settings icon
share icon
Swali

Historia ya Ukristo ni gani?

Jibu


Historia ya Ukristo ni kweli na ni historia ya ustaarabu wa Magharibi. Ukristo imekuwa na ushawishi mwingi katika jamii kwa ujumla - sanaa, lugha, siasa, sheria, maisha ya familia, tarehe ya kalenda, muziki, na njia hasa tunafikiri sote zimerembeshwa na ushawishi wa Kikristo takribani milenia mbili. Hadithi ya Kanisa, ni muhimu moja kujua.

Mwanzo wa Kanisa
Kanisa ilianza siku 50baada ya ufufuo wa Yesu (c. AD 35). Yesu aliahidi kwamba angelijenga kanisa lake (Mathayo 16:18), na kwa ujio wa Roho Mtakatifu siku ya Pentekoste (Matendo 2:1-4), kanisa - ekklesia ( "kuitwa toka kwa mkusanyiko") – ilianza rasmi. Watu elfu tatu waliitikia hotuba ya Petro siku hiyo na kuchagua kumfuata Kristo.

Waumini wa awali wa Ukristo walikuwa Mayahudi au waongofu kwa Wayahudi, na kanisa lilikuwa katika Yerusalemu. Kwa sababu hiyo, Ukristo ulionekana kwanza kama dhehebu la Wayahudi, sawa na Mafarisayo, Masadukayo, au Waeseni. Hata hivyo, chenye Mitume walikihubiri mara kwa kiasi kikubwa ni tofauti na yale makundi mengine ya Wayahudi walikuwa wakifundisha. Yesu alikuwa Masihi wa Wayahudi (Mfalme mtiwa mafuta) ambaye alikuja kutimiza sheria (Mathayo 5:17) na kuanzisha agano jipya msingi wa kifo chake (Marko 14:24). Ujumbe huu, na malipo yake kwamba walikuwa wamemuuwa Masihi wao wenyewe, kukasirisha viongozi wengi wa Wayahudi, na baadhi, kama Sauli wa Tarso, alichukua hatua ya kukomesha "Njia" (Matendo 9:1-2).

Ni sahihi kabisa kusema kwamba Ukristo una mizizi yake katika Uyahudi. Agano la Kale liliweka msingi kwa ajili ya Agano Jipya, na ni vigumu kuelewa Ukristo bila maarifa ya kazi ya Agano la Kale (angalia vitabu vya Mathayo na Waebrania). Agano la Kale linaelezea umuhimu wa Masihi, lina historia ya watu wa Masihi, na linatabiri kuja kwa Masihi. Agano jipya, lote basi, linahusu kuja kwa Masihi na kazi ya kutuokoa sisi kutoka katika dhambi. Katika maisha yake, Yesu alitimiza zaidi ya unabii 300 maalum, kuthibitisha kwamba yeye ndiye Agano la Kale lilitarajia.

Ukuaji wa Kanisa la Kwanza
Si muda mrefu baada ya Pentekoste, milango ya kanisa ilifunguliwa kwa mashirika yasiyo ya Kiyahudi. Mhubiri Filipo alihubiri kwa Wasamaria (Matendo 8:5), na wengi wao waliamini katika Kristo. Mtume Petro alihubiria watu wa mataifa mengine katika nyumba ya Kornelio (Matendo 10), na wao, pia, walipokea Roho Mtakatifu. Mtume Paulo (mtesa kanisa wa zamani) alieneza Injili duniani kote hekaya za Kirumi, na kufikia hata Roma yenyewe (Matendo 28:16) na pengine hadi Hispania yote.

kufikia 70 AD, mwaka Yerusalemu iliharibiwa, wingi wa vitabu vya Agano Jipya vilikuwa vimekamilika na vilikuwa vinazunguka katika makanisa. Kwa miaka 240 baadaye, Wakristo waliteswa na Roma wakati mwingine na mtu yeyote, wakati mwingine kwa amri ya serikali.

Katika karne ya 2 na 3, uongozi wa Kanisa ukawa zaidi na zaidi wa vyeo idadi ilipoongezeka. Uzushi kadhaa uliwekwa wazi na kukemewa wakati huu, na Kanoni ya Agano Jipya ilikubalianwa. Mateso yaliendelea kuimarishwa.

Kujipuka kwa Kanisa la Kirumi
Katika AD 312, Constantine Mfalme wa Kirumi alidai kuwa alikuwa na uzoefu kubadilika. Kuhusu miaka 70 baadaye, wakati wa utawala wa Theodosius, Ukristo ukawa dini rasmi ya Dola ya Kirumi. Maaskofu walipewa maeneo ya heshima katika serikali, na kufikia AD 400, maneno " Roma" na "Mkristo" yalikuwa yenye maana sawa.

Baada ya Constantine, Wakristo hawakuteswa tena. Baada ya muda, ni makafiri waliingia chini ya mateso isipokuwa "waongofu" kwa Ukristo. Ubadilisho huo wa kulazimishwa ulisababisha watu wengi kuingia kanisa bila mabadiliko ya kweli ya moyo. makafiri walileta sanamu zao, na mazoea yao walikuwa wamezoea, na kanisa ilibadilisha, picha takatifu, usanifu iliofafanuliwa, Hija, na heshima ya watu waliochukuliwa kuwa watakatifu aliongezwa kwa ya ibada ya kanisa la kwanza. Kuhusu wakati huu huo, baadhi ya Wakristo walijitoa kutoka Roma, kuchagua kuishi katika maisha ya kujitenga kama watawa, na ubatizo wa watoto wachanga ulianzishwa kama njia ya kuosha dhambi mbali ya awali.

Katika karne iliyo fuata, halmashauri mbalimbali za kanisa zilifanyika kwa jaribio la kuamua mafundisho rasmi ya kanisa, kwa kupiga marufuku ukiukwaji wa ukarani, na kufanya amani kati ya pande zinazopigana. Kama Dola ya Kirumi ulizidi kuwa hafifu, kanisa ikawa na nguvu zaidi, na kutoelewana kwingi kukazuka kati ya makanisa katika nchi za Magharibi na wale walio katika Mashariki. Magharibi (Kilatini) kanisa, mjini Roma, ilidai mamlaka ya kitume juu ya Makanisa mengine yote. Askofu wa Roma alikuwa hata imeanza kujiita "Papa" (Baba). Hii haikuwapendeza vizuri kanisa la Mashariki (Kigiriki), mjini Constantinople. Theolojia, siasa, kiutaratibu, na lugha zilichangia katika mgawanyiko wote wa upinzani Mkuu katika mwaka wa 1054, ambayo Kanisa Katoliki ("Kila mahali") na Kanisa la Mashariki zilitengana kila mmoja na kuvunja mahusiano yote.

Zama za Kati
Katika Enzi za Kati katika Ulaya, Kanisa la Katoliki liliendelea kushikilia nguvu, na mapapa wakidai mamlaka juu ya ngazi sote za maisha na kuishi kama wafalme. Rushwa na tamaa katika uongozi wa kanisa ilikuwa kawaida. Kutoka 1095-1204 mapapa walipitisha mfululizo wa umwagaji damu na mikutano ghali katika jitihada za kurudisha kudidimiza maendeleo ya Waislamu na kuukomboa mji wa Yerusalemu.

Matengenezo
Kwa miaka mingi, watu kadhaa walijaribu kuangazia matumizi mabaya ya Kanisa la Roma haki za kiteolojia, kisiasa, na binadamu. Wote walikuwa kimya katika njia moja au nyingine. Lakini katika 1517, mtawa wa Ujerumani aitwaye Martin Luther alichukua msimamo dhidi ya kanisa, na kila mtu alisikia. Kupitia Luther kukatokea mageuzi ya Kiprotestanti, na Zama za Kati zikafika kikomo.

wageuzi, wakiwemo ni pamoja na Luther, Calvin, na Zwingli, walitofautiana katika hoja nying za teolojia, lakini wao waliendelea kusisitiza katika ya mamlaka ya Biblia juu ya mila za kanisa na ukweli kwamba wenye dhambi huokolewa kwa neema kwa njia ya imani pekee mbali na kazi (Waefeso 2:8-9).

Ingawa Ukatoliki ulipata nguvu tana katika Ulaya, na mfululizo wa vita kati ya Waprotestanti na Wakatoliki uliotokea, mabadiliko yalikuwa na mafanikio kubomoa nguvu ya Kanisa ya Katoliki na kusaidia kufungua mlango wa umri wa kisasa.

Umri wa Umisheni
Kutoka 1790-1900, kanisa ilionyesha nia isiyokuwa ya kawaida katika kazi ya utume. Ukoloni na alipofumbua macho na haja ya umisheni, na viwanda uliwapa watu uwezo wa kifedha kukimi wamisionari . Wamisheni walienda duniani kote kuhubiri injili, na makanisa yalianzishwa duniani kote.

Kanisa ya kisasa
Hii leo, Kanisa la Katoliki na la Mashariki Kanisa wamechukua hatua ya kurekebisha uhusiano wao uliovunjika, kama vile Wakatoliki na Walutheri wamefanya. Kanisa la kiinjili limejitegemea na kukita mizizi imara katika theolojiaya ugeuzi. Kanisa pia limeona ongezeko la Kipentekosti, harakati charismati umbwembwe, mabaraza, na ibada dini mbalimbali sisizo za kweli.

Nini Sisi hujifunza kutokana na historia yetu
Kama sisi hatujifunzi kitu kingine kutoka historia ya kanisa, tunapaswa angalau kutambua umuhimu wa kuruhusu "neno la Kristo likae ndani yetu kwa wingi" (Wakolosai 3:16). Kila mmoja wetu ana wajibu wa kujua ni nini maandiko yanasema na kuishi kwa hilo. Wakati kanisa husahau yale ambayo Biblia inafundisha na kupuuza yale ambayo Yesu alifundisha, machafuko utawala.

Kuna makanisa mengi leo hii, lakini injili ni moja tu. Ni "imani waliyokabidhiwa watakatifu mara moja tu" (Yuda 3). Na tuwe macho kwa kuhifadhi imani na kupitisha kwa wengine bila mabadiliko, na Bwana ataendelea kutimiza ahadi yake ya kujenga kanisa lake.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Historia ya Ukristo ni gani?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries