settings icon
share icon
Swali

Je, hoja ya kutoka kwa ukafiri ni nini?

Jibu


Hoja ya kutoka ukafiri ni kwamba kuwepo kwa makafiri wa kweli kunathibitisha kwamba Mungu hawezi kuwepo. Kunapendekeza kwamba kuna watu wengi ambao wako tayari kuamini Mungu, ikiwa wangepewa ushahidi wa kutosha. Ukweli kwamba watu hawa hawajapewa uthibitisho wa unaofaa inaoenekana kuwa uthibitishwo kwamba hakuna Mungu mwenye upendo wa kutoa uthibitisho huo au kuwa uthibitisho huo haupo kabisa.

Kwa ufupi, hoja ya kutoka ukafiri inadai kwamba, kama Mungu halisi, basi angejitambulisha kwa uwazi sana hivi kwamba yeyote aliyekuwa tayari kwa dhati angeamini tayari.

Kuna dhana mbili za msingi zinazounga mkono hoja ya kutoka kwa ukafiri; zote mbili ni za uwongo. Ya kwanza ni kwamba kitu kama kafiri mwenye shabaha, wa dhati na aliyetayari. Pili ni kwamba Mungu ameshindwa kuotoa uthibitisho “wa kutosha” ili kungoza kwenye ukweli. Pia kuna msingi wa tatu, amabao umefichwa kwa kiasi fulani katika hoja, kunao uhusiana na ikiwa Mungu anapaswa kufikia kiwango fulani cha ufunuo. Wazo la dai hili ni dhaifu sana, kiasi kwamba wazo hilo halitumiki sana katika mada yoyote.

Maelezo ya wazi ya ni kwa nini hoja kutoka ukafiri ni ya uongo yanatoka moja kwa moja kutoka kwa Maandiko yenyewe. Kitabu cha Warumi kinashughulikia hoja hii moja kwa moja, ikitatua hoja zilizo na kasoro bila shaka:

Kwa maana ghadhabu ya Mungu imedhihirishwa kutoka mbinguni juu ya uasi wote na uovu wa wanadamu waipingao kweli kwa uovu.Kwa kuwa mambo ya Mungu yanayojulikana yamekuwa dhahiri ndani yao, kwa maana Mungu aliwadhihirishia. Kwa sababu mambo yake yasiyoonekana tangu kuumbwa ulimwengu yanaonekana, na kufahamika kwa kazi zake; yaani, uweza wake wa milele na Uungu wake; hata wasiwe na udhuru;

kwa sababu, walipomjua Mungu hawakumtukuza kama ndiye Mungu wala kumshukuru; bali walipotea katika uzushi wao, na mioyo yao yenye ujinga ikatiwa giza. Wakijinena kuwa wenye hekima walipumbazika;wakaubadili utukufu wa Mungu asiye na uharibifu kwa mfano wa sura ya binadamu aliye na uharibifu, na ya ndege, na ya wanyama, na ya vitambaavyo.

Kwa ajili ya hayo Mungu aliwaacha katika tamaa za mioyo yao, waufuate uchafu, hata wakavunjiana heshima miili yao.

Kwa maana waliibadili kweli ya Mungu kuwa uongo, wakakisujudia kiumbe na kukiabudu badala ya Muumba anayehimidiwa milele. Amina.

– Warumi 1:18–25 (msisitizo umeongezwa)

Kwa ufupi, kutoamini hakutegemei uwazi au kutojua bali katika kukataa kufuata ukweli. Kwa kweli, Biblia inaonyesha kuwa kinachofanyika ni kukandamiza ukweli. Wale ambao hawamwamini Mungu wanaweza kuwa “wasema ukweli” kwa maana kuwa hawamwamini Mungu kabisa. Lakini uthibitisho ambao Mungu ameweka katika uzoefu wa mwanadamu unatosha zaidi kwa kila mtu kufuata kwa hitimisho ya kimantiki. Hata kafiri wa kweli, wakati fulani anakataa kwa udhalili na kimakusudi au kupuuza kiwango fulani cha ushahidi wa Mungu. Wanapuuza au kuchagua kutofuata “vitu vinavyoonekana waziwazi, ikitambuliwa kutoka yale aliyoyafanya” Warumi 1:20).

Zaidi ya hayo, Maandiko inaonyesha kwamba Mungu ameweka uthibitisho wake katika asili (Zaburi 19:1) na atamjibu yeyote anayemtafuta (Mathayo 7:7-8). Biblia inaelezea jinsi nia ya mtu daima inashinda ushahidi: mtu anapaswa kutaka kujua ukweli kabla ya ushahidi au mantiki kuleta tofauti yeyote (Yohana 7:17). Hakuna kiasi cha ushahidi kinachoweza kumshawishi mtu ambaye ni kinzani (Luka 16:19–31), na jinsi mtu anavyozidi kudai kuwa “anataka ushahidi zaidi,” ndivyo anavyothibitisha kwamba hakuna ushahidi utakaotosha (Mathayo 12:39).

Uzoefu unaunga mkono mafundisho ya Biblia kuhusu suala hili. Mantiki na uzoefu hufanya liwe jambo la busara kusema kwamba hakuna kitu kama “mtu asiyepinga uwepo wa Mungu”. Sambamba na hili ni watu wanaodai kwamba dunia ni tambarare.

Watu fulani katika ulimwengu wanaisistiza kwamba dunia ni tambarare. Licha ya ngano zinazopinga, wanadamu kwa ujumla walijua kwamba dunia ni duara muda mrefu kabla Christopher Columbus. Ushadili wa alisi uliopatikana katika siku za waandishi wa Agano la Kale na wanafalsafa wa Kigiriki ulikua wa moja kwa moja na ulizingatiwa na kutafsiriwa. Wale wanaozingatia hoja ya kutoka ukafiri dhidi ya Mungu wangesita kudai kwamba wanaoshikilia kwamba dunia ni tambarare “wako wazi” kuamini katika sayari ya duara. Au kwamba kuna uwezekano wa wao kubadili mawazo yao pindi wanapopewa ushahidi. Uwezekano huo unaweza kuwa kweli katika nadharia lakini sio kwa vitendo.

Licha ya madai ya kibinafsi ya “unyoofu,” uzoefu unaonyesha kwamba imani ya kwamba dunia ni tambarare inahitaji kiwango fulani cha nia ya makusudi. Ukweli fulani unapaswa kupuuzwa au kugeuzwa juu chini. Katika maneno mengine, anayeshikilia kwamba dunia ni tambarare ambaye anadai kukubali ushahidi basi hayuko“wazi.” Hata akipewa ushahidi mwingi, anayeshikilia imani ya dunia tambarare basi yeye hukataa na kupuuza.

Zaidi ya hayo, mantiki inaonyesha kwamba kuwepo kwa anayeshikilia kuwa dunia ni tambarare ilhali hana maarifa haiwezi kuthibitisha kwaba dunia ni tambarare. Hii inafichua msingi wa watu wa uwongo wa hoja ya kutoka kwa kutoamini: kwamba Mungu lazima atoe kiwango fulani cha ushahidi kulingana ratiba fulani. Msingi huu umeshindwa kwa sababu umejikita katika tatizo lile lile linalosababisha ukafiri: dhana kwamba Mungu lazima afanye kama vile kafiri angefanya. Mtu anaweza kuwa mkweli, na mkweli katika makosa; Mungu hatakiwi kuzingatia matakwa ya binadamu anayoweka.

This is not to say that conversion—either for flat-earthers or atheists—is impossible. But, in almost every case, converted atheists admit that at least part of their problem was a deliberate unwillingness to

Hii haimaanishi kwamba uongofu wa -wanaoamini kwamba dunia ni tambarare au makafiri hauwezekani. Lakini katika karibu kila kisa, makafiri wanaobadilika wanakubali kwamba sehumu ya tatizo lao ilikuwa kutotaka kuamini kimakusudi. Wanatambua ukweli kwamba walikuwa wanaruhuru ubaguzi na upendeleo kutupilia mbali ushahidi. Nukuu kutoka kwa makafiri maarufu zimejaa hisia, woga na kukiri moja kwa moja hawataki Mungu awe halisi. Hii ndiyo sababu mabishano ya hisia ndiyo yanaoongoza katika kupinga uwepo wa Mungu.

Zaidi ya hayo, tuna ushahidi wa aina nyingi wa kuwepo kwa Mungu. Ushahidi huu unasaidia katika kukanusha hoja ya kutoka kwa ukafiri. Ikiwa Mungu hajatoa ushahidi “wa kutosha” kwa mtu mnyoofu, makafiri waliobadilika wanaodai kwamba ushahidi uliwaongoza katika uongofu wana waliitikia mwito gani? Utetezi pekee unaowezekana wa hoja kutoka kwa ukafiri, katika wakati huo, ni kuhoji kwa mzunguko, ikidai kwamba wakanamungu wa awali walidanganyika, huku wasio-waumini sugu wakiwa si wepesi kudanganyika, ufafanusi kila uchao unazidi ukibadilika katik ukweli wake na ushahidi.

Zaidi ya hayo, akili ya kawaida inasema kwamba baadhi ya watu wanaodai kwamba sasa hawaoni uthibitisho wa kutosha wa kuwako kwa Mungu watageuka wakati fulani wakati ujao. Ikiwa hoja kutoka kwa kutokuamini ina maana yoyote, uongofu kama huo ungemaanisha kwamba Mungu kwa kweli yuko. Hapo tena, asiye muumini atalazimika kutumia aina fulani ya hoja ya ”Not True Scotsman” bishano au ulaghai mwingine ili kukwepa mantiki ya msimamo wake mwenyewe.

Maandiko na uchunguzi rahisi unaonyesha kwamba misingi yote miwili mikuu ya hoja kutoka kwa kutoamini ni ya uongo. Watu hawaelekei kuwa na akili timamu, na walo la Mungu si dogo. Suala la kuwepo kwa Mungu lina maana kubwa ya kibinafsi, kwa hiyo hakuna sababu ya kuamini kwamba mtu yeyote anaweza kulitazama kwa njia isiyo na maana. Sio busara kudai kwamba sababu pekee ambayo ni wa nini mtu fulani hajasadikishwa juu ya kuwepo kwa Mungu ni kwamba Mungu hakumpa yeye, kibinafsi Ushahidi wa kutosha. Hiyo sio tofauti sana na wale wanao iona ardhi kuwa tambarare ambao husema vivyo hivyo.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, hoja ya kutoka kwa ukafiri ni nini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries