settings icon
share icon
Swali

Je, baadhi ya mifano ya hoja ya mduara katika masuala ambayo Wakristo hubishana ni gani?

Jibu


Kwa ufupi, hoja ya mduara ni jaribio la kuunga mkono kauli au madai kwa kuirudia rudia kwa maneno tofauti au yenye nguvu zaidi. Hoja ya mduara ni mantiki ya uwongo, na inajitokeza katika nyanja nyingi ambapo dhana na dhamira hufanywa. Mfano wa kawaida ni utia miadi wa wanamageuko wa visukuku kulingana na tabaka za miamba zinamopatikana, na wakati huo huo kukadria tarehe ya tabaka kulingana na “kielezo cha kisukuku” kilichomo. Kukadria umri wa mwamba kwa msingi wa kisukuku kilichomo itawezekana tu ikiwa itadhaniwa kwamba mageuko kweli yapo. Kama vile mwanasayansi mmoja wa paleontilojia (elimu ya visukuku) alivyokubali, “kwa wanabaolojia wengi, sababu yenye uzito zaidi ya kukubali nadharia ya mageuzi na kukubali kwao nadharia fulani inayohusisha hilo” (David G. Kitts, “Paleontology and Evolutionary Theory,” in Evolution, September 1974, p. 466).

Wakristo pia, wakati mwingine hutumia hoja ya mduara. Kauli “Ninaamini kwamba Biblia ni ya kweli kwa sababu Biblia inasema ni kweli” yanaweza kuwa na maana kamili kwa muumini-ni kauli yenye msingi katika imani- lakini katika hoja ya kimantiki inaweza chukuliwa kuwa hoja ya mduara. Madai yanatumia madai yenyewe kuthibitisha madai yake. Wakosoaji na wahakiki wa Ukristo mara nyingi hudai kwamba Wakristo wanatumia hoja ya mduara kutetea imani ya kibiblia. Uhakiki kama huo mara nyingi si wa kweli; hata hivyo, tunapaswa kuwa waangalifu katika kutumia njia zinazofaa katika kuunga mkono ukweli.

Mfano mwingine wa hoja ya mduara unahusiana na kuwapo kwa Mungu. Baadhi ya Wakristo wamebishina kwamba Mungu yuko kwa sababu Biblia inasema Yuko- na kwa kuwa Mungu aliandika Biblia, lazima iwe kweli. Kuhoji namna huwa kuna matatizo yanayotokana na mtazamo wa kimantiki kwa vile unaweka msingi wake katika imani ya kuwepo kwa Mungu kwa imani ya Kikristo kwamba Biblia inatoka kwa Mungu.

Biblia inachukulia kuwa Mungu yupo na inadai hilo kuwa ukweli (Mwanzo 1:1; Zaburi 33:4). Kauli hizo lazima zichukiliwe kwa imani, ambayo haifai kushangaza mtu yeyote. Biblia inasema kuwa imani inahitajika. Pasipo imani, haiwezekani kumpendaza Mungu, na imani ndio msingi wa maisha ya Kikristo (Waebrania 11:6; Warumi 1:17).

Wakati huo huo, kuna joha nyingi thabiti, zenye mantiki za kuunda jambo la kuunga imani ya Kikristo. Kuwepo kwa Mungu kunaweza kubainishwa kutokana na kuwepo kwa uumbaji (Zaburi 19:1), na ukweli wa biblia kupitia ushahidi wa kihistoria (Yohana 10:37-38). Hoja ya mduara haihitajiki. Tunaweza kutumia mchanganyiko wa data ya Kibilia, kuwaza kimantiki, kifalsafa, na ushahidi wa kihistoria na kisayansi ili kuwasilisha kesi bora zaidi kuhusu mafundisho ya Kikristo. Waandishi wengi wa Kikristo wameandika tetezi za imani, ikiwa ni pamoja na C. S. Lewis, Josh McDowell, Lee Strobel, Norman Geisler, na wengineo.

Biblia inawapa Wakristo changamoto kuwa tayari kuelezea tumaini tulilo nalo. “Bali mtakaseni Kristo kuwa Bwana mioyoni mwenu. Siku zote mwe tayari kumjibu mtu yeyote atakayewauliza kuhusu sababu ya tumaini lililomo ndani yenu. Lakini fanyeni hivyo kwa upole na kwa heshima, mkizitunza dhamiri zenu ziwe safi, ili wale wasemao mabaya dhidi ya mwenendo wenu mzuri katika Kristo waaibike kwa ajili ya masingizio yao” (1 Petro 3:15-16).

Hatimaye, Biblia lazima ukubalike kwa imani, na ndilo Neno la Mungu pekee ambalo lina uwezo wa kubadilisha maisha (Yohana 17:17). Je, mtu anaweza kuletwa karibu na kweli kupitia hoja zenye mantiki? Naam. Mtu anaweza kukubali ukweli wa Ukristo bila imani? La.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, baadhi ya mifano ya hoja ya mduara katika masuala ambayo Wakristo hubishana ni gani?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries