujitolea kwao kwa Kristo na upendo wao kwa wengine, iwe hao watu wengine ni wameokoka au hawajaokoka. Huduma kwa wengine inapaswa kuwa na ubaguzi, mapendeleo na isiyo na masharti, kila wakati inatafuta kusaidia wengine jinsi na namna Yesu angefanya.

Huduma hii leoo imechukua maana ya taaluma tunapowaita wachungaji "wajumbe" kwa utumishi wa wakati wote. Wachungaji hutumia maisha yao katika huduma, huwa wanahudumia wengine, na wanaweza kuteuliwa kama wahudumu, lakini sio wachungaji tu ambao wanapaswa kushiriki katika huduma. Tangu makanisa ya kwanza ya Agano Jipya hadi makanisa ya siku hizi, kila Mkristo anapaswa kuwa katika huduma ya kusaidia wengine (angalia Warumi 12: 3-8, 10-13; 2 Timotheo 2: 24-26).

Kiini cha huduma kinaonekana kutanguliza huduma ya mambo ya kiroho, sio tu vitu vya kimwili. Huduma lazima itilie mkazo kushiriki Injili ya Yesu Kristo na wengine ili waweze kumjua na kumpokea kama Mwokozi wao kibinafsi, na kuendelea kumhisi kama Bwana wa maisha yao, na kwendelea kumjua zaidi Kristo kama kiini cha Maisha yao (angalia Yohana 1:12; Wakolosai 2: 6-7; Wagalatia 2:20; Wafilipi 3: 8-10). Huduma inaweza, na inapaswa kujumuisha kuhudumia mahitaji ya kimwili, kihisia, kiakili, kitaluuma, na kifedha kwa wengine. Yesu alifanya hivyo, hivyo basi na sisi pia tunapaswa kufanya hivyo!

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, huduma ya Kikristo ni nini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries