settings icon
share icon
Swali

Kwa nini Mungu aliwachukua Henoko na Eliya Mbinguni bila wao kufa?

Jibu


Kulingana na Biblia, Henoko na Eliya ndio watu wawili pekee ambao Mungu alichukua mbinguni bila kufa. Mwanzo 5:24 inatuambia, " Henoko akaenda pamoja na Mungu, naye akatoweka, maana Mungu alimtwaa." Wafalme wa pili 2:11 inatuambia, "... ghafla kukatokea gari la moto na farasi wa moto , likawatenga wale wawili, naye Eliya akaenda mbinguni kwa kimbunga." Henoko anaelezewa kama mtu ambaye "alitembea pamoja na Mungu kwa miaka 300" (Mwanzo 5:23). Eliya labda alikuwa Nabii mkuu wa Mungu katika Agano la Kale. Pia kuna unabii wa kurudi kwa Eliya (Malaki 4: 5-6).

Kwa nini Mungu aliwachukua Henoko na Eliya? Biblia haijat upa jibu mahsusi. Wengine wanasema kuwa walichukuliwa katika maandalizi ya jukumu katika nyakati za mwisho, labda kama mashahidi wawili katika Ufunuo sura ya 11: 3-12. Hii inawezekana, lakini haijafundishwa wazi katika Biblia. Inawezekana kwamba Mungu alipendelea kuokoa Henoko na Eliya kutokana na kufa kwa sababu ya uaminifu wao mkubwa katika kumtumikia na kumtii. Kwa hali yoyote, Mungu ana lengo lake, na wakati hatujui mipango na makusudi ya Mungu, tunajua kwamba "Njia yake ni kamilifu" (Zaburi 18:30).

English


Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kwa nini Mungu aliwachukua Henoko na Eliya Mbinguni bila wao kufa?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries