settings icon
share icon
Swali

Ni hoja gani ya maadili ya uwepo wa Mungu?

Jibu


Hoja ya maadili huanza na ukweli kwamba watu wote hutambua kanuni fulani za maadili (kwamba baadhi ya mambo ni sahihi, na mengine ambayo sio sahihi). Kila wakati tunapingana kuhusu mazuri na mabaya, tunakata rufaa juu ya sheria ya juu ambayo tunadhani kila mtu anajua, anashikilia, na hakuna uhuru wa kubadili. Haki na mbaya vinaashiria kiwango cha juu au sheria, na sheria inahitaji mtoa sheria. Kwa sababu sheria ya maadili ni kuu kuliko ubinadamu, sheria hii yote inahitaji mta sheria wa ulimwengu wote ambaye ni Mungu.

Kwa kuunga mkono hoja ya maadili, tunaona kwamba hata kabila za mbali zaidi ambazo hazina ustaarabu wowote huwa na kanuni za maadili sawa na za watu wengine. Ingawa kuna tofauti hakika katika masuala ya kiraia, sifa kama vile ujasiri na uaminifu na maovu kama vile tamaa na hofu huwa katika ulimwengu kote. Ikiwa binadamu angekosa kuchukua jukumu la kanuni hio, ingekuwa tofauti kama vile kila kitu kinginecho ambacho binadamu amezindua. Zaidi ya hayo, si tu rekodi ya kile wanadamu wanavyofanya — mara chache watu huishi kulingana na kanuni zao za maadili. Je, tunapata wapi mawazo haya ya kile kinachofaa kufanyika? Warumi 2: 14-15 inasema kwamba sheria ya maadili (au dhamiri) inatoka kwa mtoa sheria mkuu, ambaye ni kuu kuliko binadamu. Ikiwa hii ni kweli, basi tunatarajia kupata hasa yale tuliyoyafuata. Mtetezi huyu ni Mungu.

Kuelezea kwa kina, dini ya kuasi Mungu haitoi msingi wa maadili, hakuna tumaini, na hakuna maana kwa maisha. Ingawa hoja hii haipingi kuasi Mungu yenyewe, ikiwa utekelezaji wa kimantiki wa mfumo wa imani hauwezi kuzingatia kile tunachojua kuwa ni kweli, inapaswa kuachwa. Bila Mungu hakungekuwa na msingi wa maadili, hakungekuwa na maisha, na hakungekuwa na sababu ya kuishi. Hata hivyo, mambo haya yote yapo, na hivyo Mungu yupo pia. Hivyo basi, hoja ya maadili ya kuwepo kwa Mungu.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ni hoja gani ya maadili ya uwepo wa Mungu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries