settings icon
share icon
Swali

Hoja ya kimaumbile ya uwepo wa Mungu ni nini?

Jibu


Hoja ya kimaumbile ya uwepo wa Mungu ni hoja inayojaribu kuthibitisha uwepo wa Mungu kwa kudai kwamba mantiki, maadili na sayansi yanategemea mtazamo wa theolojia na kwamba tabia ya kipekee ya Mungu ndiyo chanzo cha mantiki na maadili. Hoja ya kimaumbile ya uwepo wa Mungu inadai kwamba bila uwepo wa Mungu haiwezekani kuthibitisha chochote kwa sababu, katika ulimwengu wa wasioamiani, huwezi kuhalalisha au kuelezea sheria za kawaida.

Sababu zinazohusiana na mantiki zinategemea sheria za mantiki. Lakini kwa nini sheria za mantiki zinatumika? Kwa Mkristo na waumini wengine, kuna kiwango kinachovuka upeo wa kawaida wa kufikiria. Kwa kuwa sheria za mantiki zinapunguzwa kuwa vitu vya kimwili, zinakosa sifa zao za kisheria. Lakini sheria za mantiki hazitengenezwi na vitu vya kimwili, zinatumika kwa kawaida na wakati wote. Sheria za mantiki zinategemea tabia ya Mungu isiyobadilika na ni muhimu kwa ajili ya kufikiria. Uthabiti, ukuu, upeo na Mungu kutomiliki vitu vya kimwili ni msingi wa sheria za mantiki. Kwa hivyo, kufikiri kwa kutumia mantiki haingewezekana bila Mungu wa Kibiblia.

Mpinga Kristo anaweza kujibu, “Naweza kutumia sheria za mantiki, nami ni mpinga Kristo.” Lakini hoja hii ni batili. Kufikiri kwa mantiki kunahitaji uwepo wa Mungu mwenye ukuu na asiye na vitu vya kimwili, si kwa sababu ya imani ya mtu kwake. Mpinga Kristo anaweza kufikiria, lakini katika mtazamo wake wa ulimwengu tu, kufikiri kwake hakuwezi fafanuliwa kwa njia ya mantiki.

Ikiwa sheria za mantiki ni madai tu yaliyotengenezwa na binadamu, basi tamaduni tofauti zingeweza kukumbatia sheria tofauti za mantiki. Kwa sababu hii, sheria za mantiki hazingekuwa sheria za ulimwengu wote. Mjadala wa kimantiki haungewezekana ikiwa sheria za mantiki zingekuwa za kawaida, kwa sababu pande zote mbili zinaweza kupitisha sheria tofauti za mantiki. Kila upande ungekuwa sahihi kulingana na viwango vyake vya kiholela.

Ikiwa mpinga Kristo anasema kuwa sheria za mantiki ni matokeo tu ya fikra za ubongo, basi sheria za mantiki haziwezi kuchukuliwa kuwa za ulimwengu wote. Kile kinachotokea ndani ya akili yako hakiwezi kuchukuliwa kama sheria, kwa sababu hakiwezi kulingana na kile kinachotokea katika akili ya mtu mwingine. Kwa maneno mengine, hatuwezi kudai kuwa mwingiliano wa mantiki hauwezi kutokea katika mazingira mengine mbali na wachunguzi.

Jibu moja la kawaida linalotumika ni “Tunaweza kutumia sheria za mantiki kwa sababu zimeonekana kufanya kazi.” Hata hivyo, hii ni kukosa lengo. Wote tunakubaliana kwamba sheria za mantiki zinafanya kazi, lakini zinafanya kazi kwa sababu ni kweli. Swali halisi ni, jinsi gani mpinga Kristo anaweza kuelezea viwango vya upeo wa mantiki kama sheria za mantiki? Kwa nini ulimwengu unahisi kulazimishwa kuzingatia sheria za kimwili? Zaidi ya hayo, kurejelea nyuma ili kufanya uchambuzi kuhusu jinsi vitu vitakavyokuwa katika siku zijazo- kutokana na mtazamo wa kimada- ni mzunguko. Kwa kweli, siku za nyuma, vitu vimefuata utaratibu wa kawaida. Lakini mtu anawezaje kujua kuwa utaratibu huo utaendelea katika siku zijazo isipokuwa kama tayari mtu amekubali kuwa siku zijazo zitajionyesha kama siku za nyuma (yaani, utaratibu)? Kutumia uzoefu wa mtu wa siku za nyuma kuelezea msingi wa matarajio yake ya siku zijazo ni kudai usawa wa mantiki. Kwa hiyo, wakati mtu asiyemwamini Mungu anadai kuamini kuwa kutakuwa na utaratibu katika siku zijazo kwa kuwa kulikuwa na utaratibu siku za nyuma, anajaribu kuthibitisha utaratibu kwa kudai kuwepo kufanana, ambao ni mjadala usio na mwelekeo.

Kwa kumalizia, mjadala kuhusu kuwepo kwa Mungu unadai kwamba kumpinga Mungu ni kujikana mwenyewe kwa sababu mwenye kumpinga lazima afikirie kinyume cha kile anachotaka kudhibitisha ili aweze kuthibitisha chochote. Inadai kwamba mantiki na hoja zinaweza kueleweka tu ndani ya mfumo wa wasioamini Mungu. Wanaokana uwepo wa Mungu wanatumia sheria za mantiki, lakini hawana msingi wa kuegemeza sababu zao ndani ya mtazamo wao wenyewe.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Hoja ya kimaumbile ya uwepo wa Mungu ni nini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries