settings icon
share icon
Swali

Je, kutakuwa na hekalu la mwisho katika Yerusalemu?

Jibu


Biblia inasema kwamba matukio ya nyakati za mwisho yatatokea katika hekalu huko Yerusalemu (Danieli 9:27; Mathayo 24:15). Waraka wa Pili wa Wathesalonike 2: 4, inazungumzia juu ya Mpinga Kristo, inatuambia, " yule mpingamizi, ajiinuaye nafsi yake juu ya kila kiitwacho Mungu ama kuabudiwa; hata yeye mwenyewe kuketi katika hekalu la Mungu, akijionyesha nafsi yake kana kwamba yeye ndiye Mungu." Kabla ya baadhi ya matukio ya nyakati za mwisho hutokea, hekalu lazima liwepo huko Yerusalemu. Hili litakuwa hekalu la tatu-ya kwanza lilikuwa la Suleimani; na la pili lilikuwa la Zerubabeli, baadaye kupanuliwa na Herode.

Bado kuna shida "ndogo" ya ile ema ya Kiislam ya Mwamba ambayo iko mahali kwenye hekalu la Kiyahudi linapaswa kuwa. Waislamu wanaamini hapa ndiyo mahali ambapo Muhammad alipanda kwenda mbinguni, akaufanya kuwa takatifu sana katika makabila ya Kiislamu. Kutokana na hali ya leo ya kisiasa, haiwezekani kwamba Wayahudi wangeweza kuchukua nafasi hii na kujenga hekalu huko. Lakini, kabla au wakati wa dhiki, hekalu litajengwa, labda kama matokeo ya agano la Mpinga Kristo na Israeli (Danieli 9: 24-27).

Ujenzi wa hekalu la Kiyahudi itakuwa dalili ya uhakika kwamba unabii wa nyakati za mwisho unatimizwa. Lotakuwa hekalu la wakati wa dhiki ambalo Mpinga Kristo atastahili na "chukizo lake linalosababisha uharibifu," ambalo linalotajwa na Kristo katika Marko 13:14. Unyakuo ungeweza kutokea wakati wowote-sio lazima ujenzi wa hekalu ufanyike kwanza-hivyo ni muhimu kuwa tayari.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, kutakuwa na hekalu la mwisho katika Yerusalemu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries